Ndugu yangu fazili.
Kwanza hongera kwa uzi wako lakini kwa kua hapa ni jamvi huru labda naomba nioanishe mawazo yangu na yako lakini kwa utofauti pengine wa kimtazamo.
Nimesikiliza kwa makini audio ya pengo na gwajima na kutafuta mantiki ya kitu ulichoandika, lakini nasikitika kusema kwamba sijaona kosa wala tatizo gwajima alilofanya na kwaupande wa matusi hakuna tusi lolote maana upuuzi ni "hali" ya kufanya jambo ambalo unafahamu si sahihi.
Nadhani pengine umeguswa na neno hilo na ujasiri wa gwajima kuyasema haya mbele ya umati wa wafuasi wake pamoja na kujua anarekodiwa, ikumbukwe hata maandiko yameinajisisha dhambi ya unafiki (japo sikumbuki kitabu mtanisaidia wanatheolojia),sasa ni wengi wanaofahamu kua pengo ameteleza kwa kutoa tamko tofauti ama kinyume na makubaliano ya baraza la maaskofu Tanzania na hii ndo sababu kubwa ukisikiliza kwa makini hii audio ya gwajima analaumu usaliti uliofanywa na pengo wakati yalikua ni makubaliano ya mabaraza mbalimbali yakikristo na yy akiwa ni sehemu ya wajumbe(hata kama hakuwepo lakini aliwakilishwa).
Kama ilivyo pengo alitoa maoni lakini pia na gwajima ametoa maoni na nikuhakikishie bora gwajima alietoka hadharani kuliko baadhi ya maaskofu waliokaa kimya lakini wanakunywa na kula nae ila wanaumia na tamko la pengo.
Naomba niseme mimi si muumini wa katoliki na kadhalika gwajima lakini kama swala ni la uwazi na kimantiki sina budi kutoa mawazo yangu kwakusema gwajima yupo sahihi na pengine imewagusa wengi kwa sababu za kiudhehebu lakini vinginevyo namsifu gwajima kwa ushujaa alioonyesha na amesema kama pengo anaguswa na hili aende mahakamani lakini akaongeza kua malaika wamuombee ili arudi kwenye mstari wa kiuongozi maana amebadilika na kua msaliti.
Kwahaya machache nadhani hata mimi mawazo yangu utayaheshimu.