Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Makamu
Bila shaka kwa nafasi hii watu hawalali, Lumumba na viunga vyake, baraza la Mawaziri nalo lipo tumbo joto maana lazima pangua pangua itakuwepo, kwa nafasi ya VP hapo January ndio chaguo la mama, kiufupi CCM ya asilia inarudi, MATAGA mwisho rasmi umefika.
Makamu mwislam, rais mwislam ,unamanisha nini?
 
Tena wanga sana hawa Wakubwa, huyu aliye anzisha hii post/thread anatakiwa awe wodini pale milembe-wodi namba 5, maana si kwa mawenge haya! Hatuja zika wewe unakuja ushuzi huu wa kipumbavu, hebu acheni banaaa!
Mahiga alifariki 1may 2020,siku inayofata kabla hata hajazikwa, marehemu Magufuli, akamchagua mwigulu kuchukua nafasi yake, Uwezi kuzuia watu kujadili nani anafaa kuwaongoza!! Wala Uwezi kuwachagulia muda wa kujadili, ameshakufa uyo, Nchi haiwezi kusimama.. mijadala ni muhimu.
 
Viti vya Wahudhuriaji wa Msiba havijapangwa bado hadi Ratiba ya Msiba (Mazishi) haijapangwa tayari mmeshaanza kuja na hopeless Speculations zenu, hivi mkiambiwa nyie ni Wachawi mtabisha au Kukataa?
Mpwa kaenda zake..... Polee mkuu[emoji26][emoji26][emoji26]
 
Bila shaka kwa nafasi hii watu hawalali, Lumumba na viunga vyake, baraza la Mawaziri nalo lipo tumbo joto maana lazima pangua pangua itakuwepo, kwa nafasi ya VP hapo January ndio chaguo la mama, kiufupi CCM ya asilia inarudi, MATAGA mwisho rasmi umefika.
Huiskitikii Tanzania unawaza MATAGA tu.

MATAGA wana ngozi nyingi.
 
Poleni Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na kiongozi wetu Mahiri Mh joseph magufuli . Ni kiongozi aliyepigania wanyonge .ameiweka nchi ktk msingi mzuri ktk kila sekta.

Tumeshuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa kwa maendeleo ya taifa letu. Narejea ktk heading yangu Taifa linahitaji mtu wa kufanana na Magufuli ambapo ahadi zake kwa wananchi zinatekelezeka. Mtu huyu si mwingine bali ni Mh Paramagamba kabudi huyu ni zao la Rais magufuli ni mtu makini ktk kazi yake yupo serious na ni mkali tunahitaji mtu wa kuendana na Magufuli
 
Nasikia Wasukuma wanataka hiyo nafasi kwa udi na uvumba. Waziri wa ujenzi ndio chaguo lao ikishindikana basi hata Askofu Rashid au Makonda.
Umeishiwa wewe, leta hoja weka pembeni ukabila. Wasukuma kama tungekuwa tumependelewa wote si tungekuwa madarakani sasa?
 
Back
Top Bottom