Baada ya janabi kushinda naona taasisi za kiislamu zinampongeza tofauti na alivyoshinda ndungulile

Baada ya janabi kushinda naona taasisi za kiislamu zinampongeza tofauti na alivyoshinda ndungulile

Hii umenisgangaza sana sijajua kwanini wakuu labda wengine mnifafanulie naona baada ya kushinda janabi kuwa mkurugenzi wa WHO africa naona taasisi nyingi za kiislamu zinampongeza tofauti na ushindi wa ndungulile naona taasisi nyingi za kiislamu zilikaa kimya ila taasisis za kikiristo ndizo zilimpongeza je huu ni udini? Au waislamu wako proud baada ya ushindi wa janabi? Je ile tafasiri ya watu wa dini nyingine ya kusema waislamu hawataki elimu dunia naona imewaishia na je watu wa dini nyingine wamechukia baada ya ushindi wa Dr janabi?
Tumshukuru mheshimiwa rais daktari profesa SSH kwa kuonyesha tabia nzuri za kiislam duniani. Aliyeshinda si Janaba bali SSH.
 
Wewe andika utakavyo andika, lakini huo ukweli hauwezi kubadilika. Sababu hili hata aliyewaumba na anaye wajua vizuri amelisema hili.

Nukta.
Acha hizo wewe aliyetuumba unamjua au mbwembwe za ki Quraish,
Ukweli gani weweee aaah acha Viroja basiii!
😁😁
 
Mambo mengine na Sisi wakristo tuwe tunakaa kimya... Professor Janabi kupongezwa na waislam wenzie ni Jambo la kawaida Tu...
Prof Janabi ni mtanzania.Mimi ni mkristu na najisikia fahari kubwa kwa yeye kuaminiwa na kupigiwa kura za kutosha.Ukisoma majukumu yake mapya,hutaona kama dini yake iwe mjadala.
Hongera Janabi !Hongera Tanzania!
 
Hii umenisgangaza sana sijajua kwanini wakuu labda wengine mnifafanulie naona baada ya kushinda janabi kuwa mkurugenzi wa WHO africa naona taasisi nyingi za kiislamu zinampongeza tofauti na ushindi wa ndungulile naona taasisi nyingi za kiislamu zilikaa kimya ila taasisis za kikiristo ndizo zilimpongeza je huu ni udini? Au waislamu wako proud baada ya ushindi wa janabi? Je ile tafasiri ya watu wa dini nyingine ya kusema waislamu hawataki elimu dunia naona imewaishia na je watu wa dini nyingine wamechukia baada ya ushindi wa Dr janabi?
Kwahiyo mnataka kuwapangia watu hisia zao?

Hongera kwake…. Hata sisi wakristu tuko happy
 
Kuna namna flani, humu JF, Kuna kampeni kuuubwa sana ya kuwaponda Waislamu........nafuatilia nyuzi nyiingi sana! Ukiangalia nyuzi hii na comments nyingi, Ina Siri yake nyuma; ni kama watu flani wamejipanga hv kushambulia hilo kundi la waislamu. Wamepongeza kina nani?!!!! Wamepongezaje?!!

Mada inasema wakristo hawajampongeza janabi lakini hata hauoni mashambulizi kwa wakristo wakati tunaambiwa walimpongeza ndugulille. Hata kichwa Cha habari kimeanza na shutuma dhidi ya Waislamu.
 
Hii umenisgangaza sana sijajua kwanini wakuu labda wengine mnifafanulie naona baada ya kushinda janabi kuwa mkurugenzi wa WHO africa naona taasisi nyingi za kiislamu zinampongeza tofauti na ushindi wa ndungulile naona taasisi nyingi za kiislamu zilikaa kimya ila taasisis za kikiristo ndizo zilimpongeza je huu ni udini? Au waislamu wako proud baada ya ushindi wa janabi? Je ile tafasiri ya watu wa dini nyingine ya kusema waislamu hawataki elimu dunia naona imewaishia na je watu wa dini nyingine wamechukia baada ya ushindi wa Dr janabi?
We una virus wa udini, unapataje muda wa kufuatilia petty issues km hizo? Mtu km hajakupongeza unamlaumu? Usilazimishe hisia za watu, fanya mambo yako songa mbele. Muhimu km Taifa litafaidika inatosha.
 
Hii umenisgangaza sana sijajua kwanini wakuu labda wengine mnifafanulie naona baada ya kushinda janabi kuwa mkurugenzi wa WHO africa naona taasisi nyingi za kiislamu zinampongeza tofauti na ushindi wa ndungulile naona taasisi nyingi za kiislamu zilikaa kimya ila taasisis za kikiristo ndizo zilimpongeza je huu ni udini? Au waislamu wako proud baada ya ushindi wa janabi? Je ile tafasiri ya watu wa dini nyingine ya kusema waislamu hawataki elimu dunia naona imewaishia na je watu wa dini nyingine wamechukia baada ya ushindi wa Dr janabi?
Mimi siyo muislsmu lakini naweza kuwapita Waislamu wengi tu tukifuata dini.

Nimeshachangia harambee tofauti za misikiti na nimenunuwa majuzuu kusaidia Madrasa.

Sasa mwislamu mwizi mla pesa za wajane na yatima ana Uislamu gani? (Simsemi Janabi)

Kinachotusumbuwa sisi Watanzania ujinga katika wale maadui watatu wote bado tunao.

Leo hii utashangaa kundi la wanazuoni wa kiislamu wanahutubiwa na mwanamke kisa ni Rais wakati waziri mkuu mwislamu yupo.
 
Wao w
hawatanufaika chochote mambo ya uisilamu wapi na wapi?
anachosema si kunufaika ila wao wanasema ninyi wakristo mlikuwa mnawasema waislamu hawaitaki kusoma elimu dunia je janabi ile ni elimu gani?
 
Unajua kuna wakati huwa tunaamua kunyamaza kimya tu

Kuna kama namna fulani ya Uislamu kupigwa vita au kuandaamwa

Je,ni mara ngapi zinaanzishwa nyuzi za kupondwa waislamu,lakini huwezi kutukuta sisi tunaanzisha kuutukana au kuuchalenge ukristo,kama zipo nyuzi ni kidogo sana

Kuna nyuzi nyingine mpaka unaogopa hata kusoma wala kuchangia kwakuwa tumeaswa sana Waislamu tunapoona upuuzi unazungumzwa basi tukae kando,Kuna nyuzi iliandikwa kuhusu Nabii Muhammad swalla aallahi alahyi wa aalih wa sallam kuwa sijui hajataihiriwa,unajiuliza hivi tumefikia wapi?

Kwakuwa ni upuuzi basi hata kusoma tunaacha tunapita kushoto

Kama sisi ni mbumbumbu tuna elimu zetu za madrassa sasa kwanini kutwa kucha tupo katika midomo yenu?

Kama sisi elimu yetu ya kuungaunga basi si mtuache tupongezane wenyewe wa kuungaunga,shida iko wapi?

Yani ajabu sana tunaonekana wa daraja la mwisho,hatuna mapofressor,hatuna wasomi wengi,sasa kinacho washughulisha nyie ni nini kwa watu duni kama sisi?

Kwa wale wakristo ambao mnajitambua nawashukuru sana,kwani nyie walau mnajitahidi kuwa na subira na uvumilivu wa kuficha hisia zenu juu ya Uislamu ingawa ndani yenu mnawaka moto

Hili sisi hatubahatishi ila Allah alishasema katika qur'an kuwa Wakristo na wayahudi hawatakuwa na radhi nanyi mpaka muingie katika mila zao

Sisemi haya kwa ubaya ila ni hali halisi.
 
Nani awe na Chuki na mbumbumbu wa Mecca acheni kujistukia hakuna mkristo serious anawachukia Waislamu ila asilimia kubwa hua naona Wakristo wakiwahurumia Waislamu Maana kundi kubwa la Dini yenu ni ngumbaru first class,
Hiyo Chuki kwa mkristo imeanza lini kama Sio nyie wazee wa kujilipua na jazba za kijuha Ndio sera yenu?
Maghayo
😁😁😁

Mna chuki na husda nyinyi. Mtawatukana na kuwakashifu Waislam hawajasoma sekula, mtawatukana kuwa hawana akili. Halafu wakipambana katika biashara zao, Allah akawafungulia mtaanza kulia lia wanaendekeza "udini" katika mambo yao kama Bakhresa. Sasa wao hawajasoma, hawana akili na wako nyuma, kama mnavyodai, kama wakinyanyuana mbona mnaumia? Nyinyi si mna akili na maisha yenu yako juu kuliko wao? Na hata Waislam kumpongeza ndugu yao mnaumia!

Mtoto wa Madrasa kapata sehemu tu ya dunia yenu mnayoitolea macho (dunia ambayo kwenu ndio Pepo yenu) mnaumiiia. Allah ambariki ndugu yetu Profesa Janabi na atuongoze sisi na yeye katika njia iliyonyooka.

Kama Muislam mtamtukana kwa Dini yake pale anapokosea, na sisi tunamsifia kwa Dini (Uislam wake) anapofanya vizuri, sio mtu akifanya vibaya basi ni Muislam, akifanya vizuri ni mtanzania huyo sijui "msilete Udini".
 
Back
Top Bottom