Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Kwanza mkuu naomba nikusahihishe, Pengo sio mkuu wa kanisa katoliki Tanzania na wala cheo hicho hakipo.

Pengo ni askofu mkuu wa jimbo la Dsm na mamlaka yake yanaishia Dae es salaam, Pengo ni sawa tu na askofu mkuu wa Dodoma, Mtwara au Shinyanga, Kadinali maana yake, ni mkatoliki ambaye ana fursa ya kwenda Vatican kushiriki uchaguzi wa Papa, si zaidi ya hapo, Kadinali anaweza hata akawa hajaufikia uaskofu, Historia inaonyesha watu makadinali ambao walikuwa hata hawajafikia hata hatua ya upadri.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, Pengo amejishushia sana heshima kwa sababu ya undumilakuwili na kuonekana ni kama anayejipinga mwenyewe. Yeye ni sehemu ya baraza la maaskofu katoliki(TEC)amesaini waraka huo wa jukwaa la wakristo na ameruhusu usomwe makanisani katika jimbo lake, je, anapokuja leo kuponda waraka huo jamii imweleweje?

Yeye anasema kuwa haipaswi kuwaamlia wananchi wapige kura ya hapana, yeye anavyotaka wapige kura ya ndiyo sio kuwaamria wananchi?
Kanisa limetimiza wajibu wake wa kutoa wosia wa kinabii juu ya nini jamii inachotakiwa kufanya, je Pengo si sehemu ya kanisa?
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani. Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo. Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.
 
aidha pengo alipata ngao wa escrow au ana hisa kwenye benki ya mkombozi vinginevyo hana sababu yoyote ya msingi ya kuitetea katiba ya akina samwel sita, chenge na ngeleja
 
Mahakama ya kadhi nimeiweka kwenye kifungu cha peke yake kabisa ktk post yangu. Haihusiani na katiba pendekezwa na CCM, nadhani umeshindwa kunielewa kijana.

Ungefungua thread yako basi usiharibu topic hapa..
 
Pengo hastahili kutukanwa kama gwajima alivyofanya!! Kama MUNGU angekuw anatuadhibu pale tunapokoseq sidhani kama duniani pangekalika ila yeye gwajima anaeneza neno la Mungu kakosea sana!!!
 
Sasaa, mahakama ya kadhi kiukweli kwa sisi tuliyoisoma katiba pendekezwa hamnaa mahala imeandkiwa, alafu kwa kuwasaidia tu wale ambao wanafikiri hii nchi ni yakidini basi waitafute katiba pendekezwa waisome
 
Kwanza mkuu naomba nikusahihishe, Pengo sio mkuu wa kanisa katoliki Tanzania na wala cheo hicho hakipo.

Pengo ni askofu mkuu wa jimbo la Dsm na mamlaka yake yanaishia Dae es salaam, Pengo ni sawa tu na askofu mkuu wa Dodoma, Mtwara au Shinyanga, Kadinali maana yake, ni mkatoliki ambaye ana fursa ya kwenda Vatican kushiriki uchaguzi wa Papa, si zaidi ya hapo, Kadinali anaweza hata akawa hajaufikia uaskofu, Historia inaonyesha watu makadinali ambao walikuwa hata hawajafikia hata hatua ya upadri.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, Pengo amejishushia sana heshima kwa sababu ya undumilakuwili na kuonekana ni kama anayejipinga mwenyewe. Yeye ni sehemu ya baraza la maaskofu katoliki(TEC)amesaini waraka huo wa jukwaa la wakristo na ameruhusu usomwe makanisani katika jimbo lake, je, anapokuja leo kuponda waraka huo jamii imweleweje?

Yeye anasema kuwa haipaswi kuwaamlia wananchi wapige kura ya hapana, yeye anavyotaka wapige kura ya ndiyo sio kuwaamria wananchi?
Kanisa limetimiza wajibu wake wa kutoa wosia wa kinabii juu ya nini jamii inachotakiwa kufanya, je Pengo si sehemu ya kanisa?

Mkuu nafahamu vinzuri sana majukumu ya ukardinali, na ninajua wale makardinali wasio maaskofu eneo lao la kazi linakuwa ni Vatican. Lakini pia unapaswa kufahamu uwepo wa Kardinali unamaanisha nini. Majukumu ya Pengo yanaisha Dar es salaam katika muonekano wa uaskofu mkuu wa jimbo kuu Katoliki la Dar es salaam, ila katika muonekano wa ukardinali majukumu yake ni Tanzania nzima. Pia ni kweli Pengo si mwamuzi wa mwisho wala hayupo juu ya TEC, ila nafasi yake ya ukardinali inampa heshima katika maamuzi yoyote yanayopaswa kutolewa na TEC.

Tukija kwenye ishu ya kupiga kura, sidhani kama upo sahihi kusema Kardinali Pengo alishiriki mazungumzo hayo yaliyofanyika Arusha, mwadhama alikuwa India kwenye matibabu na alivyorudi alikuta tayari wameshaandika tamko lao na magazeti yameshaanza kuandika sasa yeye kama yeye hakuweza kuzuia usisomwe kwa sababu hayupo juu ya mamlaka ya TEC. Lakini kusomwa huko hakumzuii yeye kutoa maoni yake, ufafanuzi na msingi wa Kanisa Katoliki. Nikujulishe tu kuwa, katika mahubiri yake hakuna sehemu hata moja aliyowaambia waumini wakapige kura ya NDIYO, hakuna. Kama hukusikiliza mahubiri yake, nimeattach audio hapa chini uisikilize maana usije ukawa unamtuhumu kitu ambacho hakukisema.
 
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani. Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo. Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.

Kwa hiyo maaskofu woooteee hawana akili ila yeye peke yake? Maamuzi ya kikao na maamuzi ya mtu mmoja yepi yana weight?
 
Gwajima asamehewe hajui atendalo amejipotezea umaarufu kwa waumini wake sisi RC tumejifunza kusamehe na hasa mtu kama Gwajima anataka kuharibu hali ya hewa nimemsikiliza nimeshindwa kuamini ni yeye au mtu kaigiza sauti yake yeye hajui mabaya yake
 
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani. Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo. Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.

Umekuwa mkiwa kaka pole!? kusema anachokiamini sawa lakini alitakiwa azisome alama za nyakati, unaposema fikira zako ambazo haziendani na "General mood ya Waumini/wananchi, utapewa kavukavu za uso Kama hizi za Gwajima, Pengo kajimaliza, nadhani anataka kuhamia ACT kwa Mayuda Iskariot wenzie, kwa kuwa alijua hawezi kuzuia waraka usomwe maparokiani, basi busara alitakiwa kunyamaza kimya bila kwenda public, kufanya kazi Kama Kova kumemponza, imagine Cardinal mzima anakashfiwa hadharani kiasi hiki!? pole kaka
 
kwahio ndio imehalalisha askofu gwajima mtumishi wa Mungu kutoa matusi hayo tena mbele ya madhabahu???

Mkuu umesahau kale kamsemo maarufu.."Ukiwa unaishi nyumba ya vioo kamwe usithubutu kuwarushia mawe wanaokuzunguka"...
 
kweli pengo kakosea lakini nazani gwajima kajidhalilisha zaidi
Hata mimi naona hivyo. Ni afadhali Pengo aliongea kwa upole tena akiwa neutral, wala hakusema muipigie katiba kura ya NDIYO, bali alisema watu waamue wenyewe (kupiga NDIYO au HAPANA). Huyu Gwajima nimemdharau zaidi kwani kuongea maneno hayo madhabahuni inatia shaka kama anamtumikia Kristu. Bado nasita kuamini kama ni Gwajima kaongea hayo
 
sipati picha kama hayo maneno ya gwajima angeyasema Pengo!!
 
Back
Top Bottom