Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mheshimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Mgosi Makamba apewe wizara ya mambo ya nje akijiandaa kwa ajili ya 2025.
 
1. Jakaya Mrisho Kikwete, apewe umakamu wa rais

2. Butiku

3. Kimei

4. Kinana

5. Warioba

6. Prof Muhongo

7. Makinda

7. Mwamunyange

8. Lissu

9. Chikawe

10. Mwandosya

Hao akina January, mwigulu sijui kabudi bado sana. Anatakiwa mkongwe na mwenye busara ya kumwongoza mama kuliweka taifa pazuri
Hivi mkuu kweli unafatilia hata katiba ya nchi yako? Mtu akishakuwa Rais wa JMT hawezi kushika madaraka yoyote ya kiutumishi serikalini akishastaafu.

Jakaya Kikwete awe makamu wa Rais seriously?
 
January Makamba

Advantage ana misimamo akisema A ni A hakuna kingine.

Disadvantage anawaza upuuzi sana kichwani kwake saa zingine, not realistic on priorities za 3 world country.

Huyo mtu hafai kwa nchi inayotaka kujikomboa kiuchumi, he never saw eye to eye na Magufuli.

NEMC kutoa vibali vya go ahead chini yake ilikuwa shida. Yote kutokana na upuuzi wake wa extensive environmental impact assessment zinazo chukua muda mrefu kukamilika.

Makamu wa raisi apewe Kassim Majaliwa alimuelewa Magufuli.
 
Chuki zako dhidi ya Waislamu unazitoa wazi wazi .Unaonekana weye ni mdini na una chuki na hikdi juu ya Waislamu Allah akuangamize watu kama weye na mfano wake.Laana za mungu ziwe juu yako hawa watu wabaya sana.
Mbona laana tena? Watu wazungumze hoja, majibu yako yanaonyesha chuki uliyonayo wewe
 
Mimi nashauri kwenye nafasi hii ateuliwe moja kati ya viongozi toka vyama vya upinzani ili kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa ambao kwa miaka ya hivi karibuni uliingia dosari na kutugawa kama watanzania
Nani wa kuteuliwa kutoka upinzani?
 
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mheshimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Si nilisikia ni Andrew Chenge? but Kabudi angefaa kabisa.ila sometimes ni maajabu.Maana mwenyewe alishasemaga asingeruhusu raisi ajaye awe mzee
 
Mi nashauri Mh. Samia amtafute makamu wake ambaye ni mchumi mmbobezi ambaye amtamsaidia kuurudisha uchumi kwenye mstari, lakini mtu mwenye ufahamu wa diplomasia vizuri itamsaidia pia kuurudisha mahusiano na nchi marafiki na mwisho mtu walau mwenye uzoefu wa shughuli za serikali.

Possible candidates include former CAG, former Katibu mkuu kiiongozi Sefue,

Proffesor Mkenda, Mizengo Pinda.

Mheshimiwa aepuke kutea makada ambao wanaweka chama mbele na sio taifa

Mizengo pinda akafuge nyuki si kuonyesha njia
Hapa ni Kabudi
 
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mheshimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Ni aibu! Mnaanza kugimbania vyeo tangu siku ya kwanza ya maombolezo! Haraka ya nini? Huyo uliyempendekeza tayari umeshamharibia! Ni kama mlikuwa mnatamani msiba utokee ili mpate nafasi!! Watanzania tuna akili!
 
IMG-20210318-WA0000.jpg
 
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mheshimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Paul Makonda
 
Back
Top Bottom