Unajua kuna wakati huwa tunaamua kunyamaza kimya tu
Kuna kama namna fulani ya Uislamu kupigwa vita au kuandaamwa
Je,ni mara ngapi zinaanzishwa nyuzi za kupondwa waislamu,lakini huwezi kutukuta sisi tunaanzisha kuutukana au kuuchalenge ukristo,kama zipo nyuzi ni kidogo sana
Kuna nyuzi nyingine mpaka unaogopa hata kusoma wala kuchangia kwakuwa tumeaswa sana Waislamu tunapoona upuuzi unazungumzwa basi tukae kando,Kuna nyuzi iliandikwa kuhusu Nabii Muhammad swalla aallahi alahyi wa aalih wa sallam kuwa sijui hajataihiriwa,unajiuliza hivi tumefikia wapi?
Kwakuwa ni upuuzi basi hata kusoma tunaacha tunapita kushoto
Kama sisi ni mbumbumbu tuna elimu zetu za madrassa sasa kwanini kutwa kucha tupo katika midomo yenu?
Kama sisi elimu yetu ya kuungaunga basi si mtuache tupongezane wenyewe wa kuungaunga,shida iko wapi?
Yani ajabu sana tunaonekana wa daraja la mwisho,hatuna mapofressor,hatuna wasomi wengi,sasa kinacho washughulisha nyie ni nini kwa watu duni kama sisi?
Kwa wale wakristo ambao mnajitambua nawashukuru sana,kwani nyie walau mnajitahidi kuwa na subira na uvumilivu wa kuficha hisia zenu juu ya Uislamu ingawa ndani yenu mnawaka moto
Hili sisi hatubahatishi ila Allah alishasema katika qur'an kuwa Wakristo na wayahudi hawatakuwa na radhi nanyi mpaka muingie katika mila zao
Sisemi haya kwa ubaya ila ni hali halisi.