Baada ya kuona nimepata mirathi kawa mpole sana

Baada ya kuona nimepata mirathi kawa mpole sana

Usimpe hata sh 10 mshenzi huyo! Halafu Hio hela ukiitumia vibaya itaisha bila kuelewa uliifanyia nini cha maana. Be careful kwenye matumizi !
 
Et siku hizi naandikiwa sms mchana mamy umekula..yan nacheka mpaka nakojoa
Hapo kwenye kucheka hatuna shida napo ... Ila hapo unapokojoa ndo umetuacha njiani ...ni mkojo gan wakawaida au ulee...........[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hela za mirathi sijui ni kwanini huwa zinapukutikaga mapema sana..unakuja kushtuka umebakiwa na laki tatu benki toka Milioni 18[emoji28]
 
Et siku hizi naandikiwa sms mchana mamy umekula..yan nacheka mpaka nakojoa
Sasa nawewe km umemgundua hana mapenzi nawewe, nawe pia huna mapenzi naye, na amevutika na pesa tu mchane faster ili ajikatae, usimfuge fuge mwishoni akikuona unakuwa mgumu zaid anaweza kukuua au kukutengenezea mtego wowote achukue hela hiyo
 
Sister nakushauri nunua bond za serikali hautojuta ,fixed account unapewa riba ndogo sana yaani Sana. Mfano nishawahi taka kuweka 35M nikaambiwa for 3 months nitapata 135k nikaona ni ujinga. Mana riba zake kwa mwaka ni 3-5% kwa mwaka. So piga hesabu. Ila bond za serikali unapata riba from 12-17 kutegemeana kuwa unaikopesha serikali muda gani. Kumbuka huwa ni kuanzia miaka mitano ndipo unapopata riba nzuri ingawa Kuna bills and notes za miezi ama under one year.
Ila Kama hautolkuwa na shida hela iyo. Utalipwa riba yako semi annually or quarterly.

Kama ukiona vipi Kuna jamaa akatoa ushauri mzuri Sana kuwa nunua ardhi Ila usiwe na haraka.
Mana ardhi huwa hakuna inflation Kama hizo bonds or fixed account.ardhi inaweza ikakupa maisha. Mana ikitokea Boss mmoja amependa eneo lako unatangaziwa day la maana unashawishika unaiuza.yaani ulinunua 3-5M ukauza even above 100M. Mana inategemeana na potentiality ya eneo husika.
Ardhi ni Mambo yote Mana kila siku Kuna watu wanaongezeka kuhitaji ardhi ya kujenga kumbuka saivi vijana walio chini ya 20yrs hao after 10yrs wote wenye from 15+ watahitaji kuwa na malazi so laizma land value iongezeke
 
Pesa huisha..
Saa hvi ulivo na hasira na huyo Mwanaume utampata mwingine pasua kichwa Zaid ya huyo na atakua anakusindikiza bank.
 
Tafuta sehemu nzuri nunua viwanja vyako kama vi 3, kutokana na sehemu hiyo.hakikisha havina mgogoro, hakikisha una hati. Piga kimya. Kama kuna kitu cha kuchangia ndani ya familia kisichozidi mil 2 changia.

Usipofata ushauri wangu utalia kwa uchungu hapo baadae. Eti kisa anajua sasa hivi una pesa ndo mapenzi moto moto? Huyo anataka pesa hakuna cha mapenzi.

N.b aridhi ndo kitu pekee chenye thamani ambacho hakihitaji usimamizi wa mara kwa mara.
Huwajui wanaume anaweza kukudanganya ukampa hesa na akazila na mwanamke mwingine.
Unatusingizia bure tu mkuuu
 
Miezi kadhaa nyuma niliondokewa na baba mzazi,,, tukaanza process za mirathi, wiki iliyopita tumepata kama mil 18 kila mtu.

Sasa huyu shemeji yenu simuelewi hapo nyuma alibadilika akawa haeleweki tangu mirathi imetoka kawa mpole mapenzi motomoto simuelewi kaamua kujirekebisha au nii hii mirathi anaiwinda.

Hapa nimetulia pesa nimeweka bank sijajua naifanyia nini.
Shemeji yetu amekuoa?
 
Miezi kadhaa nyuma niliondokewa na baba mzazi,,, tukaanza process za mirathi, wiki iliyopita tumepata kama mil 18 kila mtu.

Sasa huyu shemeji yenu simuelewi hapo nyuma alibadilika akawa haeleweki tangu mirathi imetoka kawa mpole mapenzi motomoto simuelewi kaamua kujirekebisha au nii hii mirathi anaiwinda.

Hapa nimetulia pesa nimeweka bank sijajua naifanyia nini.

Atakua amejirekebisha.
 
Back
Top Bottom