Aliwahi kusema lini kwamba mama yake amekufa?! Mimi ninachojua kuna yule mama ambae alijiweka sana mbelembele kwenye issues za Aziz hadi watu wakaamini ndie mama yake! Hata kwenye ndoa ya Aziz yule mama akalipeleke saga Instagram kuonesha ni namna gani ndugu hawaridhika kabisa na ndoa ya Azizi na Hamisa kwa madai hawakupewa taarifa na akaenda mbele zaidi kudai yote ile ni janja ya Injinia kuhakikisha Aziz haondoki. That mama overshadowed Mama Aziz existence! Just imagine, hata wakati anailalamikia ile ndoa alikuwa anawazungumzia ndugu hususani wajomba lakini hakugusia kabisa suala la mama; na hapo ndipo watu waka-conclude kwamba mama yake mzazi alishafariki.
Hata hivyo, nakuunga mkono hilo la Diamond! Sitaki kuwa mnafiki, linapofika suala la Diamond kuwajali ndugu, simkaribii hata kidogo! Na humu watu kwa unafiki tu watashindwa kukiri kwamba Diamond anamjali zaidi mama yake kuliko majority mnavyowajali mama zenu! No wonder the boy is successful!