Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

kama mama kasema hivyo, basi kweli anaupiga mwingi..anazidi kukua kisiasa kwa kasi ya 5G.
 
Well Said
 
Umenena vyema !
 
Kashtuka na kagundua Bashiru si wa kisport sport, yahitaji umakini kumwendea Bashiru. Japo najua kaisema kinafiki naamini moyoni kakwazika sana na Bashiru, yafaa Bashiru akae chonjo
Wanasemaga wasiwasi ni Akili !! Kukaa chonjo ni muhimu. !!
 
Wao wangekuwa wanasifia sisi wananchi kwa kulipa kodi vizuri ili mambo ya serikali yaende vizuri.
Wakumbuke pia kwamba wananchi wasipolipa kodi vizuri, Serikali inakosa pesa kwenye hazina yake.
 
Shida ilianzia kwa jpm ambaye alianzisha mpaka kipindi TBC Cha eti kishindo Cha jpm. Yule baba alikuwa anapenda masifa Sana yasiyomstahili kabisa na mwasisi wake alikuwa Dr Bashiru.
 
Wakuu wa mikoa wangejiunga jf wangejifunza mengi na wangekwenda na wakati. Wengi wako na mawazo ya awamu ya tano ya kusifu na kibudu.
 
Shida ilianzia kwa jpm ambaye alianzisha mpaka kipindi TBC Cha eti kishindo Cha jpm. Yule baba alikuwa anapenda masifa Sana yasiyomstahili kabisa na mwasisi wake alikuwa Dr Bashiru.
Kama mtangulizi wako alikosea sana haina maana na wewe ni halali kipitia njia zile zile !
 
Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.[emoji23]
 

Umeongea ukwell hapa. Hii tabia ya kuwapa watu uongozi kwa ajili wanajua kusifu au kuwanyamazisha wasitoe hoja kinzani kwa serikali au kiongozi haina faida kwa Taifa.

Itafutwe namna nyengine ya uwezo wa muhusika kafanya nini na kukifanikisha katika majukumu aliyopewa huko nyuma. Hii itaondoa kwa sehemu kubwa tabia hizi za unafiki wa kujipendekeza kwa ajili eti kufikiriwa kupata cheo. Mh Rais kaonesha ujasiri kuwapa ukweli wao. Na huu ukweli utamuweka huru kweli kweli kwa kuwa atajipunguzia mzigo wa kuwabeba wakujipendekeza wasio na uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…