Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Huyo Mama naskia anatishwa atapigiwa kura ya kutokuwa na imani nae wabunge wengi waliwekwa na Magufuli, she is scared.

Let's wait & see.
Wazee waling'amua kitu tokea 2015 na ndo maana akasema kwamba yeye alimuandaa Hussein Mwinyi.

Hivyo hata ukijitahidi uwahi kiti cha mbele tatizo ni CC ya CCM ambayo yumo pia mama Anna Makinda ambae kwenye mdahalo pale Dodoma mwezi jana na mzee Butiku na yule mzee mwingine (mtu mzito ndani ya BUT) walisisitiza kulinda mwelekeo wa 2015-2025.

Huo ni uchambuzi wangu tu hapa Tandamti Street.
 
Huyo Mama naskia anatishwa atapigiwa kura ya kutokuwa na imani nae wabunge wengi waliwekwa na Magufuli, she is scared.

Let's wait & see.

Struggle for power katika nyakati is tulizonazo is as real as Reality can be!

In events like these haya yanategemewa sana!, but fortunately most times, mambo huwa “fixed”

Let’s pray for Fortune!
 
Majina ya wahariri yapo wazi watafute waulize.

Kuna uhakiki kiasi gani wa hao wahariri wa hii habari kuwa wakweli na wenye uhakika ?!

Spoiler; we got threads here in JF which date as far back as 2017 , with speculations and prophesies of what to come in 2020 & 2021! Hizi tunazizungumziaje?!?
 
Hakuna cha NCHIMBI wala mavi yake..... JK + KARUME + SAMIA Ni kitu kimoja. Afu msisahau kuwa RAIS NDIO ANAPENDEKEZA JINA sio CC inapemdekeza. MAMA SAMIA ANAWEZA KUMTEUA STEVE NYERERE NA NGOMA IKAINUKA.
VP TAYARI ANAJULIKANA KUTOKA UPANDE WA JK NA KARUME
 
Na ndo maana Rostam amewezeshwa kufungua kiwanda cha ngozi Morogoro kwa kuleta wawekezaji.

He is the kingmaker.

Ila bado matokeo halisi yaweza kuwa tunapotezwa lengo.

Lakini Mafisadi hawana nafasi katika CCM mpya.
Hiyo nafasi hawana manake wakirudisha mafisadi 2025 CDM wanachukua nchi saa nne asubuhi
 
Chief, Bashe and Smartness don’t and will never rhyme!

Kuvaa barakoa jana, his smartness + Mzee alimpenda sana??!? Sijaelewa hapa!

Muda utasema

Tusisahau hizo pesa zilishindwa kumzuia Magufuli kuwa Rais 2015
Za mvi na za membe zote zilitumika na akapenya
 
Habari wana Jamvi,

Katika fikra na matamanio yangu ni kumwona huyu bwana Dk. Assad aliekuwa Mkaguzi Mkuu Wa Serikali kurudishwa ndani ya system. Huyu ukiachilia mbali elimu na uwezo aliokua nao, amedhihirusha sana kuwa anafaa kushika nyadhifa za juu katika serikali.

Miongoni mwa sifa ni;

1) Msomi wa hali ya juu na anaeitendea haki elimu yake ya Phd (Sio mtapia tumbo kama wateuliwa wengine wenye Phd zao).

2) Amedhihirisha kusimamia vizuri na kwa weledi mkubwa sana matumizi ya hela za wananchi ambazo serikali inatumia. Kufikia hatua alikua tayari kupoteza kazi yake kwa kusimamia msimamo wake na kukataa kutumia/kuamrishwa na mihimili ya nchi.

3) Amediriki kuikosoa serikali na bunge pindi lilipoji umauma juu ya matumizi ya Sh Trillion 1.2 na lilipotaka kuficha baadhi ya makosa ya matumizi ya pesa za umma.

4) Muadilifu, Mkweli na Muwazi.

5) Msimamizi mzuri wa hela za umma.

6) Hana maswala ya kuwa na team (Hayupo team CCM MPYA wala CCM KONGWE). Team hizi sasa hivi zinapambana kuona mtu wao anashikilia hicho kiti, na team itakayo shindwa basi itakufanyia hujuma kuelekea 2025 kuliko hujuma za vyama vya upinzani.

7) Hana makuu wala kujionesha (CAG alikua akiendesha Toyota IST).

8) Hana sifa ya kutumia cheo chake kukandamiza watu au kujipatia hela (Waliokua watendaji wake katika Ofisi Za CAG wanamjua na kusikitika kumpoteza).

9) Hana Kashfa wala figisu wala chuki (Hana visasi na utanijua mimi nani).

10) Anajua kazi zake kwa hali ya juu (Mafisadi ndani ya serikali watachemka matumbo na kuharisha huyu bwana akirudi serikalini, maana hakuna wakumdanganya kwenye swala la mahesabu na matumizi -Bunge nalo lijipange kwake huyu mtu, hawana cha kumdanganya).

11) Miradi alioacha Marehemu Magufuli ni mingi sana, bila msimamizi mzuri katika mahesabu na matumizi ya hela basi ufisadi utakithiri kupita kiasi.

12) Kuna tetesi za hela kuibiwa mara baada tu ya Rais kufariki dunia, kwa kigezo zimetumika katika ununuzi wa mashine za kumtibu Rais, huyu mtu atahakikisha UKWELI JUU YA HILI - Risiti za manunuzi au pesa zitawatokea katika tundu lolote wanaosadikiwa kuzichota hizo hela.

Tafakari ushauri huu, utani shukuru baadae moyoni mwako. Huyu mtu ni muhimu sana kwetu wananchi kama msimamizi wa hela zetu za kodi na atakua mshauri bora sana kwako.

Akikataa uteuzi, alazimishwe. Tuweke udini na ukabila pembeni na tuangalie taifa letu (2015 mpaka sasa ukabila ulitaka kushika kasi sana).

Wako mtiifu,
Alexander The Great
Naona sasa roho kwatu kwenu ,kwa maana hii orodha wote wangekuwa akina Patrick tungeanza kusikia kelele za oh wakristu wanajipendelea,na mlivyo na tabia za ajabu sasa hatutawasikia mkiuliza maswali yenu ya mbona hakuna Muislamu!
 
Safari hii watanzania msishangae mkaletewa kitu fulani hivi cha ajabu, hamkijui kabisa, mtajuliwa na kuaminishwa kuwa kiko poa na mtarejea kupiga makofi.

CCM ni mabingwa wa mazingaombwe.
 
Back
Top Bottom