Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Makamu atokee kati ya maveteran waliowahi kuwa katika Wajumbe wa Baraza la Mawaziri, Wajumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa, Sekretariat ya Baraza la Mawaziri, Sekretariat ya Baraza la Usalama wa Taifa.

Hii nafasi haitajiwi outsider. VP ni mtu ambaye kwa wadhifa wake atakuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri, Baraza la Usalama wa Taifa, Kamati Kuu ya Chama kinachotawala in this case CCM, Halmashauri Kuu ya Chama (CCM) na Consumer wa Taarifa za kiintelligensia.

Imagine akaletwa mtu ambaye ni mpya katika vikao vyote??
 
Na kwa sifa hapo juu, watakaofaa katika nafasi hiyo ni maveteran wafuatao;
1. Mizengo K.P. Pinda(Mzee wa Asali)
2. Abdulrahman Kinana(Comrade)
3. Othman Rashid(OR)
4. Francis Kipilimba, Kp
5. Davis Mwamnyange(Generali)
6. Fredrick Sumaye(Mr. Zero)
7. Anna Makinda(Mama Mwenda)
8. Ombeni Sefue(Balozi)
9. Philemon Luhanjo(PL, kama ana nguvu)
10. Andrew Chenge( nyoka wa makengeza, mzee wa vijisenti)
11. William Lukuvi
12. Mathias Chikawe
13. George Mkuchika
14. Kasimu Majaliwa.
Mpangilio ni random. Haina maana yoyote kiuzito na kimapendeleo.
 
Balozi Mahiga alifariki tar 1 May 2020, kesho yake tar 2 May Rais akamteua Nchemba kuziba hiyo nafasi (kabla hata ya mazishi).

Naamini huko Magufuli aliko, angependa tumuenzi kwa kuziba nafasi hizo haraka sana tena kabla ya mazishi.
Nasikia wanataka kumpa DR Slaa
 
VP atateuliwa kutoka JWTZ. Ni jina ambalo litawashangaza wengi maana hajulikani wala hajawahi kusikika popote na ndiyo makubaliano.
 
Wana JF

Sote humu tunaangaika kupata mtu sahihi wa kusaidiana na Rais SSH, huku tukitaka kitoona mabaki ya CCM ya zamani iliyokuwa Na malengo ya kujirundikia Mali huku ikilindana kiutawala na kufanya wanyonge tuwe maskini wa kutupwa kabla ya Rais Hayati JPM kuipangua na kuirudisha kwa wananchi. Vyeo vya kulindana na kurithishana vinaweza kurudi ikiwa hatutamchagua mwanamapinduzi wa kweli.

Dr. Charles Kimei amefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kibiashara ya kibenki mpaka akacha urithi mkubwa wa kimaendeleo benk aliyoiongoza ikapata mafanikio. Yeye akiwa mshauri wa mwenendo wa kiuchumi aliwahi kusahihisha makosa fulani tunayopitia akataka kuletewa zengwe kabla ya kuambiwa kanusha ili alinde ugali wake kwani alikuwa anakalibia kustaafu.

Kwa udhubutu wake kusema ukweli na makosa anayoyaona kiuchumi, na alighubikwa na serikali isiyotaka ukweli, sasa ni wakati wa CCM kumchagua akatuletee maendeleo kwani hana makundi. Sisi tunachotaka ni maendeleo dhabiti ya watu na vitu sio vitu tu huku wanyonge tukisaga Lami. Angalau tukimkosa Antoni Mataka naye anafaa, Mkoa wa Simiyu ulikuwa nyuma sana na ameunyoosha, ameonyesha diplomasia makini kwa kutatua migogoro ya wafanyakazi.
 
Na wachaga watajimilikisha nchi yote,kumbuka crdb ilivyojaa wachaga.
Ukabila ukabila ukabila.
Hii kitu ndio nyerere alikataa.
CRDB ina manos ambao si Wachaga. branch managers ambao di wachaga.. mpaka watumishi wa ngaz ya chini.
Kisa tu imeanzishwa na mchaga basi unadhani wote ni wachaga.
kwann tusiseme kampuni yote ya azam ni waarabu?
kwa nn tusiseme bakhresa kaajiri wazaramo tu?
 
Back
Top Bottom