Azam TV wazindua mitambo mipya ikiwemo VAR, kamera moja tu imegharimu Tsh. Milioni 500

Azam TV wazindua mitambo mipya ikiwemo VAR, kamera moja tu imegharimu Tsh. Milioni 500

Aisee nimeangalia uwekezaji wa Azam TV kwa kununua mitambo mipya ya mabilioni ya pesa.Duuuh kuna media zina pesa wallah....Mabilioni ya pesa hapo yametumika!!

Hawa watu wamejipanga kweli, nimeona tu kamera moja ya ubora wa kimataifa kama zile wanazotumia huko Hollywood nk ni milioni 500.na hapo wamenunua kamera kibao ambayo kila moja ni milioni 500!!

Hapo hujaweka mitambo mingine ya kisasa, VAR etc.
Mitambo ya VAR wamezindua!

Azam wanatumia pesa kuwekeza ndo maana wanapata kila wanachokitaka. Wameweza kufanya channel zao zote kuwa HD sio kazi rahisi. Hawa wanatakiwa waje na laini za simu sasa.

TV nyingine na media za kibongo nyingine wana la kujifunza kwa Azam!!
Million 500 umeirudia sana je wataalamu wanao!
 
Unaweza ukawa na vifaa vizuri ila ukashindwa kulipia supporting bills,
Mfano Ili urushe hayo matangazo transponder Moja kukodi Kwa wamiliki wa satellite yenye uwezo wa kurusha matangazo Kwa njia ya full hd, 4k gharama yake inaweza kuzidi gharama ya vifaa vyako na studio Kwa ujumla, hivyo wengi hawashindwi kwenye vifaa vya ardhini ila Kuna mabwenyenye yenye satellite zao ndio mtihani
Frequency yenye kubeba vichannel 3 kwa kiwango Cha SD(mpeg 2) ni zaidi ya 150 million kwa mwaka
 
Unaweza ukawa na vifaa vizuri ila ukashindwa kulipia supporting bills,
Mfano Ili urushe hayo matangazo transponder Moja kukodi Kwa wamiliki wa satellite yenye uwezo wa kurusha matangazo Kwa njia ya full hd, 4k gharama yake inaweza kuzidi gharama ya vifaa vyako na studio Kwa ujumla, hivyo wengi hawashindwi kwenye vifaa vya ardhini ila Kuna mabwenyenye yenye satellite zao ndio mtihani
Frequency yenye kubeba vichannel 3 kwa kiwango Cha SD(mpeg2) ni zaidi ya 150 million kwa mwaka
🙌
 
Hata wanunue mitambo ya namna gani. Siwezi kuangalia media zao. Infact siwezi kuangalia media yoyote ya Tanzania iwe Radio au TV wote ni uchafu tu.. Acha niendelee na ABC news, CNN,BBC, FOX , NSBC, DW tv, RT, France 24.
 
Jamaa yangu nilitaka nikupige bonge 1 la Neno ovu Ila nikakumbuka Kapeace mtu wangu wa faida alishanisihi sana nisiparangane na vitukuu na vilembwe vya Kambarage Nyerere hivi vitukuu na vilembwe na vilembwekeze havielewi hata vieleweshwe vipi

Ukileta Andiko lenye mashiko mithili ya Habari mzito lazima uisupport na ushahidi km picha, Video na sauti sasa Wewe unatuandikia udaku hivi tunakufikiriaje mtu wangu au unataka utembezewe matusi hizo camera za million 500 zipo Wapi picha ipo Wapi videos zipo Wapi zikionyesha hizo camera na mitambo hio mipya? Mengine sitaki kukuhoji sana maana najua nikikuhoji utabust bure
Tumegoma kula matango pori
 
Azam Media hana mpinzani wameleta kamera za 4k,seti ya Kamera moja inafikia 500M na pale zilikuwa Kamera zaidi ya Tano....ni balaa.
Azam wakipata kibali cha kuonyesha EPL na Uefa DSTV anakosa wateja.
Nafurahi kuona tunapata pongezi
 
Back
Top Bottom