Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Kama ccm unataka kuvuka salama 2025 lazima ifanye uchaguzi mzuri Sasa wa viongozi waandamizi kuanzia makamu wa Rais, kushuka Chini ambao wataenda kumsaidia Rais kubadili taswira ya nchi. Kuendeleza baadhi ya mambo aliyoasisi Magufuli lakini pia kuyakataa na kuyabidili Yale yaliyoyoleta maumivu kwa wananchi.

Miradi aliyoanzisha Magufuli ni mingi na mikubwa na inayohitaji fedha nyingi na njia pekee kuikamilisha lazima uchumi ukue kwa Kasi na mapato yakue tupunguze kukopa. Sasa kuyafikia haya lazima kuwe na visionary leaders na wenye passion na maendeleo ya watu kuliko vitu.
 
Hili ndio jaribio la kwanza kubwa kwa Taifa hili baada ya JPM kututoka. Mungu wa mbinguni awasaidie watakao endesha huu mchakato wa kumpata Naibu wa mh Rais Samia. Wakikosea kubalansisha the equation imekula mazima kwao.

Tukumbuke yale mapinduzi ya pambio chamani. Kilicho saidia wakati ule ni kuwa JPM alikuwepo na alitumika kama karata ya turufu or buffer solution after the event. Nani ni karata ya turufu kwa Umakamo/who would be a buffer solution in the time around?

Deep State Msituangushe, jamani msiliangushe Taifa hili linawahitaji pengine kuliko wakati mwengine wowote huko kipindi cha nyuma. Simameni imara jivikeni ujasiri mkiwa na maamuzi ya pamoja na yenye maridhiaano ya kuliweka hili Taifa mbele kwanza na maslahi binafsi nyuma. Mkifanya hivyo mtakuwa mmewasaidia sana Watanzania wenzenu na vizazi venu.
 
Tulikuaga na Jakaya na Shein, Jakaya na Gharib Bilali..

Kipi ulipunguza? Ambacho wakati wa Magufuli na Samia ulikiongeza?
Kikwete aliwahi kuwa na makamu mkristo?
Kosa lenu mmeangalia nafasi 2 tu ya rais na makamu mimi nimeangali nafasi zote mpk waziri mkuu kwa hizo tawala mlizojengea hoja waziri mkuu alikuwa upande gani halafu mlinganishe na sasa kwa hiyo hiyo nafasi lzm awe mkristo tena wa kutoka bara kama waziri mkuu akibaki yuleyule.
 
Chuki zako dhidi ya Waislamu unazitoa wazi wazi .Unaonekana weye ni mdini na una chuki na hikdi juu ya Waislamu Allah akuangamize watu kama weye na mfano wake.Laana za mungu ziwe juu yako hawa watu wabaya sana.
Hayo ya chuki ni yako wewe mimi nimeangalia namna ambavyo mara zote imekuwa ikitendeka hivyo ktk tawala zote nikatoa nami mtazamo wangu
 
Kigezo cha kwanza kwenye majina lazima awe mkristo ili kubalance haiwezekani wote wakawa waislamu haya tuanze upya kufikiria
Kigezo mfu na muflisi kwenye siasa na akili ya kiuongozi. Only in African thinking.. Why kufikiria hiki, unabalance ili iweje..Africa tunarudi sana nyuma kwa kufikiria huu ijinga kumpa mtu nafasi hata kama hana vigezo vinavyotakiwa kisa dini au kabila..
 
Mimi nashauri kwenye nafasi hii ateuliwe moja kati ya viongozi toka vyama vya upinzani ili kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa ambao kwa miaka ya hivi karibuni uliingia dosari na kutugawa kama watanzania
 
Back
Top Bottom