#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

You are not a scientist ndiyo sababu unapima madhara ya chanjo kwa mwendo wa mwezi mmoja. Wewe subiri miaka kumi ndipo ujue mbivu na mbichi.
 
Vifo vipo vingi toka wakati wa JPM, sema kwako ndio ilikuwa haijafika.

Hivi hushangai kwa nini walitoa tamko la kuficha data kama wana nia njema. Bora wangekaa kimya kuliko kupiga marufuku data kwa nguvu kubwa na vitisho.
 
Vifo vipo vingi toka wakati wa JPM, sema kwako ndio ilikuwa haijafika.

Hivi hushangai kwa nini walitoa tamko la kuficha data kama wana nia njema. Bora wangekaa kimya kuliko kupiga marufuku data kwa nguvu kubwa na vitisho.

Inahitajika kukaa kwenye neutral point ili kujadili suala hili rationally.
 

Wasikamatwe waliotengeneza kirusi na chanjo zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia mpya ya kutotumia sehemu ya mdudu bali inaingia moja kwa moja kwenye chembe hai ya mwanadamu na bado ikaruka testing phase kucheki km ni salama kwa wanadamu akamatwe Gwajima anaehoji usalama wa chanjo kweli!... hapa utakuwa umejihoji vizuri mkuu?!
 
Vifo vipo vingi toka wakati wa JPM, sema kwako ndio ilikuwa haijafika.

Hivi hushangai kwa nini walitoa tamko la kuficha data kama wana nia njema. Bora wangekaa kimya kuliko kupiga marufuku data kwa nguvu kubwa na vitisho.

Wangetoa data ndio watu wasingekufa mkuu?!
 
Ni heri angeishia tu kwenye msimamo wake wa kuikataa chanjo. Lakini kusema viongozi wa serikali wamehongwa ili kuingiza chanjo, wamechanjwa kwa kufake, waliochanjwa watakufa in 2 years, yanaashiria serikali imeazimia kuangamiza raia wake.. Sidhani kama serikali inapaswa kunyamazia haya.
 
Inahitajika kukaa kwenye neutral point ili kujadili suala hili rationally.
No noo just use your common sense achana na " personality cults" kama JPM na utawala uliopita walikuwa wana nia njema wasingepiga marufuku data za covid na kutoa vitisho kwa atakaetoa data.

Na kuna " tetesi" kwamba hata waliokufa Covid madaktari waliambiwa waandike pneumonia.

Huenda walificha kwa nia njema kwamba baada ya muda covid ita evoporate kama kesi nyingine. Lakini covid haitoki haraka kiasi hicho. Jamaa walikuwa very short sighted sasa wana dhambi ya kuuwa watu wengi.

Ile chanjo ya Sputnick sawa ni controversial ingawa kwao wanachanja na Zanzibar wanachanja aina hiyo.

Warussi walitaka EU wainunue waitumie wakaenda Lab point to point na Warussia wakakosa kutoa majibu na data za walivyofanya research na analysis mpaka leo. You can check it even on google.
Lakini wa russia wanawalaumu EU kwa kuwa na Russophobia wakati wao wameshindwa kutoa maelezo na data.

Kwa hiyo Mkuu kuna umakini kwenye hii kitu. Ila ni hiari kwenye maamuzi, bahati mbaya nchi hii watu wasioenda shule wana influence kubwa kwenye masuala ya kitaifa na wasomi wanawashabikia.

Gwajima ana Degree za Juu za theolojia lakini yeye nchi hii ndio mtalaam wa 5G ,na COVID 19.

Utawala uliopita mbaya zaidi wakatuaminisha wtz ugonjwa umeisha. With no data na wasemaji wakila kitu wakiwa wao.

Uwe nuetral bro kwa ajili yako na family sio gwajima ndio awe source, data zake nyingi zipo kwenye open internet.
Akiitwa kwenye panel la watalaam wa biomedical sciences atakuwa hana la kusema kubwabwaja kanisani ni kitu kingine kwenda point by point kwenye sample na data na analysis na kitu kingine.

Imagine anazungumzia barcode na serial #. Conspiracy theories.
Kwamba kuna watu huko Europe wana ni track mimi nilechan kupitia ile barcode na serial number ya code kwenye kile kichupa cha sindano.

Yaani alitaka iwe blank. No barcode no serial number.

Mtu wa ajabu sana.
 
Wangetoa data ndio watu wasingekufa mkuu?!
Ndio tungejua ukweli waliposema ugonjwa umeisha sasa hivi wanaonekana wana dhambi ya kuua watu wengi kwa kutudanganya ugonjwa umeisha.
Na hapo hapo walituma ndege madagascar na Mhe alionekana ana bwia on camera ile dose kule kule, halafu yale ma box waliokuja nayo mpaka leo hatujui yaliishia wapi.

Ulikuwa utawala comedy haijawai tokea toka nchi hii iwe huru.
Kiongoxi akiwa mtalaam wa mambo yote ya Covid.
Na dawa haendi kuchukua waziri wa afya mabingwa wake bali " wanasiasa"
 
Kwa hiyo wewe ndio umetumwa kuja kupendekza aina ya mashitaka yanamstahili anayeenda kinyume na maamuzi ya viongozi wake hata kama yana walakini?

Kwamba aliyekosoa au kukaidi kutii anastahili kuwajibishwa kwa makosa haya?

1. Defiance to comply with a collective responsibility clause

2. Insubordination

Definition: An employee's intentional refusal to obey an employer's lawful and reasonable orders. Such a refusal would undermine a supervisor's level of respect and ability to manage and, therefore, is often a reason for disciplinary action, up to and including termination.

*Did her excellence order the parliament members or normal citizens to be compulsorily vaccinated and in default, one would be held accountable?

*Is the committee recommended that the vaccination was compulsory or voluntary?

*Was the MPs mentioned as one of the special groups prioritized for vaccination?

*Have you decided to wage a personal war against those challenging the authenticity and side effects of the COVID-19 hypo-vaccine?

Kwanini hujanukuu kipenegele kinachosema mtumishi ana haki ya kukataa kutii malekezo ya kiongozi wake ambayo ni kinyume na sheria na yana athari ya kiafya, kiusalama, kuichumi na kijamii?
 
Tatizo sio hilo
Tatizo ni kiongozi kuwa na kauli mbili kwa kipindi kimoja chenye awamu tofauti.
1. Fikiria kuwa mtu ni prof tena yuko kwenye kada yake halafu anakuambia hizi CHANJO SI ZA KUAMINI.
Sababu anasema hazijafanyiwa UTAFITI. Then awamu ya kesho anakuambia CHANJO ni SALAMA. Je aliyetengeneza tatizo ni nani?

2. Tatizo niutoaji wa ELIMU SAHIHI kwa WAKATI SAHIHI
Wengi wa raia wetu wako kijijini na hawana uelewa na mambo ya Utaalamu, tume ilipoundwa na kuthibitisha baada sio tu kuripoti kwa mteuzi wangeweka mkakati wa kuelimisha jamii na kujibu maswali ambayo yapo. Huwezi kuwalazimisha watu kwa MATAMKO pasipo elimu na kujibu HOJA zao.

USALITI itatokana na tofasri ya yule anaitumia,. Mfano wanaamini CHANJO ina manufaa wataita msaliti yule anapinga, lkn wale wanaamini BIASHARA ya watengenezaji wataamini ni Usaliti kutumia rasilimali za taifa au kupokea mgawo ili ziuzike kwako.
Ukimsaliti kiongozi kwa kutokubaliana na UOVU anaotenda sijui kama ni kosa kisheria.

Hadi sasa hakuna anayethibitisha kisayandi madhara ya muda mfupi na mrefu ya chanjo aganist Mazuri yake.

Kila anayesimama kutetea au kupinga aje na uthibitisho kwa kile anasema.
Ova
 
Hakuna kitu unajua bw mdogo.
Acha kubwabwaja. Kama hataki angekaa kimya akatae yeye na familia yake. Kupinga au kutangaza mawazo tofauti hadharani au kanisani au kuhutuba watu chini ya mtu ni mti ndio insubordination kabla ya kujibiwa au nini ajiuzuli tu aachie ubunge.

Mtu aliyepishana na mamlaka wakati nadhani wewe Duniani ulikuwa haupo ni Edwin Mtei Gavana wa Benki kuu Tanzania aliyemvimbia Nyerere kwamba masharti ya IMF anakosea msimamo wake.

Nyerere alipokataa ushauri Mtei kaandika barua ya kujiuzulu.

Gwajiboy anatishia kujiuzulu na bla bla kibao, wakati yupo tofauti halafu anauma na kupuliza. Na anakunja mil11 kila mwezi.
 
Tumeshatoka dhama za zidumu fikra za mwenyekiti, mwili ni wangu kwanini mtu mwingine aniamulie juu ya mwili wangu. Ukiona chanjo ni muhimu kwako kachanje ila usimlazimishe mwingine akubaliane na wewe hizo habari za kulazimisha ni udikteta. Wakati wa kipindi cha urais wa marehemu Magufuli hakuruhusu chanjo lakini kuna watu walichanja wala hatukusikia hizi kauli za waliochanja wamekiuka agizo la kiongozi hayo mengine ni unafiki wa kujipendekeza badala ya kukaa na kufanya maamuzi yako.
 
Huyu Gwajizo anapotosha umma na kuhadaa napenda awe na ushahidi na tafiti aliyofanya sio kuhadaa watu hovyo. Mtu mwenyewe hana credibility ya mambo anayo fanya na kusimamia alichokisema, so anatafta kiki
 
Huyu Gwajizo anapotosha umma na kuhadaa napenda awe na ushahidi na tafiti aliyofanya sio kuhadaa watu hovyo. Mtu mwenyewe hana credibility ya mambo anayo fanya na kusimamia alichokisema, so anatafta kiki

Ushahidi!

Mbona aliyesema katesti mitambo hamjaomba ushahidi?

Double standards.[emoji1614][emoji276]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…