KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwa maoni yako "Mwenye aliye nacho aongezewe zaidi"?Tanga na Mtwara mbona zinapanuliwa kitambo tu lakini ujenzi unaenda taratibu sana sababu bajeti ipo stretched sana.
Sababu kubwa ya Bagamoyo ni muwekezaji ndio ameonyesha opportunity hapo sio kwamba pesa ni yetu tunaweza amua wapi iwekwe. But maadam ni Tanzania hakuna hasara yoyote hta Gesi ipo mtwara but inachakatwa Dar!!
Bagamoyo kwa maoni yangu ipo karibu na social amenities nyingi kwa uwepo wa Dar tu mfano SGR, Airport kubwa, service sector karibu yote imejikita Dar (Bima,logistics etc) so Bagamoyo itakua kma extension tu ya jiji la Dar but kwa Mtwara inabidi mpka lami zijengwe, Airport zitanuliwe, mfumo wa Reli na vitu kibao vianze kujengwa upya so inakuwa disadvantage kwa uwekezaji mkubwa kama huo.
Bagamoyo ni sehemu nzuri ya kuwepo kwa bandari ya nguvu; lakini kwa sababu tunataka maendeleo yaenee nchi nzima, ni bora tuweke jitihada za ziada kuwekeza na huko kwingine, ili nako mchango wao kwa taifa uonekane.
Ukiangalia tu hata ramani, pakiwepo bandari yenye uwezo mzuri Tanga, na miundombinu (iliyopo) kama reli na barabara ikaimarishwa, bandari hii itakuwa na umuhimu wa kipekee sana kwenye eneo lote la kaskazini hadi kuelekea kwenye ukanda wa Ziwa, hadi Uganda, DRC na kwingineko.
Hii itakuwa ni bandari muhimu inayofanya kazi kwa pamoja na hii ya Dar.
Tukiimarisha bandari hiyo, sehemu hizo zinazonyemelewa sana sana sasa hivi na bandari ya Mombasa, hawatakuwa na usumbufu tena wa kusubiri mizigo toka Dar.
Usafiri wa ndani ya Ziwa Victoria utawafanya waganda wengi kutegemea bandari hii. Kifupi ni kuwa itaweka ushindani mzuri sana kwa Mombasa.
Sasa hivi Mombasa wanategemea kushika sehemu zote hizo bila ushindani - Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na hata sehemu za ukanda wa ziwa, maeneo haya hatimaye yatashikwa na Mombasa, na hakuna atakayezuia hilo lisitokee.