Baada ya kuona mke wake corporate feminist lady kakomea watoto wawili, katafuta mchepuko form 4 kafyatua watoto wanne, ni sawa ?

HIVYO NDIO INATAKIWA mke akijifanya anaishia kuzaa watoto 2 au 3 basi tafuta mwanamke mwingine zaa nae watoto wasio pungua 3 au 5
Ni upungufu wa akili na ni upumbavu mwanaume unakufa una watoto chini ya 4 au 5
 
Kuzaa watoto wengi naweza kuelewa miaka ya baba zetu huko nyuma, lakini kwa miaka hii ni dalili ya kukosa elimu na kuishi kijima.

Angalia nchi zote zilizoendelea zenye watu walio na elimu halafu angalia idadi ya watoto. Utaona watoto wachache.

Halafu angalia nchi ambazo hazijaendelea zenye watu wajinga wengi, utaona idadi kubwa ya watoto.

Baada ya kuangalia hizi namba kama hujaelewa bado kuwa kuzaa watoto wengi ni alama ya umasikini na ujinga utakuwa na matatizo.
 
Mazingira tofauti, huku mtoto muda wowote anakufa kwa bodaboda, uzembe wa dereva wa school bus, dada wa kaz na madokta uchwara, maradhi n.k

Watoto weng n tahadhari
 
Elon Musk ana watoto wengi na ni tajiri no 1 duniani
Leta hoja nyingine

Mimi nina watoto watano na ndo kwanza wawili wako English medium schools (4.5 mil per year) na bado naishi good life huku michongo yangu ikichanua zaidi.Unadhani mimi ni maskini kisa watoto?
Ninyi ndiyo mnaoamini ili uoe kwanza uwe na pesa nyingi unasahau ukichagua mke mwema kupata kipato cha juu ni uhakika karibia 80% labda uwe mjinga mwenyewe.
Hao wazungu unaowasemea wanapingana sasa juu ya uzao maana nguvukazi imepungua kwao na matokeo yake wanakimbizana Africa kusaka wafanyakazi.Hope umenielewa vema
 
Nyie natalists wa KiAfrica hamna akili. Trump amechaguliwa sababu mojawapo kubwa ikiwa ni afukuze manamba wahamiaji wa nchi za ulimwengu wa tatu za Africa, Ulaya yote vyama visivyotaka manamba kutoka Africa ndivyo vinazidi kuongezeka umaarafu na kushinda uchaguzi.

Elon Musk anapenda manamba wa bei rahisi hasa kutoka India hadi anakorofishana na MAGA wenzake, hapo bado hatajongelea AI zao hao wakina Elon zitakavyoondoa kazi nyingi hasa za vibarua manamba.

Hii Africa yenyewe manamba na wachuuzi wahamiaji hadi kutoka Tanzania, na Nigeria wanafukuzwa Africa Kusini na wenyeji, hawataki kujaziwa nzi na watu wanaozaa kama Sungura. Tanzania mamilioni ya vijana wamejaa wanazitumia hizo nguvu kazi zao kuendesha boda, kuchuuza maji, pipi na maandazi stendi, wengine wanazurura bar wakiuza suruali moja ya mtuma, mbegu za maboga, protector za simu wakiwa na sura za kizee tayari.
 
Una maelezo meeengiii!Yuko wapi huyo mzee baba apewe tuzo?
 
Kwa hiyo Sisi tufanyeje? Unatushirikisha ujinga! Mwache na maisha yake!
 
Inawezekana Tanzania na sehemu kubwa ya Africa inahitaji viongozi wa mkono wa chuma kama wale wa China waliopanga na kutekeleza "One Child Policy" China maana ujinga wa aina hii wa Watanzania wengi ni wazi tunaenda kuwa Nigeria, Pakistani au Bangladesh nyingine miaka michache ijayo.
 
Kuna drama za wake wa nyumbani kuachwa halafu kuna scenarion nyingine kabisa za corporate feminist lady kuachwa, elimu ipo, wanaijua sheria, wana connections, wana power... ni jambo jengine kabisa
Ushamuogopa mkeo?
 
zaeni mkaujaze ulimwenguπŸ’
 
Fresh tu cha mhim anahudumia
Km mke aligoma ye afanyaje
 
Watoto 6 kwani anaishi kwenye ujima bado?
Kuzaa watoto wengi au wachache sio suala la usasa au ujima kinacho zingatiwa ni kuzaa idadi ya watoto ambao utaweza kuwatimizia mahitaji yao basi.
Kama mtu una uwezo ww zaa hata mia nne ila hakikisha unaweza kuwatunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…