Una uhakika mzee ya kwamba January ndiyo chaguo la mama ?
 
Doctor Slaa anafaa kabisa kuvaa viatu vya Magu, mtizamo wangu angepewa u makamu wa Rais ange endana na matakwa yetu, kwa upande Mwingine kassim majaliwa yupo vzr Sana Ila sitaki kumuondoa pale Kati maana tunahitaji mtu makini wa kusukuma jahazi Kama waziri mkuu
 
Sema kwakuwa kazi yenyewe ya umakamu wa rais kwa hapa bongo haina issue zaidi ya kukata utepe kwenye zinduzi basi. Hata awekwe nani kwa katiba hii atakuwa hana nguvu kimamlaka.
Makamu wa rais ana umuhimu mkubwa sana ila hapa bongo kwenu ndo mnam-profile kidogo kidogo
 
Hivi tunamchagua mtu kwa ajili ya uwezo wake au kwa ajili ya dini yake ?
Kigezo ni uwezo lakini vipi linapokuja kwamba wapo wenye uwezo katika dini zote hizo mbili kubwa?

Kama kuna Wakristo wengi wenye uwezo na hawapo katika nafasi zote kubwa za juu kwanini uendelee kuwaweka Waislam ambao tayari wameshikilia nafasi zote za juu kwa bara na visiwani?
 
Suala la dini lisipewe nafasi.
Kwani wanaenda kuhubiri huko?
Tena waislamu wangepewa nafasi zote ili kupunguza malalamiko
 
Hii nafasi haina ushawishi wowote.
Ni ya washika mikasi kuzindua miradi kama alivyokuwa akifanya Gharib Bilal
 
Kigezo cha kuwa VPURT haijawahi kuwa uwezo. Kigezo kikubwa ni upande wa Muungano anaotokea na busara za kumsaidia Rais bila kumhujumu au kutamani kuwa na mamlaka ya Rais au Maarufu kuliko Rais au kutaka kumrithi Rais.
Hivyo ndio vigezo. Na ndio maana nashawishi nafasi hiyo apewe veteran mojawapo.
 
I wish vice president awe wa kanda ya ziwa au wa pwani/Tanga


πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯
Ninyi ndio wale wenye roho ya mgawanyo. Je, kanda ya Magharibi nao wakisema they wish atokee Kigoma au Katavi? Wa Mtwara nao? Hili ni Taifa moja lisilo na vipande. Hata hiyo kanda ya ziwa ina kibao kama ukianza kutambua viongozi kwa kanda zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…