Baada ya kimya kingi nami nitie neno DP World, Mtazamo wangu ni Tofauti kidogo

Baada ya kimya kingi nami nitie neno DP World, Mtazamo wangu ni Tofauti kidogo

Kwa ufupi ni kwamba DP World wamekuja kwa njia ya uani kuzuia Bagamoyo Port Project...

Na hii issue ipo Serikalini wanajua...
Alipofariki Magufuli hii project ilirudi mezani na walishaanza kurejesha mazungumzo na China na Oman kujenga Bandari kubwa sana ukanda huu wa Africa...

Kumbuka malighafi nyingi zinatoka Uarabuni na Asia kuja Africa...

Sasa Dubai anapanua Bandari yake iwe ya mfano... Kwahiyo malighafi nyingi za Uarabuni na Asia zitapitia Dubai kwanza kisha kusambazwa Africa...

Kwahiyo DP World wana ushirika mkubwa na US... Hawakutaka kamwe Bagamoyo Project Isimame...

Ndio maana utaona mkataba badala hata ya kuwa Dar Port alone... Wanasema bandari zoteeee.... Na ukitaka kujenga Port mpya Baharini omba Ruhusa Dubai... Kitu ambacho itakuwa ni ngumu sana...

Kiufupi tumeshasaini toka mwaka jana... Na kutoka huko kuna kazi ya ziada kama sio kulipa mabilioni ya dola katika mahakama za kimataifa
 
Habari za siku nyingi, nimekuwa kimya kidogo tokea sakata laBandari limeanza,

Uwekezaji ni mzuri sana na hasa unapofuata misingi sahihi, hasa kwa bandari zetu hizi zinataka mapinduzi makubwa sana kuto au kuondoa ukiritimba uliopo,

hivo siwezi kupingana na aliyeleta hoja ya kuwakaribisha wawekezaji, japo naweza pingana naye kwa namna sakata linavyopelekwa au lilivyobebwa,

A. KWANINI NAUNGA MKONO HOJA
Bandari yetu imekuwa ni ya hovyo sana kwa miaka mingi mno, kupotea kwa mali za wateja, kuchelewa kwa huduma, kutozwa tozo zisizo sahihi, kuharibu mali wakati wa utoaji,
kwenye suala la mwekezaji bandarini isiishie kwenye kuleta mikono ya kupakua mizigo au kuweka tehama tu, bali hata usimamizi wa mapato na mchakato mzima wa kumtoza mteja uwe wazi na makusanyo yaelekee sehemu husika,


B.MAPUNGUFU KATIKA MCHAKATO MZIMA
Natambua fika kwamba wenye bandari sisi ndo ilibidi tuande draft ya jinsi gani tunataka bandari iendeshwe alafu tumpe anayekuja kuwekeza, najua hilo litakuwa limefanyika ila kama yamefanyika basi zitakuwa zimepitiwa hatua hizi

Mwenye bandari sisi ndo ilibidi kuandaa proposal na tena kuna hatua.
1. Unaandaa hadidu za rejea yaani terms of reference (TOR).

2. Unaandaa tangazo ili wazabuni waombe kufuatana na vigezo vyako vya kwenye Hadidu za rejea yaani terms of reference (TOR)

3. Unatangaza tenda ili watoa huduma waombe kufuatana na vigezo vya kwenye Hadidu za rejea.

4. mnafungua tenda mbele ya wazabuni.

5. Mnachuja wazabuni kufuatana na vigezo.

6. Mkimpata anayewafaa mnamfahamisha kupitia offer letter.

7. Anajibu offer letter

8. Wewe mwenye zabuni ambaye ndiye unahitaji huduma unaandaa MKATABA. Unawapa draft Upande wa pili nao wanaupitia wakikubaliana mnasaini.

Nadhani huu utaratibu au unaofanana na huu ulifuatwa. Tunasubiri CAG akija kwenye ukaguzi asije kusema trillion kadhaa zilipotea kwa sababu ya kutofuata taratibu za MKATABA.

C.UDINI NA UKANDA
Ukiwasikiliza vijana wengi mtandaoni kwa sasa hawajibu hoja bali hisia zimejengeka tayari ndani yetu au yao kwamba wenda Wazanzibar wanauza Tanganyika, wakati huo huo Wazanzibar wanatetea hata kila lisilotetewa kisa watekelezaji wanatoka upande wao, hapa ningeshauri kwanza vijana wazichambue hoja zote za msingi, tuweke ukanda na udini pembeni ili sasa tuongee points, juzi kuna sheik mmoja nimemuona anamparua Prof Issa Shivji, kama mtoto mdogo bila kujua mzee shivji ni Miongoni mwa wanazuoni 7 waliopewa direct approach ikulu na kutoa maoni na katika maoni ambayo uwa yanazingatiwa sana ni ya Issa, anatokea mtu anajiita Sheik bila kujibu hoja anambagua kwa rangi yake, hilo suala halikuwa sahihi kabisa, Masheik na Ma Askofu Umakini katika kuyaongelea masuala ya msingi kama haya, hasa nisifiche MMEPWAYA

D. CCM INATUMIA WATU WA HOVYO KUFIKISHA UJUMBE
Chama changu pendwa cha CCM mmetumia watu wa hovyo sana kufikisha ujumbe au kuelimisha jamii nina mifano

--Hili suala la uwekezaji au ubinafsishaji kwenye bandari wapinzani wametupiga bao kwenye kutumia watu wajanja na wajuzi wa mambo kudadavua undani, na ndo maana kila mwananchi wa kawaida anadhani au anajua bandari imeuzwa tayari kwakuwa wamejadili masuala ya msingi, na hata wasio wapinzani wamejadili mambo ya msingi haswa
Mfano Mama Anna Tibaijuka alieleza kwa kina juu ya usalama wa anga (air space) kwamba mkataba kwa kipengele alichosoma kuna sehemu inasema kwamba bandarini pale sehemu kadhaa ft kadhaa kwenda juu hatutakuwa na mamlaka nayo, hili suala halijajibiwa zaidi ya kusema na kushambuliwa kwamba ESCROW ni ya Tibaijuka, mara anamtetea Karamagi wa TCTS, Je hoja yake imejibiwa?

lissu yeye kazungumzia suala la watakapokuwa na bandari kavu hatutaruhusuwa kujenga feeder roads, kashambuliwa kwa matusi je hii hoja imejibiwa?

mkataba hauna ukomo ni hoja ya kila mtu, mbona nayo haijibiwi?
Mgawanyo wa jinsi gani tutapata share haikuwekwa wazi, basi inabidi CCM watumie wataalamu kueleza kwamba uwenda itasemwa hapo baadae au kuna sababu kadha wa kadha kutosemwa,

Chakushangaza Watetezi wa CCM ni Steve Nyerere ambaye hata wasanii wenzake hawamkubali popote hata kwenye sekta ya usemeji walimkataa, ndo CCM inampa airtime kusemea mambo mazito,
Mtu kama Manara huyo ndo kaaribu kabisa kwa maelezo yake yamejaa na ubaguzi ndani yake kwamba watu wa mikoani hawaruhusiwi kuhoji bandari, are we serious?

CCM au Serikali ina watu wengi wa kuweza kueleza jambo likaeleweka Wapo kama Mzee Adam Simbeye wa this week in perspective na wazee wa namna hiyo wengi wasomi wanaoelewa masuala haya ya mikataba,

linapokuja suala la mambo ya Msingi ya Nchi Tafadhari akina Mwijaku sijui baba levo wakae kwenye miziki na media huko mambo ya msingi wataalamu wawaeleze wananchi kinaga ubaga, kuliko kuwatumia watu watakao watibua watu au kuwa mislead na serikali ikaeleweka visivyo kumbe si lengo la serikali waseme hivo,

USHAURI WANGU
1. Kama Tumekaa na TICTS miaka zaidi ya 20, aongezewe mwaka mmoja huku serikali na wadau waanze kuufanya mchakato upya kwa kutangaza magazet ya serikali na kwenye telvisheni ya Taifa kiwepo kipindi maalumu cha kuuelezea mkataba kwa kiswahili tu na kidadavuliwe na wataalamu, ifanyike hivyo kila week mara tatu kwa muda maalumu ndani ya week 52,

2. Mwekezaji naye aelezwe kwamba kuna ABCD tunataka wananchi waelezwe ili kuzuia baadae asije kuja raisi wa kariba ya wale wasifuata sheria kama fulan akaufutilia mbali ,

MWISHO TANZANIA NI ZAIDI YA CHADEMA,CCM,ZANZIBAR,TANGANYIKA,ACT,UISLAMU,UKRISTO AU UPAGANI,


Britanicca
Tangu nimekufahamu, leo umeandika kwa kutuliza akili,, Naona umeacha kunywa LUBISI,,!

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kuna kipengele muhimu sana cha DP world wanawekeza how much kwenye uwekezaji wao sababu ni
1.Tayari tumeshawekeza zaidi ya Tril 1.4 pale JPM alitoa,
2.Kama ni uwekezaji wa $400m ni pesa ambayo hata sisi kama Taifa tunaweza kuiweka kisha tukakodi kampuni ya kuendesha tu Bandari kwani tayari miaka miwili iliyopita tumeshaweka pesa zaidi ya iyo inayosemekana mwekezaji anakuja kuweka (kama sio kuendesha tu maana tayari tumeshaweka iyo ela pale )
 
Mi namlaumu huyu katibu mkuu wa CCM wa sasa, shida ni kiwango cha elimu au ni kwamba ni mzito kichwani. Hivi kweli Sofia Mjema ndiyo awe katibu mwenezi wa chama? Are they serious? Kilichaongaliwa ni jinsia au dini. Km wanaweka watu kwa kwasababu binafsi km hizo tegemea failure. Nauliza UV-CCM wako wapi, au kwasababu mwenyekiti mzanzibari. Huyu mama kajaza waislamu na wazanzibari kwenye chama ktkt uchaguzi wa 2022 akifikiri sijui amekuwa shehe badala ya mwenyekiti wa CCM Taifa. Mi sintashanga chama kikimfia mikononi, halafu inaonekana km ana kibri flani ya kutoshauriwa. CCM ninayoijua siyo hii, katibu mwenezi wa CCM na UV-CCM wasingelala wangekuwa wamesambaa nchi nzima na kwenye mitandao kutoa ufafanuzi wananchi waelewe, wako wapi, au wanafikiri wamepewa nafasi ya kula siyo ya kazi?
Kama na wao hawakubakiani na huu "Umangungo" jee!!??
 
Shida Moja kubwa ni kwamba kwa Nini huo mkataba unahusisha bandari zote za maziwa na bahari?
Pia mkataba hauoneshi ukomo wake kwa mantiki hiyo watu tunaona tushakaribisha koloni hivi.
 
Back
Top Bottom