Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Umuhimu wa bandari sio tatizo,tatizo ni mapato yatokanayo na bandari yanamnufaisha nani?
Hata hiyo Dar Port,container terminal kwa undani anaefaidika ni TICS siyo TPA sababu ya mikataba mibovu.
Iwe kupanua bandari za Mtwara, Dar na Tanga au Kujenga bandari upya kama Bagamoyo,Kilwa n.k,tusiwabebeshe wananchi mzigo mzito wa madeni wakati mfaidika au wafaidika ni watu wachache.
Mkataba wa ujenzi wa Bagamoyo uwekwe wazi ili umma ujue mazuri na mabaya yaliomo.
TICS ni kitu gani bwana mkubwa?
 
hizo meli kubwa haziwezi kuingia Dar, kwanini zisipelekwe mtwara ambayo ni natural port mpaka hapo mtakapo baadaye miaka 10 au 20 inayo kuja baada ya wachumi na wana sheria kuupitia vizuri,sio wanasiasa.
Mambo mengine kama huyajui nakushauri bora ukae kimya badaya ya kujidhalilisha...
 
TICTS-: Tanzania International Container Services (TICTS) Company
Oh kumbe TICTS... maana niliona TICS nikadhani kuna kampuni nyingine tena

TICTS = Tanzania International Container Terminal Services Ltd.
 
Atupe ushahidi kuwa bandari ya Dar imezidiwa. Kama ndivyo kwanini Bagamoyo? Miradi ya akina Kikwete na Ridhiwani ya mambo ya kuachiliwa huko China tusileteane hapa. JK na kijana wake akamalizane na wachina huko. MTU mmoja asituharibie mabilioni ambayo yatasaidia watanzania wengi
 
Bandari ya Bagamoyo haiwezi kujengwa pasipo kuzuia utendaji wa bandari zingine, ni sharti la lazima linasemwa kuwepo ndani ya mkataba. Huwezi kupata vyote.
Nashukuru wewe umenielewa vizuri sana,ikiwa mkataba wake utazuia utendaji wa bandari zingine na pia kuzuia MAMLAKA zetu katika kukusanya mapato ni kwamba #MRADI_HUO_HAUTUFAI.
 
Bandari ya Bagamoyo haiwezi kujengwa pasipo kuzuia utendaji wa bandari zingine, ni sharti la lazima linasemwa kuwepo ndani ya mkataba. Huwezi kupata vyote.
Nashukuru wewe umenielewa vizuri sana, ikiwa mkataba wake utazuia utendaji wa bandari zingine na pia kuzuia MAMLAKA zetu katika kukusanya mapato au kupata mapato ya 50% ni kwamba #MRADI_HUO_HAUTUFAI.
 
Zungu mawazo yake hayana faida Kwa taifa kashindwa kuiongoza Ilala kuwa na barabara nzuri kwa kipindi chote Cha ubunge wake.
Na mlivyo wajinga mkapokea rushwa yake mkapiga kampeni ashinde na kuiba kura mlimsaidia
 
Two wrongs can't make it right. Kwa mtindo wako huu tutakuwa tunakosea kila siku.

..ninachopendekeza ni uwazi ktk miradi yote tukianza na sgr na stieglers.

..tazara ilijengwa kwa miaka 5 toka Tz mpaka Zmb. Lakini sgr kipande cha Dar to Moro kinakwenda mwaka wa 4.

..pia hakuna sababu za msingi zilizotolewa za kuruka kipande cha Makutupora - Tabora - Isaka badala yake tumekwenda kuanza ujenzi Isaka - Mwanza.
 
Jambo la msingi ni kuboresha bandari zilizopo za dar, Tanga na Mtwara... Bandari ya bagamoyo ni ufisadi na mwiba kwa bandari zilizopo...

Kuboresha bandari ya tanga ni vizuri ukizingatia bomba la mafuta kutoka Uganda litaishia pale...
Wataboresha matumbo yao mpaka yapasuke. Wanasiasa bongo ni wezi! All of them are morons!
 
..ninachopendekeza ni uwazi ktk miradi yote tukianza na sgr na stieglers.

..tazara ilijengwa kwa miaka 5 toka Tz mpaka Zmb. Lakini sgr kipande cha Dar to Moro kinakwenda mwaka wa 4.

..pia hakuna sababu za msingi zilizotolewa za kuruka kipande cha Makutupora - Tabora - Isaka badala yake tumekwenda kuanza ujenzi Isaka - Mwanza.
Wamekula hapo mabillioni. Hivi kwa nini wasiwajibike wakimaliza muda wao? Mama kazi ni panga pangua na kusafri nje na bombardier.RIP Magufuli.
 
Wamekula hapo mabillioni. Hivi kwa nini wasiwajibike wakimaliza muda wao? Mama kazi ni panga pangua na kusafri nje na bombardier.RIP Magufuli.

..Yote hayo yalifanyika wakati wa uhai wa Magufuli.

..Na Samia alikuwa anasafiri hata wakati wa Magufuli.

..Yeye ndiye alikuwa akimuwakilisha Raisi ktk mikutano ya kimataifa.

..Nakubaliana na wewe kwamba Mama anatakiwa afichue USIRI unaoendelea ktk miradi ya kimkakati. Kufanyike UKAGUZI ktk miradi hiyo.
 
..ninachopendekeza ni uwazi ktk miradi yote tukianza na sgr na stieglers.

..tazara ilijengwa kwa miaka 5 toka Tz mpaka Zmb. Lakini sgr kipande cha Dar to Moro kinakwenda mwaka wa 4.

..pia hakuna sababu za msingi zilizotolewa za kuruka kipande cha Makutupora - Tabora - Isaka badala yake tumekwenda kuanza ujenzi Isaka - Mwanza.
Nikadhani ulimaanisha kwasababu hiyo mikataba ya Stiglers na SGR hatuijui, basi na huu wa Bagamoyo tuupotezee tu.
 
Mambo mengine kama huyajui nakushauri bora ukae kimya badaya ya kujidhalilisha..
Sorry nimeambiwa wewe unajua sana than any other person(s), so we should listen / or agree with U
 
Kwani gharama za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni TSH ngapi?
 
Bagamoyo special economy zone ni mkombozi wa ajira ila shida hapa ni matango pori watu walilishwa basi wao ni kupinga tu ila huu mradi ni muhimu
 
Back
Top Bottom