Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Nimepokea ujumbe kutoka Azam kupitia simu yangu kuwa bei za vifurushi zitapanda kuanzia tarehe 1 April.

"Ndugu mteja, kuanzia 01/04/2022, kuna mabadiliko ya bei kwa baadhi ya vifurushi; cha 20,000 kuwa 23,000; 13,000 kuwa 15,000; 4,000 kuwa 5,000: na 800 Kuwa 1000." Azam Tv.

Vv
Vipi kile cha 28,000?
 
Dstv ni kama bia tu kwa radha yke ata ipande bei tutalipia nyie watizama etiguru mnateseka sana
 
Ndugu mteja, kuanzia 01/04/2022, kuna mabadiliko ya bei kwa baadhi ya vifurushi; cha 20,000 kuwa 23,000; 13,000 kuwa 15,000; 4,000 kuwa 5,000: na 800 Kuwa 1000.

Vita ya Urusi na Ukraine inatuonyesha mambo.
Takbiiir
 
ACHENI KULALAMIKA NA KULIALIA
KWANI LAZIMA MUANGALIE/KUTUMIA AZAM
MSHAKUWA WATUMWA NA MNA ADDICTION

Ova
 
Hawana Akili, watakosa hela za Vifurushi na badala yake watu wataenda kwenye vibanda umiza na maisha yataenda.

Hawajafanya tafiti kabisa kwenye hili.
Ndy mfanye hivyo
Hilo ndy suluhisho

Ova
 
Wameshalikamata soko sasa ndio muda wa kula faida, zile bilioni kadhaa hazikwenda bure.
 
Hii ni taarifa tuliyo tumiwa watumiaji wa king'amuzi cha Azam mapema leo tarehe 24/03/2022 kupitia ujumbe mfupi kwenye simu. Kuanzia tarehe 01/04/2022 bei ya malipo itabadilika. Na hivyo sisi watumiaji wa kile kifurushi pendwa cha elfu 20, itatulazimu kuongeza elfu 3 nyingine! Yaani tutaanza kulipa (23,000/=) kika mwezi!

Na ikumbukwe ni miaka michache tu walipandisha kutoka elfu 18, mpaka kufikia elfu 20! Sasa sijui sababu ni za kiuendeshaji, kuongezeka kwa kodi/tozo kutoka serikalini, au ni kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine!

Hakika Watanzania tutanyooka kwenye awamu hii ya Mama! Maana kila kitu bei juu! Halafu hakuna anayejali eti! 🤔
Vifurushi vingine vitakavyo pandishwa hiyo tarehe 01/04/2022 ni kile cha elfu 13, na sasa kitakuwa elfu 15! Cha elfu 4, kitakuwa elfu 5! Na cha mia 8, kitakuwa elfu 1!

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......Kazi iendelee...✍️
 
Hii ni taarifa tuliyo tumiwa watumiaji wa king'amuzi cha Azam. Kuanzia tarehe 01/04/2022 bei ya malipo itabadilika. Na hivyo sisi watumiaji wa kile kifurushi pendwa cha elfu 20, itatulazimu kuongeza elfu 3 nyingine! Yaani tutaanza kulipa (23,000/=) kika mwezi!

Na ikumbukwe ni miaka michache tu walipandisha kutoka elfu 18, mpaka kufikia elfu 20! Sasa sijui sababu ni za kiuendeshaji, kuongezeka kwa kodi/tozo kutoka serikalini, au ni kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine!

Hakika Watanzania tutanyooka kwenye awamu hii ya Mama! Maana kila kitu bei juu! Halafu hakuna anayejali eti! 🤔
Vifurushi vingine vitakavyo pandishwa hiyo tarehe 01/04/2022 ni kile cha elfu 13, na sasa kitakuwa elfu 15! Cha elfu 4, kitakuwa elfu 5! Na cha mia 8, kitakuwa elfu 1!

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......Kazi iendelee...✍️
Sisi tunaotumia visimbuzi vya Azam vya Kenya tulishakutana na hali hiyo toka mwezi uliopita
 
Ndio maana walisaini miaka 10, sababu ya mambo yao kama haya....
Ila wajue tu, ikiisha hiyo watakuwa kwenye wakati mgumu.

Dah! Noma sana. Wanaongeza bei, huku chaneli zao nyingi zikiwa ni za kawaida tu. Na kwa sisi tunao fuatilia ligi kuu ya NBC, hatuna namna. Tutaendelea tu kusikilizia maumivu kimya kimya.
 
Back
Top Bottom