Azam Ongezeni watu wanaotafsiri kazi za Sana za nje.

Azam Ongezeni watu wanaotafsiri kazi za Sana za nje.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Lengo lenu ni zuri sana, lakini kitendo cha kazi nyingi za sanaa kutoka nje ya Tanzania zinazotafsiriwa kwa kiswahili kuwa na sauti zile zile kwa kazi tofauti tofauti, siyo sawa.

Itapendeza kama mtaweza kuwa na watia sauti tofauti wengi kuliko Kila kazi ya sanaa kutumia sauti zile zile za watia sauti.
 
Nimekuelewa na nitalifanyia kazi mkuu..

Asante kwa ushauri wako....🙏🙏🙏🙏🙏
 
changamoto itakuwa ni ngumu kuwapata

watanzania wanaojua kituruki, kikorea, watakuwa wachache

au wanawafundisha wenyewe?

halafu si unajua huku bongo ukisoma kozi za lugha unadharaulika
 
changamoto itakuwa ni ngumu kuwapata

watanzania wanajua kituruki, kikorea, watakuwa wachache

au wanawafundisha wenyewe?

halafu si unajua huku bongo ukisoma kozi za lugha unadharaulika
Mtu anadharau kozi za lugha wakati hizo lugha zenyewe zinamfua kiroho mbaya?Huyo atakuwa zuzu grade one!
 
changamoto itakuwa ni ngumu kuwapata

watanzania wanajua kituruki, kikorea, watakuwa wachache

au wanawafundisha wenyewe?

halafu si unajua huku bongo ukisoma kozi za lugha unadharaulika
Mkuu zile muvi huwa zinakuja na subtitles..
Sema ni vile bongo tuu kuna lack of team work.

Watu wanataka kila kitu wafanye wao tyu we assume et unakuta ni wale wale hii hata mimi nilifikilia sana..

Unajua kuna vijana wengi wanafatilia hizi mambo lakini nafasi hakuna...

Yaani hapo azam hapo daah mavi mavi tuu
 
nakataa kuamini dubbing inafanywa kwa kuangalia subtitles

inabidi dubber ajue lugha husika

mfano sentensi ya kiingereza "head in the clouds" ukiitafsiri kama ilivyo mtazamaji atapoteza maana kwasababu huo ni msemo unaomaanisha mtu kapoteza umakini

kuna mafunzo fulani inabidi upitie
Amini mkuu...
Nilikua deptment ya karibu na hao translator...

Labda sijajua kama hayo mambo yamebadilika...

We assume sauti zile zile je hao wote wanajua lugha zote hizo...

Pia watalamu wa lugha wapo sana tuu
 
mshamba_hachekwi wanaotafsiri hizo "Subtitles" si lazima wawe ndiyo wanaoingiza sauti.

Mimi nazungumzia wanaoingiza sauti. Watafsiri wanaweza kuwa hata wawili tu, bali watia sauti kwa kuwa hutumia Muongozo (Script) uliotafsiriwa tayari, ni rahisi kuwabadili.
poor brain amesema waingiza sauti wanatumia subtitles, sio lazima wajue lugha

ndo nikawa nambishia

kumbe wanatumia script! basi hapo kweli shida ipo

nilijua waingiza sauti wanatunga scipt zao wenyewe kwasababu nilidhani lazima wajue hizo lugha
 
Back
Top Bottom