Azam Tv wazindua chaneli mpya Azam Sports 4HD, watarusha La liga pamoja na Serie A

Azam Tv wazindua chaneli mpya Azam Sports 4HD, watarusha La liga pamoja na Serie A

Nje ya mpira wa bongo hamna kitu kinanivutia azam.
Ila uswahilini huwaambii kitu kuhusu azam, na pia jamaa wanajitangaza mno mno.

Haipiti siku hujasikia tangazo la azam media iwe redioni, au huko kwenye harakati utakutana nao tu wanazunguka na magari yao au myamvuli yao wanauza madishi.

Dstv iko poa sana tatizo gharama.
Kuna tamthilia yao fulani mie ilikuwa inanikera
Sijui mtaa wa kazamoyo

Walikuja waswahili,wavuta bangi,wacheza vigodoro na wambea wote wakanishambulia.

.......
DsTv sisi wapenda kandanda safi acha ituue tu.
 
Nje ya mpira wa bongo hamna kitu kinanivutia azam.
Ila uswahilini huwaambii kitu kuhusu azam, na pia jamaa wanajitangaza mno mno.

Haipiti siku hujasikia tangazo la azam media iwe redioni, au huko kwenye harakati utakutana nao tu wanazunguka na magari yao au myamvuli yao wanauza madishi.

Dstv iko poa sana tatizo gharama.
Nunua Canal+ dishi complete kwa Dar ni 160k
 
Azam Tv wamezindua chaneli mpya ya Azam Sports 4HD na watarusha La liga ( Ligi Kuu ya Hispania) pamoja na Ligi Kuu ya Italy (Serie A)

Chaneli hiyo itaanza kuruka hewani 1 August 2024.

Tayari Azam Tv anarusha Ligi Kuu ya Tanzania, Ligi Kuu Kenya, Saudia Arabia, Ufaransa, Caf Champions League and Confederation Cup.
Wasije Kuongeza kifurushi kutoka 35 hadi 38.
 
Hatua kubwa kwenye Sekta ya habari, michezo na Burudani

Na ni jambo la kujivunia kuona Mswahili mwenzetu akipiga hatua kubwa za KiUwekezaji

Tulizoea kuona Wazungu na Makaburu ndiyo wanafanya Uwekezaji Kwa kiwango hicho, tumpe Maua yake akiwa hai

Kama ataweza aombe haki ya kurusha mchezo wa mieleka yaani WWE 🙏
 
Kama kuna mtanzania kuanzia leo ataendelea kuisema vibaya Azam media, atakuwa na matatizo binafsi!

Hili ni kampuni la kizawa limetengeza ajira nyingi sana! Hakika wanatuheshimisha watanzania!
Upo tayari kulipia bei mpya za vifurushj?
 
Back
Top Bottom