Awamu ya Rais Samia ndiyo awamu iliyofeli kuliko awamu zote na kufanya wananchi kujutia zaidi uongozi huu

Awamu ya Rais Samia ndiyo awamu iliyofeli kuliko awamu zote na kufanya wananchi kujutia zaidi uongozi huu

Serikali dhaifu kupata kutokea toka Tz imeumbwa ni hii ya 6 sijui, ni kama mbwa koko!.
Serikali pekee iliyobariki upigaji, rejea Mama akiwaambia wasaidizi wake (Mawaziri) wale kwa urefu wa kamba zao shingoni!.
Et wale ila wasivimbiwe!.
 
Mimi naona ni awamu iliyo fanikiwa kuliko iliyopita.

Miradi mingi ya kimkakati imeanzishwa na mingine kumaliziwa ya awamu ya tano na ikiendelezwa vizuri.

Bei ya bidhaa kama Korosho , ufuta na Mbaazi kuimalika.

Biashara kuimalika

Ajira zinatangazwa na watoto wa masikini wanaajiriwa

Mzunguko wa pesa kuonekana

Uchumi wa mtu mmoja mmoja kuboreka na huduma za kifedha kuwa Bora zaidi hasa kibenki

Foreign direct Investment imeongezeka na viwanda vipya vinafunguliwa huko Mkuranga na Kibaha

Uboreshaji wa maslahi ya watumishi angalau kidogo

Uhuru wa mawazo na mikutano ya kisiasa umezidishwa

Wakulima angalau wanaona faida

Elimu ya juu pesa imeongezwa.
umesema kweli
 
Ulitaka kuagiza nini nje ya nchi kwa kutumia Dollar ukakosa?
Katika yote aliyoandika umeona suala la Dollar tu? Kwa taarifa yako dollar haitumiki kuagiza tu kitu nje kwa matumizi ya mtu binafsi bali serikali nzima hivyo kupelekea ugumu wote ulipo sasa hivi hapa nchini. Vilevile tamaa ya wanasiasa ikijumuisha na wafanyabiashara wenye ushawishi na nguvu kiuchumi kwa kutaka faida kubwa wanatoa hongo ili mambo yao yaende huku majority wakiumia, tazama suala la umeme na mfumko wa bei.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Petrol inatoka nje ya nchi inanunuliwa kwa fedha ya kigeni, hakuna namna ambayo sisi tunaweza kuwa na utawala wa bidhaa ya kutoka nje, wanaitawala wenye kumiliki hizo biashara na sio sisi.

Huko Lindi wamepata hospitali mpya tangu nchi ipate uhuru, unapowaambia awamu hii ni mbovu inabidi uje na hoja zenye kuingia vichwani mwao.

Kodi huwezi kukwepa kuzilipa iwapo unataka huduma ziboreshwe. Hao wanaotupa misaada wanajinyima matanuzi ili sisi tuweze kuishi, kumbuka hilo kabla hujaendelea kulialia.

Bandari inapata mwekezaji DP World na mwezi Novemba anaanza kazi, kule Mbegani Bagamoyo pia anakwenda kupatikana mwendeshaji mahiri, hiyo sekta ya uchukuzi serikali imejipanga kisawasawa.

Masuala mengi ya kiuchumi yanakwenda kupata ufumbuzi.

Punguza kulialia.
Hili shairi umeandika hapa kisha nikicheck hakuna umeme, natamani hata ugongwe na gari ufe au upate kilema Cha maisha.
 
Mkuu, nilichoandika ninaushahidi nacho, bila shaka hata wewe, kinachobaki ni ushabiki usio na tija
Nimekuuliza swali jepesi sana, unaanza kuhororoja, kubwabwaja na ngonjera zisizo na manufaa.

Jibu swali.
 
Ttzo lilianzia kwa jiwe mambo ya uchumi sio yakuchezea na uchumi kuurudisha ktk hali yake ya mwanzo hua ni kaz sana na huwa inachukua mda sana
Na mattzo ya uchumi huwa yaanza mdg mdg mwisho wa sku yanakua makubwa
Kipindi cha jiwe biashara na shuguli nying sana zilifungwa matajiri weng walipewa makesi na wengne kuzurumiwa pesa zao na serikal ya jiwe
Lakin pia mashirika ya kimataifa pamoja na wawekezaji toka njee walipoteza imani kwa nchi na serikal na wawekezaji wanapokosa imani na nchi uchukua mda mrefu sana kurudisha imani yao

Ebu angalia wahindi iv unazan kwann wahindi ad leo hawajengi majumba Tz km ilivyokua zamak kbla ya nyerere ebu angalia waindi leo uwekezaji wao ulivyo kwa ufupi wahindi hawana imani na serikal ya tz kutokana na matendo walofanywa na mwalimu nyerere ya kuwanyanganya na kutaifisha mali zao

Huyu mama kuna baadhi ni makosa yake ila ving ni muendelezo wa makosa ya jiwe jiwe aliharibu sana nchi.
 
Huduma zote mhimu kwa wananchi zimefeli vibaya mno

Huduma za matibabu hovyo

Dollar hakuna

Umeme hakuna

Huduma ya maji safi ni taabu

Pesa mtaani hakuna

Bidhaa juu, hadi kero

Mafuta hayana mdhibiti, mfanya biashara akiamka vibaya tu, hasira zote anazielekezea kwa walala hoi, anapandisha bei ama kuficha bidhaa hiyo

Bei za vifaa vya ujenzi havishikiki!

Bandari zimemshinda kuzisimamia

Ni awamu itakayeongoza kuwapeleka jela wanawake

Kodi nyingi na za ajabu ajabu, ni awamu hii

Lilianza suala la umeme, kutoka 27,000 hadi malaki ya fedha kuingiziwa umeme, badaye kulifuata Bima ya mtoto utadhani mtoto ana hatia kuzaliwa duniani!

Badala yake, tumeona sheria za wake za maraisi kuingizwa kwenye kulipwa utadhani na wao wanaingia ofisini

Mbona hawazungumziwi na au sheria hiyo kuwahusu wake za watumishi wote wa umma?
Watakuita mchochezi
 
Huduma zote mhimu kwa wananchi zimefeli vibaya mno

Huduma za matibabu hovyo

Dollar hakuna

Umeme hakuna

Huduma ya maji safi ni taabu

Pesa mtaani hakuna

Bidhaa juu, hadi kero

Mafuta hayana mdhibiti, mfanya biashara akiamka vibaya tu, hasira zote anazielekezea kwa walala hoi, anapandisha bei ama kuficha bidhaa hiyo

Bei za vifaa vya ujenzi havishikiki!

Bandari zimemshinda kuzisimamia

Ni awamu itakayeongoza kuwapeleka jela wanawake

Kodi nyingi na za ajabu ajabu, ni awamu hii

Lilianza suala la umeme, kutoka 27,000 hadi malaki ya fedha kuingiziwa umeme, badaye kulifuata Bima ya mtoto utadhani mtoto ana hatia kuzaliwa duniani!

Badala yake, tumeona sheria za wake za maraisi kuingizwa kwenye kulipwa utadhani na wao wanaingia ofisini

Mbona hawazungumziwi na au sheria hiyo kuwahusu wake za watumishi wote wa umma?
Unaambiwa wananchi wamechoka hadi watoto wao wananunuliwa viatu vya msaada
 
Ukiwa kwenye mfumo lazma uone maisha yako sawa maana uzembe hauna mashtaka awamu hii. Wizi umepewa baraka zote kwahio mtajenga sana, kununua sana mashamba kwa hela ya wizi.

Ishu ni kwa mtanzania ambaye riziki iko miguuni mwake. Hana bima wala support yeyote. Maisha hayawezi kuwa sawa
Hebu ngoja tuone hao wanaoitwa wanyonge kipindi Cha awamu iliyopita na hali zao ilikuwaje.

Wakulima:
Hili kundi halina bima na ridhiki yao ni jembe la mkono.
Asilimia almost 70% ya Watanzania wanajihusisha kwa namna Moja ama nyingine.

Lakini hali zao ziliboreka kipindi Cha awamu iliyopita?

Tuwatazame wakulima wa Korosho mikoa ya Pwani, Lindi,Mtwara na wilaya ya Tunduru.
Kabla serikari haijaingilia bei ya Korosho ilikuwa vizuri na wakulima waliita dhahabu nyeupe.

Lakini awamu ya tano ikaingia, tena mbaya zaidi ikatuma jeshi ndilo likusanye badala ya makampuni ya kigeni, matokeo yake,
Watu kudhulumiwa Korosho zao, vipigo kwa walanguzi na kushusha bei ya soko.

Kilimo Cha Mbaazi
Kilikuwa vizuri kilo ilienda mpaka 3000 na kunufaisha hawa wanyonge unao waits matokeo yake awamu ya tano ikaingiliwa, ikabiruga Soko na Mbaazi kushushwa mpaka 1000 kwa kilo.

Yaani muokota chupa za plastiki anapata pesa nyingi kuliko mkulima wa mbaazi, hebu fikiria kwa umakini.

Kilimo Cha Mahindi
Nani asiyejua bei ya pembejeo iliendelea kupanda kwa awamu iliyopita lakini bei ya mazao sokoni ilishushwa.

Wakati gharama ya kuhudumia shamba la mahindi ipo juu, Kuna mtu mmoja aliamua kuathiri chain nzima kwa kupiga marufuku masoko ya nje ambayo ni Kenya na Zambia.

Matokeo yake kaya masikini kule Sumbawanga na nyanda za juu kusini wakulima walikuwa wanapata hasara, kumbuka kule vijijini ndani ndani hutegemea kilimo hicho kuendesha maisha yao.

Hawakupunguziwa gharama za pembejeo za kilimo Wala kupewa chochote na serikari.

Kilimo Cha Nyanya
Waza mkoa wa Iringa na kitendo Cha kufungwa mipaka kilifanya Nyanya zishuke bei mpaka sado 500.

Je gharama za Nyanya, mbolea, mbegu, vibarua ilipungua?
Vipi wananchi wenye hali duni kule kilolo? Uliwafikiria?
Au hawa si wanyonge, labda Wana bima za kiasili kutoka kwa Mkwavinyika?

Mliaminishwa propaganda ambazo wachache walipata ukwasi usiomithilika na wengi mlikuwa bendera fuata upepo.

Vipi upotevu wa 1.5 Trillion ambazo CAG kazitaja kipindi Cha awamu iliyopita?

Vipi ununuzi wa Ndege kwa Cash ambazo value of money haionekani?
Kwenye Taifa masikini

Kwa nini sheria ya fedha, na budget ilikuwa haifuatwi?
Unajua kwenye ujenzi Kuna wizi mkubwa zaidi?
Kwa nini sheria ya manunuzi haikufuatwa?

Kwa nini Vijana wachache kina makonda na wenzie wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini mabenki yalifilisika?

Kwa nini mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa merged?

*Acheni propaganda na uzalendo uchwara huku wachache wakifaidika

Je wamachinga aliwaundia sheria ya kuwalinda?

Aliboresha maslahi yao ya kazi?

Au ilikuwa kete ya kisiasa
 
Serikali dhaifu kupata kutokea toka Tz imeumbwa ni hii ya 6 sijui, ni kama mbwa koko!.
Serikali pekee iliyobariki upigaji, rejea Mama akiwaambia wasaidizi wake (Mawaziri) wale kwa urefu wa kamba zao shingoni!.
Et wale ila wasivimbiwe!.
ziko mbwa zinamtetea huku ngoja zije!
 
Back
Top Bottom