#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

Ndugu Mayalla "njaa" kisukuma, kumbuka kuna Genge la aliyetangulia linamhujumu SSH.
huu mtandao bila kuvunja baraza la mawaziri haufi.
 
Hata kama wengi wanapinga chanjo ya uviko, lakini viongozi wote walitakiwa kuwa na lugha moja. Tatizo baadhi ya viongozi naopinga hii wanaogopeka sana kaka.
Angepatikana mmoja mwenye imani hata kama ni kidogo kama chembe ya haladali angeweza kulikemea hili.
 
Kaka Paskali, hili napinga na wewe kwa more than 100%
Labda naomba unijibu hili...WALIMAANISHA NINI WALIPOSEMA KUCHANJA NI HIARI?
Mkuu Ngalikihinja , hiari, ni consent, yaani lazima uridie wewe mwenyewe, mwisho wa uhuru wako ni pale ambapo hautaingilia uhuru wa mwingine, hivyo unapokataa kuchanjwa ni hiyari yako, lakini pia una wajibu wa kuwalinda wengine, hivyo usipochanjwa, wewe ndio utawaharisha wengine kwa kuwaambukiza, hivyo hata kama wewe hutaki chanjo, lakini kwa ajili ya wengine, hiyo chanjo inageuka wajibu.
Ndani ya chama CCM na ndani ya serikali, kuna kitu kinachoitwa uwajibikaji wa pamoja, a collective responsibility, mkiisha kubaliana jambo, then wote mnasimama pamoja, kama wewe hukubaliani nalo, unanyamaza, ukiamua kulipinga hadharani, unapaswa kwanza u fall out, then pinga!.

Rais wako na Mwenyekiti wa chama wako, awahimiza Watanzania tuchanje, halafu wewe ni mwanachama, kiongozi, unawaambia watu wasichanje!, hiyo ni insubordination na usaliti.
If you have your cake and you love it, you have only two options, if you love it so much and you desire to eat it, una mawili, ama control your desires usiile hiyo keki ubaki ukiiangalia tuu na itakuwepo, au tamaa ya kula keki imekuzidia, ukaila hiyo keki, then its gone!, you can't have both, you cant eat your cake and still have it.
P
 
Uliiona ile sirenji Pascal Mayalla . Kwamba alichanjwa ?!. Hila hizo. Mimi mwenyewe naunga chanjo lakini siungi zidumu fikra za mwenyekiti. Nyerere mwenyewe aliikataa hii kitu.
 
Mbona unazidi kujichanganya?

Je, ukichanjwa hauwezi kuambukiza?

Je, ukichanjwa hauwezi kuambukizwa?

Je, Ukichanjwa na tayari umeambukizwa utapona?

Je, Chanjo hiyo inaponyesha UVIKO-19?

Kwanini unavaa barakoa hata unapochanjwa?

Tuchambulie mahusiano ya chanjo ya UVIKO-19 na DNA, MRN na Nanotechnology kuhusu afya ya mnufaika wa chanjo inayoendelea


Unatumia nguvu nyingi mno ambazo sio za kisayansi kushawishi watu wakuunge mkono kuhusu chanjo; ndugu yangu HIARI YASHINDA UTUMWA usilazimishe. Nakushauri uanze kuhamasisha baada ya miezi sita au mwaka ndipo utapata wa kukuamini vinginevyo 'you are lost'
 
Hii ni kwa viongozi tu wa umma au Hadi watumish wa Serikali wa kawaida tusio na cheo
Public servants ni watu wote wanaolipwa by taxpayers money, ndani yao wapo watumishi wa serikali, wa wizara, wakala na idara zinazojitegemea, watumishi wa mashirika ya umma, na vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku.

Rais wa JMT ndio mtumishi no.1, akiishasema tuchanje, wewe mtumishi wa umma usiokubali chanjo, usichange ila jikalie tuu kimya, usianze kuhamasisha in public watu wakatae chanjo, hii ni insubordination, na kumsaliti bosi wako!.

Hata Jeshini, baada ya CinC kuchanja, huko ni amri, sio hiyari.

Uhiyari wa chanjo ni kwenye kupata tuu ridhaa, consent, kama ilivyo ndoa, ukiisha ridhia kuingia kwenye ndoa, huna mamlaka juu ya mwili wako kwenye kuihudumia ndoa, ukitaka huduma, lazima upewe, ule sasa unakuwa ni wajibu.

Kwa vile kutokuchanja, hakukuhatarishi wewe pekee bali wewe unayekataa kuchanja, unawahatarisha wengine, hivyo unawajibu wa kuwalinda wengine. Kama unavyowajibika kwenye ndoa, kuna siku mwanandoa mmoja hajisikii kuwajibika, yuko kwenye bad mood, au amechoka sana, lakini huduma inapohitajika hujikuta japo hataki lakini lazima ahudumu. Vivyo hivyo kwa wasiotaka chanjo, wana wajibu wa kuchanja ili kuwalinda wengine, hivyo ni hiyari yenye wajibu.

P
 
Mkuu,

Huko jeshini vyeo vya chini kunafukuta wakitumia amri ya kuchanja wote hoja zako ni nadharia inayokinzana na uhalisia.
 
Mkuu,
Kipengele hiki huna hoja ya mashiko na ushawisho wowote kwa sababu kama umechanjwa au hujachanjwa tishio ni lilelile tu halina upungufu au nyongeza ya kuzuia au kulinda kikamilifu afya ya mtu basi ni kujilisha upepo bure.
"....Kwa vile kutokuchanja, hakukuhatarishi wewe pekee bali wewe unayekataa kuchanja, unawahatarisha wengine, hivyo unawajibu wa kuwalinda wengine...."

Tumieni mbinu na njia zingine kushawishi na kuhamasisha lakini sio hii , 'You will never make it'.
 
Paschal,
Napenda watu wachanje lakini sipendi ulivyoifikisha hoja yako.

Unaposema kwamba ni usaliti unatufanya wote tunaopenda chanjo kama tuna akili za kibabe kama wana CCM maana ndiyo huwa wanatum maneno hayo wanapokosa ushawishi.

Sisi tuna utajiri mwingi wa facts kuhusu chanjo, kwanza hata hatukuhitaji Samia ajionyeshe hadharani.

Mimi nitachanja wiki ijayo.


 
Waliposema kuchanja inabaki kuwa HIARI ya mtu, walijua uhuru wangu unaishia wapi..!! Nasema walijua na ndiyo maana wakasema hakuna atakayelazimishwa..!!! Usaliti ni pale tunapokubaliana jambo, halafu mmoja anakwenda tofauti na mlichokubaliana.. Lakini kama tumekubaliana kwamba iwe hiari, how come mimi ninayefuata makubaliano ionekane ni msaliti??? WANGESEMA BASI KUCHANJA NI LAZIMA NA ATAKAYEKATAA KUCHANJWA HUYO NDO MSALITI

BADO HUJANIPA JIBU KWANINI WALISEMA KUCHANJA NI HIARI?
 
Tuliza kinyeo p ulijipendekeza kwa maccm ukakosa ubunge
Sasa unaleta majungu kumfitinisha mbunge na chama chake Ili afukuzwe

Unadhani hiyo nafsi yake utaipata!,?
 
Ameshirikishwa ugaidi wa sukuma gang
Wanogopa atawa blackmail
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…