Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

we ni mnafiki kama wanafiki wenzio waliouza bandari utadhani wao na vizazi vyao wamepata uhamisho kuhamia nchi nyingine na kuishi huko milele!!
 
Unalindajee maslahii wakati yeye ndo main operator?? anyway kiukweli waafrika sisi ni wezi sanaa ila mbona kuna makampuni kama voda wanasimamiwa na wakurugenzi kutoka nchi za wenzetu wanawin tu bora ubadilishe uongozi ila sio kubinafsisha kabisa bandarii... leo unaona watanzania wanaibaa ila amini hao waarabu wataiba zaidi maana wapo na watu wajingaaa ambao unawapa kioo wanakupa almasi. Kuna shirika la elimu kibaha lilikufa huku tunaliona kwa machoo baada ya wazungu kuliweka chini ya uangalizi wa waafrika yote sababu ya wizi so nakuelewa ila linapokuja suala la bandari kumpa mwarabu kisa waafrika wezi haimake sense bhas WAZUNGU WARUDI KUTUTAWALAAA.
 
Akili ya kawaida ni lazima mtu ashangae inakuwaje mgeni afikirie kuendesha bandari ya nchi nyingine lakini akili halisi yenye uzoefu wa hizi bandari haswa hii ya Dar inatosha kwa serikali kuja na wazo hili.

Pia kuna vita ya kutafuta nafasi ya urais wa 2025, imeanza na watu wanaparurana mitandaoni katika hizi mada haswa hii ya bandari kupewa DP World.
 
Hakuna utetezi kwenye hili la DP maana hata mtu asiye na akili sawa hawezi fanya haya...
 
Inasikitisha mno, tena sana!
Badala ya kutafuta maarifa ya kujenga na kuendesha bandari wenyewe, tunatafuta kujengewa na kuendeshewa bandari.

Kwa lugha ya Kinyakyusa tunasema: "Tukuleka ukuloonda amahala gha kulobha iswi, tukusuuma iswi!" Yaani tunaacha kutafuta maarifa ya jinsi ya kuvua samaki, tunaomba tupewe kitoweo cha samaki na wanaojua kuvua!" Tutabaki ombaomba daima milele!!
Mimi naumia na kuumwa sana!
 
Nchi yetu ina viongozi wabinafsi na wenye roho mbaya bora wangempa jirani yetu Kagame.
 
Mimi sioni kama ubinafsishaji ni Tatizo?? shida ipo kwetu sisi wenyewe......

Kagame aliwai kutu insult kua apewe Bandari ya dar es salaam inamtosha kuendesha uchumi wetu wa Tanzania....

Najua Kuna Watanzania wengi smart upstair ambao wameamua kukaa mbali na siasa kwasabb husema siasa ni mchezo mchafu................

Kumbukumbu zinaniambia tulimpaga mkaburu Tanesco enzi za Ben NET GROUP SOLUTION......

NB;
Kama financial analyst ikifanyika na ikatuambia faida ya ubinafsishaji ni Bora mara 100 kuliko kuendesha wenyewe ni Bora wakapewa Kwa mkataba maalum wenye mutual benefits Kwa Kila upande........
 
Afrika ubinafsi na tamaa ni laana inayohitaji mfungo wa maombi ya siku 40, watu wa sacrifice maisha yao kwa maombi labda laana itaondoka
 
Hakuna utetezi kwenye hili la DP maana hata mtu asiye na akili sawa hawezi fanya haya...
Kwa mawazo yako mwenye akili atakubaliana na ufisadi wetu sisi wenyewe usiotufikisha popote?.

Tusikariri kuwa kila mwekezaji anakuja kutuibia, tunavyojiibia sisi wenyewe ni vibaya zaidi kuliko wanavyotuibia hawa wageni.
 
Kwa mujibu wa Kigogo wale waliotemwa bandarini (TICTS) ndio wanaosambaza propaganda za bandari kukodishwa kwa miaka 100 kitu ambacho si kweli. Pia, ubinafsishaji mpya bandarini unaenda kuzima ulaji wa mafisadi wa bandarini ambao walikuwa wakibebwa na mifumo kuiba mapato.
 
Mti wenye matunda mazuri ndio unaoongoza kwa kupopolewa mawe.
 
It will never happen. We jiulize hizi kelele zote za nini. Kuna kitu kitatokea in case watawala wakikaidi. Uzuri wa nchi yetu ina mkono wa Chuma hasa baada ya mzalendo Dkt Magufuli kujenga ujasiri wa watu kuhoji na kujiamini. Hivyo ondoa wasiwasi Sultan Mangungo Story will never repeat! Wao wenyewe viongozi wanajua kabisa the burning fire in the middle of nowhere.
 
Hebu thibitisha ni wapi inaonesha bandari imebinafsishwa miaka 100
Hebu tusaidie na sisi wengine kufahamu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…