Kuna mama mmoja alipiga simu kwa kiongozi mmoja wa dini kuwa afanye haraka mno aende kwake kuna tatizo, basi yule kiongozi akachukua vijana kama watatu wakafuata location.
Walipofika yule mama akawafungulia mlango akawakaribisha vizuri kisha akawaelekeza mlango wa mbele yake akamwambia yule kiongozi nyie nendeni tu ingieni moja kwa moja.
Walipoufungua ule mlango ghafla! wakamkuta kijana wa kiume mwenye umri kati ya miaka 18 mpaka 25 akiwa uchi wa mnyama na mbele yake kuna laptop screen inaonesha video chafu ikiwa paused, jambo baya zaidi yule kijana akiwa amefariki tayari huku akiwa na athari ya kufanya punyeto muda mfupi uliopita na akafa katika hali hiyo.
Yule kiongozi akabaki kimya asijue cha kufanya kwa haraka, mama yake yule kijana marehemu akawa analia tu kwa kwikwi anamuuliza yule mtu wa hekima; "vipi kwa mwisho huu wa mwanangu, itakuwaje?" yule kiongozi asijibu lolote.
ushauri wangu, ndugu zangu ambao bado tunasumbuliwa na mihemko ya ujana au matamanio tuwe makini sana na hizi tabia tunazofanya tukiwa peke yetu maana ikitokea equation ikabalance basi aibu yake tunawaachia watu wetu wenye heshima kama mama, baba na watoto au mke.
Mwenye masikio na asikie.