Ukiwa kwenye mfumo lazma uone maisha yako sawa maana uzembe hauna mashtaka awamu hii. Wizi umepewa baraka zote kwahio mtajenga sana, kununua sana mashamba kwa hela ya wizi.
Ishu ni kwa mtanzania ambaye riziki iko miguuni mwake. Hana bima wala support yeyote. Maisha hayawezi kuwa sawa
Hebu ngoja tuone hao wanaoitwa wanyonge kipindi Cha awamu iliyopita na hali zao ilikuwaje.
Wakulima:
Hili kundi halina bima na ridhiki yao ni jembe la mkono.
Asilimia almost 70% ya Watanzania wanajihusisha kwa namna Moja ama nyingine.
Lakini hali zao ziliboreka kipindi Cha awamu iliyopita?
Tuwatazame wakulima wa Korosho mikoa ya Pwani, Lindi,Mtwara na wilaya ya Tunduru.
Kabla serikari haijaingilia bei ya Korosho ilikuwa vizuri na wakulima waliita dhahabu nyeupe.
Lakini awamu ya tano ikaingia, tena mbaya zaidi ikatuma jeshi ndilo likusanye badala ya makampuni ya kigeni, matokeo yake,
Watu kudhulumiwa Korosho zao, vipigo kwa walanguzi na kushusha bei ya soko.
Kilimo Cha Mbaazi
Kilikuwa vizuri kilo ilienda mpaka 3000 na kunufaisha hawa wanyonge unao waits matokeo yake awamu ya tano ikaingiliwa, ikabiruga Soko na Mbaazi kushushwa mpaka 1000 kwa kilo.
Yaani muokota chupa za plastiki anapata pesa nyingi kuliko mkulima wa mbaazi, hebu fikiria kwa umakini.
Kilimo Cha Mahindi
Nani asiyejua bei ya pembejeo iliendelea kupanda kwa awamu iliyopita lakini bei ya mazao sokoni ilishushwa.
Wakati gharama ya kuhudumia shamba la mahindi ipo juu, Kuna mtu mmoja aliamua kuathiri chain nzima kwa kupiga marufuku masoko ya nje ambayo ni Kenya na Zambia.
Matokeo yake kaya masikini kule Sumbawanga na nyanda za juu kusini wakulima walikuwa wanapata hasara, kumbuka kule vijijini ndani ndani hutegemea kilimo hicho kuendesha maisha yao.
Hawakupunguziwa gharama za pembejeo za kilimo Wala kupewa chochote na serikari.
Kilimo Cha Nyanya
Waza mkoa wa Iringa na kitendo Cha kufungwa mipaka kilifanya Nyanya zishuke bei mpaka sado 500.
Je gharama za Nyanya, mbolea, mbegu, vibarua ilipungua?
Vipi wananchi wenye hali duni kule kilolo? Uliwafikiria?
Au hawa si wanyonge, labda Wana bima za kiasili kutoka kwa Mkwavinyika?
Mliaminishwa propaganda ambazo wachache walipata ukwasi usiomithilika na wengi mlikuwa bendera fuata upepo.
Vipi upotevu wa 1.5 Trillion ambazo CAG kazitaja kipindi Cha awamu iliyopita?
Vipi ununuzi wa Ndege kwa Cash ambazo value of money haionekani?
Kwenye Taifa masikini
Kwa nini sheria ya fedha, na budget ilikuwa haifuatwi?
Unajua kwenye ujenzi Kuna wizi mkubwa zaidi?
Kwa nini sheria ya manunuzi haikufuatwa?
Kwa nini Vijana wachache kina makonda na wenzie wakawa matajiri ghafra?
Kwa nini mabenki yalifilisika?
Kwa nini mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa merged?
*Acheni propaganda na uzalendo uchwara huku wachache wakifaidika
Je wamachinga aliwaundia sheria ya kuwalinda?
Aliboresha maslahi yao ya kazi?
Au ilikuwa kete ya kisiasa