Tetesi: Aziz Ki anataka Dola laki tano kubaki Yanga

Ameshafanya kazi tuliyomtaka afanye. Kama anauzika kwa faida, basi auzwe tu ili kuzuia matabaka ya miongonzi mwa wachezaji wetu kwani dau analotaka litaweka tofauti kubwa sana na wachezaji wengine, jambo linaloweza kuwapunguzia motisha kama timu.
 
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu, Yanga itabaki palepal

Kila la heri kwake huko aendako
 

Engineer sio boya kihivyo. Hakuna pesa hiyo
Atakavoamua yeye yanga ni kubwa kuliko Aziz ki
 
Wakati yanga wanamchukua akiwa free agent waluchekelea, Sasa hivi zamu yao.
Kama Kibu mwenye goli moja alipigiwa debe apate mamilion Aziz K anastahili maradufu.
 
Aende tu huyo asijione mkubwa
Kila mtu aringie alichojaliwa! Ni haki yake! Kama Yanga wanataka kupiga hela wampe hiyo hela asaini mkataba chap chap halafu mwamwuze kwa Al Ahly au Masandawana!
 
Izo Hamptati hata mia maana yuko huru hana mkata na yanga kwa sasa
Mlishangilia alipoondoka Mayele mkifikri mtapumzika mateso, sasa hivi mmeanza tena kwa Aziz Ki! Taabu iko pale pale!
 
Mi nadhani timu zetu ziwekekeze zaidi kwenye wachezaji wa nyumbani.
Tusajiri wa kigeni lakini mkazo mkubwa tuweke nyumbani.
Itapunguza gharama na pia kujenga uwezo wa watu wetu
Hawa wa kwetu hata ukiwekeza huwezi kupata quality ya akina Aziz Ki na akina Pacomé! Jamaa hawakwepeki!
 
Mnapenda sana kuokoteza habari za vijiweni, habari haina hata source. Wewe ulikutana na Aziz Ki akakuambia haya??
 
Napendekeza aondoke tu Bora wapatikana wakina pacome 3
 
Naunga mkono Hoja , Ila kama Mtindo ni huu wa kuachia kila mchezaji anaefanya vizuri kwasababu ya kukosa hela Ubingwa wa Afrika tutausikia tu kwenye Bomba.
Virabu vya Tz havina uwezo huo wa kipesa wa kuweza kumzuia mchezaji, wanachama hiyo pesa tu ya kulipia kadi kwa mwaka ni mtihani!! Na ndio maana kamwe amewambia sio tu kupiga kelele, kama mnataka abaki changeni pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…