Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Wapi Bunge limejadili?
hilo bunge Mungu alilaani kwa kukubali uzandiki uendelee ndani ya nchi karne hii.ni bunge la hovyo ambalo halijawahi tokea tangu tupate uhuru.tuhamasishane katiba mpya pamoja na kuwaondoa kwenye sanduku la kura wabunge wote wa bunge hili.leo nimesikia tbc radio serikali inawaondoa wananchi wote waliovamia ardhi ya zanzibar pale bagamoyo.nimejiuliza sana tena kwa uchungu inakuwaje zanzibar wanakuwa na ardhi bagamoyo?Mungu inusuru nchi hii na haya majanga ambayo yana athari kubwa huko mbeleni.
 
apo maana yake ni kwamba nchi inakuwa uchi kwa mfano jeshi letu linataka kuingiza siraha mpya au mitambo ao waarabu watajua kilakitu..
 
Kakoko alikuwa mtu sahihi, wa kuongoza bandari. Angeweza dadavua huo mkataba kinaga ubaga; tija ipo wapi.

Fair to current management ya TPA wamejaribu kuita waandishi wa habari kuelezea upande wao kwanini wanahitaji uwekezaji. Shida ni kwamba TBC, Azam na vyombo vingine ambavyo avijali cheap shorts awakuona umuhimu wa kuhudhuria.

Personal sijapenda vipande vya habari ambavyo Global TV na Millard Ayo vimeamua ku cover; based on what on what they thought it was important content.

Naelewa kwa upande wao, muhimu ni kuweka vitu wanavyodhani jamii inataka kusikia kwa uelewa wa uwezo wetu wa data usage na kukata mengine. But then if you are deeper you feel awakumtendea haki mkurugenzi na wasikilizaji kwa kutoa full interview.

That is why you need TBC involvement au taasisi husika kuwa wana channel zao kuhakikisha full interview is heard.

Not that ni wazalendo; mimi binafsi naamini Kakoko was the best.
Mbona wanauza vya Tanganyika tu ?
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona wanauza vya Tanganyika tu huko kwao hawana cha kuuza ?
 
NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
____________________
Kuna nyakati huwa Natamani Sisi Watanzania Kuwaomba Msamaha mababu zetu akiwemo Chief Mangungo kwa KUWACHEKA na Kuwa na HASIRA nao kwa kuingia Mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa Kikoloni Karne ya 19.

Ni wazi kabisa kizazi chetu cha sasa kila kinaporejea kusoma namna mababu zetu walivyoingizwa Kingi kwenye mikataba ya ulaghai hasa kwa kumrejea Chief Mangungo wa Msowero hucheka na kuona walikuwa wajinga kiasi gani mpaka wakubali?

Lakini mababu hawa kina Chief Mangungo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali yaani hawakuwa na exposure, mababu hawa walidanganywa kwasababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa.

Kizazi hikihiki cha baada ya Ukoloni, kizazi chenye elimu, kizazi kinachojua lugha zote rasmi duniani, kizazi cha kidigitali, kinashindwa kujiuliza na kuhoji na kuwacheka viongozi wake ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miaka ya zaidi ya 100 ambayo ndani yake kuna athari za kizazi na kizazi. Mikataba inayokuwa inamnufaisha mwekezaji zaidi na kuwanyonya wazawa.

Mikataba inasainiwa na viongozi waliosoma na kusomeshwa kwa fedha za umma na wana Degree, Masters na PhD, mikataba wanayosaini ni ya kinyonyaji na ya hovyo lakini mikataba inatetewa kwamba wawekezaji hawa wataongeza ajira na kizazi cha Kisomi kinafurahia na kushangilia, hakuna kuhoji, hakuna kuuliza. Ajira zinazoongezwa ni za Malipo ya bora mkono uende kinywani. Ajira zisizo za ukombozi wa kiuchumi.

Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Hivi mbele ya kizazi chenye wasomi lukuki viongozi wanathubutu kusaini mkataba wa kuuza bandari ya Dares salaam kwa miaka mia moja?
Je, mkataba kama huu, ulisainiwa na Mangungo? Kwanini tuwacheke wazee wetu ambao hawakuwa na elimu yoyote?

Natamani Kuwaomba msamaha kina Chief Mangungo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.View attachment 2648183
Serikali ya tanzani imejaza viongozo wala rushwa na wezi
 
Kama watu ndiyo wajinga kama nyie bora bandari ibinafshwe Tu
Ungejua kwanza mimi sinaga ushabiki na mtu au vitu...Am afree mind personality, we kikitajwa jina la JPM unahemka tu bila kujali katajwa kwa lipi? Is he your idol?
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaheri mama Tanganyika karibu utumwa kwa hisani ya Samia.
 
Mbona Serikali inatuchanganya? Which is which? Who when why?

Mkataba wa Mwaka au Jiti? Faida ya Trilioni 14 zinaatikanaje kwa huo mwaka? Maana ufafanuzi unasema Waarabu wataongeza mapato kutoka 7T mpaka 21T kwa mwaka.
 
Aise kwa kweli Tanzania sasa inaliwa. Kweli Bunge letu mmeridhia??? Kipi tumeshindwa kusimamia wenyewe.? Ndege tumeshindwa, bandari tumeshindwa,mbuga zetu tumeshindwa,migodi tumeshindwa,VIWANDA tumeshindwa, n.k. je sisi tunaweza kusimamia Nini???nchi hii tunaipiga mnada tu, kuna Nini Dubai?? Masikini TANZANIA 🤔🤔
Nchi hii hakuna tunachoweza labda ufisadi. Nitajie kitu kimoja tu ambacho kama Mtanzania unaweza kusimama mbele ya dunia ukajipiga kifua kuwa tumeweza kukiendesha kwa ufanisi. Nipo nimekaa paleeee!

Yakianzishwa mashindano ya ufisadi tunaibuka videdea bila kupingwa hata Wanaija safari hii tunawakalisha dadeki! 🚮🚮🚮
 
Kinachonishangaza ni hiki hiyo Bandari hatuwezi kuindesha wenyewe mpaka tuwape watu wengine na kwa nini vinafanyika vitu ambavyo kwa macho tuu unaona havina faida kwa Watanzania na vinakubaliwa ni kwa faida ya nani kweli Bandari tuu inatushinda tutaweza kufanya nini? Vijana wapo mtaani huko wanazagaa kama vile Nchi sio yao harafu waliopewa dhamana wanaingia mikataba isiyoeleweka kwa nini hiyi mikataba isijadiliwe Bungeni kama ni faida ya Wananchi na sio Watawala wanaogopa nini?
 
Nchi hii hakuna tunachoweza labda ufisadi. Nitajie kitu kimoja tu ambacho kama Mtanzania unaweza kusimama mbele ya dunia ukajipiga kifua kuwa tumeweza kukiendesha kwa ufanisi. Nipo nimekaa pale!

Yakianzishwa mashindano ya ufisadi tunaibuka videdea bila kupingwa hata Wanaijeria safari hii tunawakalisha! 🚮🚮🚮
Mkuu kusimamia Bandari mimi sioni kama ni kazi sana mpaka tuwape watu au mimi pana vitu sielewi kuhusu bandari yetu...
 
Back
Top Bottom