Mchezo Kama huo aliuufanya pia Manji huko Kigamboni, baada ya kustuliwa na watu wa ndani kuhusu Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kupita,yeye Manji akawafuata Wakazi wa pale kwenye mradi na kuwarubuni kununua Viwanja vyao kwa M7 kwa kila mwenye kipande chake Cha Aridhi na kweli wengi walimuuzia maana walikuwa hawajui kuwa mradi tayari unakuja, na wale wachache waliojuwa walitishwa kuwa watanyanganywa Aridhi yao na Serekali,basi kwa haraka haraka nao wakakubali kumuuzia manji, japokua kuna wachache sana wao walichukua pesa kwa Manji na bado wakamkatalia, hao wengi wao walikua Wanajeshi wastaafu,
Sasa Mradi ulivyo kuja tu,ukakuta tajiri Manji ndiyo mmiliki wa eneo lile, Sasa ndiyo ikabidi wakae na Manji awauzie,Sasa hizo bei zilizopigwa hapo! Manji alipiga pesa ndefu sana,na ndiyo maana itachukua muda mrefu sana lile Daraja la Kigamboni kurudisha pesa zote za Mradi!! Matajiri wengi ni Wapigaji!!