Uchaguzi 2020 Azimio: Bunge la Marekani laisihi Serikali ya Tanzania na wahusika wote kuhakikisha Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

Uchaguzi 2020 Azimio: Bunge la Marekani laisihi Serikali ya Tanzania na wahusika wote kuhakikisha Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

Unaweza kushangaa USA anasema viongozi wetu hata wapelekwe ICC ambayo yeye mwenyewe kaikimbia.
Duniani huwa hakuna haki Za binadamu wala demorasia inategemea tu unaruhusu kiasi gani mabeberu wakupande. Kama madini na rasilimali wanazoa watakavyo wewe Utakua unademokrasia kubwa Sana na unafaa kuigwa na nchi nyingine. Lakini ukianza kujitambua utakua hufai kabisa hata demokrasia yako iwe kubwa Kiasi gani na wanajua ukiweka demokarasia ya kiwango cha juu kukuvuruga usiendelee ni rahisi Sana.
Ukiona hupigiwi kelele na mabeberu ujue huna unachokifanya wanakukula watakavyo.
Namshukuru Mungu tumenza kuonwa Kama watu tulio serious na maendeleo tunapigiwa Kelele Sasa.
Hatuna budi kuwanunulia pepsi kubwa wakati wa vikao wanywe wakijadili. Maana wanamambi mengi yakujadili lakini wameacha yote waijadili TZ lazima Tutakua tumeanza kugoma kupandwa.


Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Jidanganye tu. Unafikiri bunge la Ndugai lile??? Yajayo yanafurahisha
Bunge letu la Ndungai ni bora mara mia kuliko hilo la kwao. Kwa nini nyie watu hampendi vitu vya kwenu, mnapenda tu vya wenzenu? Wahenga walisema chako ni chako na nyumbani kwako ni kwako hata kama ni pangoni! They have no any moral authority to tell us anything about our electral process.
 
K
Azimio la bunge la Marekani liliotolewa tarehe 17/09/2020 lenye jina la "Urging the Government of Tanzania and all parties to respect human rights and constitutional rights and ensure free and fair elections in October 2020, and recognizing the importance of multi-party democracy in Tanzania."

Limepitishwa nchini Marekani kusihi serikali ya Tanzania na wadau wote wanaohusika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 nchini Tanzania kufuata haki za binadamu, katiba ili kuhakikisha uchaguzi utakuwa wa huru na haki hapo mwezi Oktoba 2020. Tamko hilo limeonekana kukemea baadhi ya vitendo vya Serikali ya Tanzania tangu mwaka 2015 vyenye viashiria vya kuvunja haki za wananchi wa Tanzania.

Moja ya madai ya azimio hilo ni kwamba:
1. Serikali ya Tanzania imezuia ukusanyaji huru wa takwimu, utoaji wa takwimu
2. Serikali ama watendaji wa serikali wamekuwa wakitishia, kushambulia na kukamata wanahabari na kutokujali wanahabari waliopotea.
3. Serikali imezuia wanasiasa kufanya shughuli zao za kisiasa kuanzia mwaka 2016 mpaka 2019 kinyume na katiba ya nchi.
4. Serikali imedhibiti uhusiano wa taasisi zisizo za serikali NGO na taasisi nyingine zilizopo nje ya nchi kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa mnamo September 2019.
5. Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipotea vitisho, kushambuliwa na serikali kushindwa kuwakamata watenda makosa.

View attachment 1573603
View attachment 1573916
View attachment 1573915
View attachment 1573916
Soma zaidi:
Tanzania yaihakikishia Marekani uchaguzi utakuwa huru | DW | 09.09.2020
Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini
Ubalozi wa Marekani: Mbowe ameshambuliwa kikatili, wakumbushia pia shambulio la Tundu Lissu huku kukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa
Kibaraka wao hana chake,Oct 28.Wakae kwa kutulia tu.
 
Haya maneno ya USA siyapendi. Walete USS Ronald Reagan mwabao wa bahari ya Hindi kama itatokea dhuluma ya kuiba kura wamtandike mtu. Haya maneno dictators never heed to words! 🤪 🤪 🤪 🤪 🤪 🤪
View attachment 1573606

Jamani mimi ni Mzalendo, siyo kuwa nataka nchi yangu ishambuliwe hapana, ila Kiongozi akianza kuwaua watu wake, akija jirani tutamuomba msaada tusiuawe! Ni hilo tu. Ben Saanane yuko wapi? Azory Gwanda yuko wapi? Tumwombe jirani atusaidie kuwatafuta!

Wakikujibu walipo hao ndugu tupo wengi, tunahamia CCM si kwa kununuliwa.

Short of that:

"Na wapigwe tu" - in Pinda's words.
 
Bunge letu la Ndungai ni bora mara mia kuliko hilo la kwao. Kwa nini nyie watu hampendi vitu vya kwenu, mnapenda tu vya wenzenu? Wahenga walisema chako ni chako na nyumbani kwako ni kwako hata kama ni pangoni! They have no any moral authority to tell us anything about our electral process.
Umeishia darasa la ngapi???
 
Tunamzungumzia Dikteta Jiwe
Wewe unadhan twamzungumzia nani?
Huu udikteta nimeusikia kwa Hayati B.Mkapa, nimeusikia kwa Mzee Dkt M. Kikwete na sasa Kwa Dr. JPM...

Lini tangu Uhuru kuna Rais alipita na machoni mwa wapinzani aliacha kuwa Dikteta!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hawajasema ccm ishindwe chadema ishinde, wamesema uwe huru na haki. Wafuasi wa vyama hamuelewi.
 
Mie naendelea tu kufanya utafiti wa silaha za Marekani pale watakapoamua kuja kumtoa mtu kama walivyofanya kwa Noriega wa panama

Leo nimeanza na ndege vita F 22 Raptor

96C9CD91-9163-4A27-B31F-5B80D3E60B12.jpeg
 
Na yeye analijua hilo ndiyo maana anapaniki hadi naanguka jukwaani.
Daaah hivi hiyo clip ya jamaa alivyoanguka jukwaani, wakati anapiga kelele zake unayo? Nahisi inafaa kwa matumizi ya baadae[emoji1787]
 
Hii pia ni ndege vita ya Marekani inaitwa B 2 Stealth Bomber!! 😂😂😂😂😂

E6509188-6613-4B73-98E8-2CF06D5DECC0.jpeg
 
Back
Top Bottom