Hawa ni watu wakubwa (viongozi waliotoa matamko), wamekabidiwa madaraka makubwa katika kanisa na hatuwezi kuyapuuza kwa sababu yametolewa baada ya tafakari kubwa. Jambo ambalo ningependa kila moja wetu atambue ni hili; kwamba matamko yote mawili yanaashiria mgawanyiko wa taifa letu, kati ya wakrtisto na wasiokuwa wakristu, hilo lazima tulitambue na tutambue kwamba matamko haya yanaweka Jumuhiya ya Wakristu dhini ya serikali ya nchi yetu ya Tanzania. Haya mambo mawili lazima tuyatambue wakati tunasoma matamko haya
Nikiwa katika hali hii ta ukamilifu nililetewa nakala hii iliyopo hapa mbele yangu, nikaulizwa je, isomwe katika makanisa ya maparokia zote katika Jimbo Kuu la Dar es salaam? Nikasema mimi ni nani kupinga jambo ambalo limeshatamkwa na maaskofu wote. Kwa nini nizuie, hata nikizuia yamechapwa katika magazeti na yatachapwa katika magazeti. Kwa nini nizuie waamini wakatoliki katika parokia zao wasijue haya yaliyoandikwa, sina sababu.
Lakini nililonalo ambalo ni muhimu kwangu kama mchungaji ni kutoa maoni yangu mbele yenu kuhusu barua zote hizi mbili. Barua zote mbili kama nilivyosema zimetengenezwa kutokana na umakini wa hali ya juu, lakini sisi maaskofu hatuna mamlaka ya kulazimisha wakristo au waamini pamoja na watu wengine wenye mapenzi mema, hatuna mamlaka kamwe ya kuwalazimisha watende kitu kinyume cha dhamiri yao, hiyo ni msimamo hakika kabisa na haiwezekani mtu akaja kwangu akaupinga. Tungekuwa na mamlaka hayo tukawa tumeyapokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tungemwuliza mwenyezi Mungu kwa nini hujatumia mamlaka hayo watu wanandelea kutenda madhambi na wewe unawatazama.
Mwenyezi Mungu anatuacha kama wanadamu tuweze kulinda dhamili zetu na tutende kulingana na dhamiri hizo machoni pa mwenyezi Mungu kiasi kwamba tunaweza kufanya madhambi mbele ya mwenyezi mungu na mwenyezi mungu hatupigi kwa radi. Ni muhimu kwa mwanadamu machoni pa Mwenyezi Mungu atende kulingana na dhamiri yake jinsi mwenyezi Mungu jinsi anavyoamini mwenyezi Mungu anavyomwelekeza. Hilo ni neno la muhimu kabisa.
Pamoja na tafakari nzuri kabisa na mawazo makini yaliyotolewa katika barua hizi, kufikia hatua ya kumwambia kila mkristo katika lile tamko la jukwaa la wakristu kusema itakapofika siku ya kupiga kura kuhusu mapendekezo ya katiba twende kwa moyo mmoja na kila mmoja apige kura ya hapana, sijui kwa kiasi gani tunaheshimu dhamiri za waumini wetu. Kuwaambia sisi kama maaskofu tunasema mwende mkapige kura ya hapana. Na kwanini tuwafanye hivyo waamini wetu, tuwageuzi ni watoto wadogo ambao lazima kuwaambia lazima mwende mkapige kura ya hapana. Hilo ni jambo ambalo linadhalilisha uhuru wa wana wa Mungu ndani ya waamini wetu.
Hatuna uwezo wala hatuna haki ya kuwaambie mwende mkapige kura, lakini kura hiyo iwe ya hapana. Na kwanini hiyo hivyo, je waamini wetu ni watoto wadogo wasioweza kufikiri na kutafakari wenyewe kiasi kwamba tuwaambie nendeni mkapige kura ya hapana. Tumepata wapi haki hiyo, tumeipata wapi haki hiyo? Hilo ni swali muhimu sana.
Kwa matamko haya mawili narudia tena kusema, pamoja na umakini wake lengo au tukio la mwisho ni kwamba linagawa taifa lete kati ya wakristu na wasiokuwa wakristu. Matokeo yake tunaweza kuyafikiria sisi wenyewe. Vile vile linagawa wakristu kutoka kwa serikali yao jambo ambalo kwa kweli haliwezekani. Ndani ya serikali yetu ya Tanzania katika uonogozi wake wapo waumini wetu wakatoliki na wako waamini wakristo ambao ukisimama na kuwaambia serikali au kanisa linasimama dhidi ya kanisa ni kuwaambia nyinyi pia tunasimama kinyume chenu. Sasa sijui hao viongozi wanaokuww wakristu na wanaokuwa wakatoliki wafanye nini, waasi imani yao, wasimame upande wa serikali au watoke serikali wasimame upande wa imani yao, wachague lipi katika hayo.na kuna sababu ya kufanya uchaguzi wa ain hiyo.
Mama zangu niruhusu barua hii isomwe makanisani, lakini ni wajibu wangu kueleza reservations zangu, ni wajibu wangu kuwafanya kila mnalosoma liwe limetoka kwa askofu au kwa mtu mwingine yeyote mlisome mkijua kwamba mmepewa na mwenyezi Mungu ile nafasi ya ndani ya moyo wenu haiwezi kuguswa na yeyote na mwenyezi ametuacha huru hata yeye hagusi kwa maana ya kusema kutulazimisha kusema kitu.
Angekuwa analamisha anauwezo wote mbona wote hapa tungekuwa malaika, ila anatuheshimu na anatuacha kama tulivyo na kuturuhusu tutende kutokana na maamuzi yetu. Hilo siwezi kusema mbele ya mtu yeyeto kwamba najutia kulitamka hilo, siwezi nikajutia kwa sababu ninalitamka kulingana na msimamo kamili wa kanisa, tena kanisa katoliki kwamba kila muamini pamoja na kwamba anaweza kusikia maoni kutoka kwa watu mbalimbali hatuwezi kufikia hatua ya kufikia kusema nenda kapige kura ya hapana, hakuna mtu aliye na uwezo wa kumwambia mwingine akapige kura ya hapana, hakuna mwadadamu aliye na uwezo huo. Kama mungu mwenyewe hafanyi hivyo, mwanadamu anayapata wapi madaraka hayo