Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Ni ujinga mwanaume kulalamikia ongezeko la 3000 kwa mwezi

Wacha tulalamike bhana! Maana sisi ndiyo watafutaji. By the way, hakuna hela ndogo!

Na usisahau hiyo elfu 3 ni ya mimi peke yangu! Tukilipa wateja laki 1 kiasi cha @elfu 3, utapata figure tofauti kabisa!
 
Hao wengine wanakuhusu nini? We naye anzisha yako
 
Mbona kama una hasira vile! Mimi pamoja na hao wengine ni wateja wa Azam. Hivyo ni jambo la kawaida kabisa kuwashirikisha.
Jamaa utafikiri yeye anaishi majuu kumbe yumo humu humu na yeye kajazwa makasiriko na hizi bei za vitu. Anajitoa sana ufahamu.
 
Jamaa utafikiri yeye anaishi majuu kumbe yumo humu humu na yeye kajazwa makasiriko na hizi bei za vitu. Anajitoa sana ufahamu.

Labda atakuwa hajaingia kwenye maisha ya kujitegemea. Maana anayachukulia maisha kwa wepesi sana. Kwake elfu 3 ni ndogo eti!

Hajui mteja atatakiwa kuilipa hiyo elfu kila mwezi! Hapo bado kuna bili nyingine nyingi za kulipa. Mfano Luku, maji, kodi ya pango, ada, nauli, matumizi ya nyumbani, nk.

Mbaya zaidi ni miaka michache tu iliyopita walitoka kupandisha vifurushi vyao.
 
Hii ni taarifa tuliyo tumiwa watumiaji wa king'amuzi cha Azam mapema leo tarehe 24/03/2022 kupitia ujumbe mfupi kwenye simu. Kuanzia tarehe 01/04/2022 bei ya malipo itabadilika. Na hivyo sisi watumiaji wa kile kifurushi pendwa cha elfu 20, itatulazimu kuongeza elfu 3 nyingine! Yaani tutaanza kulipa (23,000/=) kika mwezi!

Na ikumbukwe ni miaka michache tu walipandisha kutoka elfu 18, mpaka kufikia elfu 20! Sasa sijui sababu ni za kiuendeshaji, kuongezeka kwa kodi/tozo kutoka serikalini, au ni kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine!

Hakika Watanzania tutanyooka kwenye awamu hii ya Mama! Maana kila kitu bei juu! Halafu hakuna anayejali eti! 🤔
Vifurushi vingine vitakavyo pandishwa hiyo tarehe 01/04/2022 ni kile cha elfu 13, na sasa kitakuwa elfu 15! Cha elfu 4, kitakuwa elfu 5! Na cha mia 8, kitakuwa elfu 1!

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......Kazi iendelee...✍️
Tafuta Pesa wenye DSTV wasemaje?
 
Labda atakuwa hajaingia kwenye maisha ya kujitegemea. Maana anayachukulia maisha kwa wepesi sana. Kwake elfu 3 ni ndogo eti!

Hajui mteja atatakiwa kuilipa kila mwezi! Na bado kuna bili nyingine nyingi za kulipa. Mfano Luku, maji, kodi ya pango, ada, nauli, matumizi ya nyumbani, nk.
Probably, yeye akishika limoti na miguu juu anaona kayapatia hajui watu wamevuja jasho kuvilipia. Wangapi hawalipii ving'amuzi wakidai ni anasa kumbe ni msoto tu.....sembuse waje waambiwe tena vifurushi vimepanda si ndio watang'oa na madishi kabisa.
 
Kwahivyo Mkuu hatuna maajabu yoyote yaani...?!

Kusema ukweli kwa sisi wadau wa michezo, nje ya kuonesha michezo ya ligi kuu Tanzania Bara, king'amuzi cha Azam hakina maajabu! Bora hata ya Startimes.

Mimi nipo Azam kwa sababu ya Ligi kuu tu. Baada ya hiyo miaka 10 ya mateso, na ikatokea wakimalizana na TFF! Na mimi siku hiyo hiyo nahamia king'amuzi kingine. Maana hakuna namna.
 
Hii ni taarifa tuliyo tumiwa watumiaji wa king'amuzi cha Azam mapema leo tarehe 24/03/2022 kupitia ujumbe mfupi kwenye simu. Kuanzia tarehe 01/04/2022 bei ya malipo itabadilika. Na hivyo sisi watumiaji wa kile kifurushi pendwa cha elfu 20, itatulazimu kuongeza elfu 3 nyingine! Yaani tutaanza kulipa (23,000/=) kika mwezi!

Na ikumbukwe ni miaka michache tu walipandisha kutoka elfu 18, mpaka kufikia elfu 20! Sasa sijui sababu ni za kiuendeshaji, kuongezeka kwa kodi/tozo kutoka serikalini, au ni kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine!

Hakika Watanzania tutanyooka kwenye awamu hii ya Mama! Maana kila kitu bei juu! Halafu hakuna anayejali eti! [emoji848]
Vifurushi vingine vitakavyo pandishwa hiyo tarehe 01/04/2022 ni kile cha elfu 13, na sasa kitakuwa elfu 15! Cha elfu 4, kitakuwa elfu 5! Na cha mia 8, kitakuwa elfu 1!

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......Kazi iendelee...[emoji3578]
Kwani kilipopanda from 18l to 20k ilikuwa awamu ipi!?
 
Back
Top Bottom