Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Majina ambayo nakuomba ukiletewa tu uteue wa Kukurithi tafadhali yachane upesi na ukiweza Mzabe hata Kofi au mpige Kichwa cha Kagere aliyekuletea ni haya...

1. Mwigulu Nchemba
2. Paul Makonda

Majina ambayo nakuomba ukiletewa Mezani Kwako tu ili umteue wa Kukurithi yapokee, furahi na mwambie Mwenyezi Mungu Asante ni haya....

1. Palamaganda Kabudi
2. William Lukuvi

Na nyie wana CCM chagueni kati ya Kabudi au Lukuvi ili amrithi Mama Samia wakati Mama Samia nae akishaapishwa rasmi kuwa Rais aanze na Kazi ya kurejesha Upendo, Amani na Mshikamano baina ya Watanzania wote ambao ulitoweka ghafla tangia 2016 na upo tu Kinafiki Nyusoni mwetu hadi leo.
 
Mi nashauri Mh. Samia amtafute makamu wake ambaye ni mchumi mmbobezi ambaye amtamsaidia kuurudisha uchumi kwenye mstari, lakini mtu mwenye ufahamu wa diplomasia vizuri itamsaidia pia kuurudisha mahusiano na nchi marafiki na mwisho mtu walau mwenye uzoefu wa shughuli za serikali.

Possible candidates include former CAG, former Katibu mkuu kiiongozi Sefue,

Proffesor Mkenda, Mizengo Pinda.

Mheshimiwa aepuke kutea makada ambao wanaweka chama mbele na sio taifa
Jina limetoka IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Tuendelee kuchapa kazi kwa kuenzi mazuri ya JPM
 
Hizo kura mgekuwa mmezipata kihalali hoja yako ingekuwa na mashiko.

Wewe mwenyewe unajua kuwa kura mliziiba tu.

Kipindi cha mzee Mwinyi mbona hakuteua msukuma kuwa VP ?

Wacha kujidanganya nakushauri kubali matokeo hata kama mtapatiwa angalau waziri atawatosha.
Muda utasema. Huu ni wakati wa siasa za vyama vingi, ndio maana hata Lisu alitumia muda mwingi wa kampeni kanda hiyo, unafikiri ni mjinga.
 
Bila shaka kwa nafasi hii watu hawalali, Lumumba na viunga vyake, baraza la Mawaziri nalo lipo tumbo joto maana lazima pangua pangua itakuwepo, kwa nafasi ya VP hapo January ndio chaguo la mama, kiufupi CCM ya asilia inarudi, MATAGA mwisho rasmi umefika.
Viti 10 angetengua akavigawa kwa upinzani kwa uwiano wa kura walizopata uchaguzi mkuu.
 
mi naona CCM iweke ma kando kando yao pembeni wampe tu kijana January Makamba - hasa wakikumbuka alikuwa kwenye top 5 wakati wa kumsaka Rais wa Tanzania... na ana uwezo mkubwa ukilinganisha na hao walamba viatu.
Nakuunga mkono 100%
 
Iteengenezwe Serikali ya mpito wazee wetu wafanye combination Mambo yakishatengamaa protocol ifuate haya ni maisha yetu hayatakiwi kufanyiwa majaribio.Tumeona wenyewe mziki ulivyopigwa,game haikuwa ya kitoto,
Haya ni maisha yetu hayatakiwi kamwe kufanyiwa majaribio.
Amen
 
Back
Top Bottom