Gwajima Kwanini hukuogopa?1SAMWELI1:14-16
Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa Bwana.
Kwa desturi wayahudi mtu awezi kuitwa masihi hadi amwagiwe mafuta na ndiomaana walimkataa Yesu kwasababu alijiita Kristo masihi wa Bwana uungu wa Mungu juu ya mwadamu mwanadamu anakuwa ana vipande viwili uwanadamu wake na uungu ulioko ndani yake, kwenye agano la kale mtu alitakiwa amwagiwe mafuta ndipo aitwe masihi wa Bwana na kwenye agano jipya mtu mpaka ajazwe Roho mtakatifu na Yesu alipobatizwa lilishuka wingu zito kutoka juu na sauti ikasikika na kitendo hicho ni kumwagiwa roho mtakatifu kwa namna ya rohoni.
Huyu kijana alipo muua sauli alienda kwa Daudi akiwa na furaha kwamba alimuulia adui wake lakini Daudi akamuua kwasababu alimuua masihi wa Bwana. Sauli alikuwa amerudi nyuma lakini Mungu alimuona kama masihi wake na Daudi naye alilifahamu hilo. Sauli hakuuwawa na yule kijana bali alitaka sifa ili Daudi ampongeze na asheherekee lakini alimkuta amekwisha kufa.
Zaburi105:15
Kama kinywa chako kinawasema vibaya masihi wa Bwana utapata laana sio vizuri.
Dada yake na Musa alikuwa anaitwa Miriam alishughulika kwenye kumficha Musa.
Hasabu12:1-
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena. Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.
Watu hawawi watumishi wa Mungu kwasababu wametaka bali ni kwasababu Mungu amewachagua wawe wakati mwingine safari ya kiroho ya mtu inaweza kukwama kwasababu ya kuwasema watumishi wa Bwana.
Gwajima twakubalina na mengi lakini kwa hili umechemka ndo maana hata kuna wakati unawalazimisha watu kupiga makofi,umesahau kuwa makofi ni hiari ya mtu na hutolewa kama zawadi tena kwa moyo wa kupenda Bwana akurudie katika hili
Yawezekana kweli Pengo amekosea kama Mfalme sauli alivyokosea lakini kwani hukufanya kama Daudi?Kwanini hukuogopa ee Gajima usiye na akili ni nani aliyekuloga?
Gwjima umesahau kuwa Pengo uliyediriki kumwita mpumbavu mmoja ni Baba wa Watoto wengi na ambao wengi wao ndio wanaotoa fungu la kumi kanisani kwako na kukufanya ndani mwako izaliwe jeuri ya kiwango hicho?ikowapi hekima yako?upo wapi uvumilivu wako?ahaaa Gwajima umesahau kwamba sote tu viongo katika mwili wa Kristo?tena umesahau kuwa imeandikwa mtu akikosea mrejesheni kwa upendo na upole?
Imeniuma kwa sababu nakuamini na nimekuwa nikiwapa sana watu habari zako na jinsi unavyoutumika kueneza Ufalme wa Kristo Duniani lakini imekuwa kinyume chake baada ya wao kupata clip hii ya kwako wamenidharau na kunitukana
Asante kwakunilipa mabaya