Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Kwangu mimi Startimes ni bora kwa kilakitu kuliko Azam tv. Startimes naangalia ligi nyingi mno (Italy kupitia K24, Spain mechi zote, Bundesliga mechi zote, Caf Champions League, Caf confederation cup, Championship ESPN, Super league ya Uturuki ESPN, Italy Cup, n.k) na yote hayo ni kwa 21k tu!!!
Kifupi Azam kwangu ni upotevu wa pesa na hakuna content ya maana, karibuni Startimes.
 
Hawana Akili, watakosa hela za Vifurushi na badala yake watu wataenda kwenye vibanda umiza na maisha yataenda.

Hawajafanya tafiti kabisa kwenye hili.
Ila inatubidi tukajazane kwenye vibanda umiza ama kwenye mabaa,mechi zenyewe za ligi zilizo muhimu ni chache sana,
 
Hivi hicho kifurushi Cha elf15 kinaonesha Azam sports yaani mechi za bongo??
 
Ndugu mteja, kuanzia 01/04/2022, kuna mabadiliko ya bei kwa baadhi ya vifurushi; cha 20,000 kuwa 23,000; 13,000 kuwa 15,000; 4,000 kuwa 5,000: na 800 Kuwa 1000.

Vita ya Urusi na Ukraine inatuonyesha mambo.

Sisi wa DSTV tushazoea hayo mambo...
 
Mimi huwa nalipa jero tuu hii ya buku labda kunao matajiri
Mwendo wa jero jero tuu
IMG_20220326_094340.jpeg
 
Sawa. Nadhani mitambo yake imeathiriwana operesheni ya kijeshi huko Ukraine.
 
Tulijua Bakhresa atakua mkombozi, lakini nimekuja kujua hakuna mfanyabiashara asiyetaka kupata faida,
Hakuna charity pale
 
Ni ujinga mwanaume kulalamikia ongezeko la 3000 kwa mwezi
Mkuu umeongea kwa kukurupuka Sana. Hii monthly subscription na niendelevu, bado Kuna vitu vingine pia vinavyohitaji hela monthly. Sasa viweke vyote kwa pamoja, then utaijua nguvu ya 3000
 
Kazi ipo aisee mi majuzi ndo nimegundua kuwa hawana tena kifurushi cha 28000 baada ya kuwapigia simu kuona baadhi ya channels sizipati kwa muda na kusema kifurushi chao cha juu kwa sasa ni 35000.

Nilibakia kushangaa tu aisee. Ila tutafika tu kwani hamna namna.
 
Back
Top Bottom