Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Na kuna wanaume wanaowapata wanawake ambao hawana tabia hata moja hapo halafu wao ndio wanazingua.

Maisha hayana usawa!
Kweli kabisa! Nina shemeji yangu aliukwaa mkenge akapata janaume la hovyo hovyo sijawahi kuona! Binti moja maridadi sana na ana cheo chake benki yaani sisi wanaume!!
 
Huko alikoenda watoto wa mbwa watamgonga wamle hadi mifupa na akirudi kwako amechoka. Usijaribu kufanya hili sio jambo zuri. Kama unamuacha muache moja kwa moja asirudi.
 
Kuchukua hela ya mwenzio owe mzazi, mume , mke bila kumuambia ni wizi . Hakuna sababu ya msingi eti ohh humpi hela. Mimi hata uache sh. ngapi, kama kuna matumizi ya lazima nitakuambia hata kabla sijachukua. Unawezaji kusachi mfuko wa mwenza wako na kuchukua hela bila taarifa?
 
Huyo mke itakuwa ulimpaa mimba ndo ukalazimishwa kuoa mkuu
Umeamua kuongeza idadi ya single mothers bila aibu?
 
Ni kuvumilia mkuu. Mimi tangu jana nina homa kali, asubuhi nimeamka nipo hovyo nikaomba wife anitengenezee tangawizi aise akaanza kurap huoni nafanya usafi! Yaani nyumba hii Kila kitu Mimi! Mtoto akaomba maji akaambiwa Kwa kufoka kanywe bombani!

Unajua usipokua mvumilivu ni unavunja mtoto wa watu.

Nikainuka nimempa mtoto maji nikajitengenezea tangawizi yangu, jioni hii yupo kawaida anaongea vizuri
 
Tena sio tabia nzuri!!
Kwanini usimwambie naomba? Mwanaume km hataki kufanya majukumu yake na fedha anayo ni kumshtaki ebooh!!
Na kingine wanawake na sisi tufanye hata biashara ndogo ndogo, tuepuke kero na unyanyasaji wa wanaume wapumbavu.
 
Iwe jumla hiyo mkuu. Ndoa ni utapeli mkubwa ona sasa ulivyokuwa unatapeliwa mda mchache tu wa kuwa single umekuwa na amani. NDOA NI UTAPELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…