Manjagata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 13,942
- 15,371
Chukua hatua na wewe!Nayaonea wivu hayo mapumziko yako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chukua hatua na wewe!Nayaonea wivu hayo mapumziko yako.
Mpaka unafika mahali unajisemea kumbe nina nafuu!Kumbe kila mtu anachangamoto zake katika ndoa!
Kweli kabisa! Nina shemeji yangu aliukwaa mkenge akapata janaume la hovyo hovyo sijawahi kuona! Binti moja maridadi sana na ana cheo chake benki yaani sisi wanaume!!Na kuna wanaume wanaowapata wanawake ambao hawana tabia hata moja hapo halafu wao ndio wanazingua.
Maisha hayana usawa!
Kabisa.Kuna member aliniambia kuwa ndoa ni biashara,biashara yenyewe ndiyo hii[emoji23]
Huko alikoenda watoto wa mbwa watamgonga wamle hadi mifupa na akirudi kwako amechoka. Usijaribu kufanya hili sio jambo zuri. Kama unamuacha muache moja kwa moja asirudi.Umuofia kwenu!!
Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;
1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha Star TV kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.
"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."
"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah
2. Nimepumzika kushuhudia mabega na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi.
3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo.
4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda.
5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku.
6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka, hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.
Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli? Arudi ili nije kupata stress tena?
Ndoa..........mh!
Kuchukua hela ya mwenzio owe mzazi, mume , mke bila kumuambia ni wizi . Hakuna sababu ya msingi eti ohh humpi hela. Mimi hata uache sh. ngapi, kama kuna matumizi ya lazima nitakuambia hata kabla sijachukua. Unawezaji kusachi mfuko wa mwenza wako na kuchukua hela bila taarifa?Katika vitu nimejiandaa kuingia navyo kwenye mahusiano ni kumiliki uchumi wangu binafsi wa kifedha.
Nitazinguana na mwenzi wangu kwa issue nyingine sio za kifedha, Inshort mwenyewe najimudu. Hizo zake ni km za ziada.
Mwanamke anayesachi pesa kwenye suruali ya mumewe namshauri atoke maghetoni.
Hahahahhaha vya masimango[emoji23]Kabisa.
Tena ni biashara yenye faida kwa mwanamke.
Umeona alivyokuwa anapita na vichenji vya mshikaji?
Na mimi nilipata gumegume hatari. Nikasepa zangu . Nilienda kuomba talaka. Yuko anabwelanwela saizi.Kweli kabisa! Nina shemeji yangu aliukwaa mkenge akapata janaume la hovyo hovyo sijawahi kuona! Binti moja maridadi sana na ana cheo chake benki yaani sisi wanaume!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Usione watu wanashabikoa ccm kumbe deepdown wana mateso yasiyokoma[emoji23]
Likizo ukaliwe na ex?Muwe mnatupa likizo kama huyo mwenzenu alivyofanya jamani. Ni muhimu sana
Sasa mtu wa kukaa ananunanuna,hilo zoezi lenyewe litakuwepo kweli? Na huenda baada ya kuona hivyo,jama ameamua tu ajue yuko mwenyewe.Utajisajili chaputa na kuchukua Sheria mkononi kwa muda.....
Si mda wa kukaa na kamati kumtafakali kama anasameheka au la? Kiburi kwanza akapeleke kwa Ex huyo. Badae,hakuna kurudi. Kaa huko huko nikiwa na shida na wewe ntakuijiaLikizo ukaliwe na ex?
Tena sio tabia nzuri!!Kuchukua hela ya mwenzio owe mzazi, mume , mke bila kumuambia ni wizi . Hakuna sababu ya msingi eti ohh humpi hela. Mimi hata uache sh. ngapi, kama kuna matumizi ya lazima nitakuambia hata kabla sijachukua. Unawezaji kusachi mfuko wa mwenza wako na kuchukua hela bila taarifa?
Dukturi huchezi mbali[emoji23]Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka, hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Tabia zilizojificha: Chanzo cha migogoro kwenye mahusiano Tabia zilizojificha: Chanzo cha migogoro kwenye mahusiano
Sent using Jamii Forums mobile app
Kusikia kwa kenge.…. 😂Kipindi cha uchumba ulidharau baadhi ya vijitabia vyake, Madhara ndo hayo