Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
January kalifanyia nini taifa letu kama siyo usanii tu. Watanzania mbona tunakuwa wajinga hivi? Tanzania imejaa watu wengi wenye akili na vision wewe unasema huyo msanii? Huyo na Makonda au Gwajima wana tofauti gani?
Watz mln 50 umewaona hapa?
 
Nafasi ya umakamu inaweza kuwadondokea chenge, pinda, nchimbi au lukuvi kuzingatia uzoefu wao katika siasa na ajenda ya ukristo japo si kigezo cha kisheria
 
Ndugu kifo fursa kwa wengne,hukumbuki aliyelala alivyomteua mrith wa Mahiga kabla ya kuzikwa?
Viti vya Wahudhuriaji wa Msiba havijapangwa bado hadi Ratiba ya Msiba (Mazishi) haijapangwa tayari mmeshaanza kuja na hopeless Speculations zenu, hivi mkiambiwa nyie ni Wachawi mtabisha au Kukataa?
 
Hapo una-assume Majaliwa anabaki kuwa Waziri Mkuu? utashangazwa
At least mkuu wewe umewaza sawa na mimi wengine wanapapalika tu kuniquote wakiishia kwa hao top 2 mara sijui kikwete nini wakisahau kwa Kikwete waziri mkuu alikuwepo Lowasa na baadaye Pinda, ila hata ikitokea changes kwa Pm bado hilo litazingatiwa
 
Hahaa
Balozi Mahiga alifariki tar 1 May 2020, kesho yake tar 2 May Rais akamteua Nchemba kuziba hiyo nafasi (kabla hata ya mazishi).

Naamini huko Magufuli aliko, angependa tumuenzi kwa kuziba nafasi hizo haraka sana tena kabla ya mazishi.
 
Shirika la Habari -Kigogo.

Lina ripoti Dr. Emmanuel Nchimbi.

Hata mm naona jamaa ni mature. Afu hamna mdomo sna. Ame komaa hana utoto wa akina Nape na January!
 
Kwa sababu ni mngoni mwenzako? Hatuko tayari kurudia makosa. Taja sifa zake hapa. Kinyume na hapo, mshauri abakie huko huko! Hatutaki kabisa watu wanafiki nawachumia tumbo safari hii.
Pigia mstari.. " Hatuko tayari kurudia makosa" .. awekwe kwenye mizani kama anafaa ama hafai.

Nimeona pia wanamtaja Anthony Mtaka.. awekwe pia kwenye mizani
 
Mwigulu hapana, hana busara

Naamini Mwigulu, Kabudi, na Mpango, wanawakilisha makundi makubwa ndani ya ccm.

Mwigulu anawakilisha kundi la wana-ccm wanaopenda siasa za kihuni-huni na unyama-unyama....
 
Believe me nikikuambia Mama Samia hatoongoza taifa zaidi ya mwaka lazima aapishwe mwanaume pale ikulu
Wewe sio mtoa roho za watu! Kwani ni lazima Makamu wa Raisi awe mwanaume! Mhe. Samia ana uwezo wa kumpendekeza Makamu wa Raisi mwanamke na kwangu huu utakuwa uamuzi sahihi sana. Nchi hii ina wanawake shupavu na wenye mawazo ya kitaifa zaidi kuliko vyama vyetu. Tuna akina:

1. Asha-Rose Migiro
2. Anna Makinda
3. Prof. Bernadeta Killian
4. Anna Mghwira

Hawa ni baadhi ya wanawake wazalendo wanaoweza kutumikia nafasi ya Makamu wa Raisi wa JMT.
 
Back
Top Bottom