Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Azam kupandisha bei za vifurushi kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022

Ukiondoa DSTV king'amuzi kinachofuata kwa ubora sema tu watu hawakiimbi ni Startimes, Mfano sisi watu wa soka kwa Tsh 21000 unaangalia

1.Ligi ya Germany
2.ligi ya Spain
3.Caf Champions League
4. CAF confederation cup
5. AFCON
6.Mechi zote za kufuzu World Cup Europe
7.Mechi zote za kufuzu world Cup Asia
8. Copa Italia
9.Kupitia Espn kwa hiyo hiyo Tsh 21000 unaangalia ligi ya Turkey, ligi ya Scotland, Championship ya England ligi ya Marekani na mechi kibao za Basketball

Kwa upande wa Tamthilia nafikiri ndio channel namba moja kwa Tanzania
 
Watz wengine kulalamika tu hata iongezeke 100 watapiga kelele na pengine wao hawana hata hivo TV
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Sisi wenye azampesa pia kulipia gharama zake n hizo hizo au zitashuka kidogo.
 
Hivi azam ana nini zaidi ya channel za mpira
 
Ndugu mteja, kuanzia 01/04/2022, kuna mabadiliko ya bei kwa baadhi ya vifurushi; cha 20,000 kuwa 23,000; 13,000 kuwa 15,000; 4,000 kuwa 5,000: na 800 Kuwa 1000.

Vita ya Urusi na Ukraine inatuonyesha mambo.
Na 8000 Kwa mwezi kitakuwa sh ngapi?
 
Hii ni taarifa tuliyo tumiwa watumiaji wa king'amuzi cha Azam mapema leo tarehe 24/03/2022 kupitia ujumbe mfupi kwenye simu. Kuanzia tarehe 01/04/2022 bei ya malipo itabadilika. Na hivyo sisi watumiaji wa kile kifurushi pendwa cha elfu 20, itatulazimu kuongeza elfu 3 nyingine! Yaani tutaanza kulipa (23,000/=) kika mwezi!

Na ikumbukwe ni miaka michache tu walipandisha kutoka elfu 18, mpaka kufikia elfu 20! Sasa sijui sababu ni za kiuendeshaji, kuongezeka kwa kodi/tozo kutoka serikalini, au ni kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine!

Hakika Watanzania tutanyooka kwenye awamu hii ya Mama! Maana kila kitu bei juu! Halafu hakuna anayejali eti! 🤔
Vifurushi vingine vitakavyo pandishwa hiyo tarehe 01/04/2022 ni kile cha elfu 13, na sasa kitakuwa elfu 15! Cha elfu 4, kitakuwa elfu 5! Na cha mia 8, kitakuwa elfu 1!

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......Kazi iendelee...✍️
Tuendelee kuvumilia, sababu utaambiwa ni vita ya Urusi na Ukraine😂😂😂 kama vile wao ndio wamezuia sattelite signals vile
 
Back
Top Bottom