Baada ya kustaafu katelekezwa na mke na watoto wake. Anaugua ugonjwa wa akili kwa sasa

Baada ya kustaafu katelekezwa na mke na watoto wake. Anaugua ugonjwa wa akili kwa sasa

Sasa utaamua.

Ujiwekee akiba binafsi.

Au, u expose kila kitu kwa ndugu wajue hadi namba za siri za benki.

Kisha mkisha filisiwa mje hapa JF kulia lia tena na kuomba msaada wa mawazo.
Siwezi kuishi kijasusi kama wataamua kunisaliti Bwana Yesu atukuwa mwokozi wangu
 
Mkuu,

Kama mwanaume unatakiwa kuwa na Akaunti yako ya Siri ya benki ambayo unaweka fedha za emergency kwa maisha yako wewe mwenyewe tu.

Hii inakuwa ni special for you.

Hata wife, watoto, wazazi wako wasifahamu.

Yani kiasi kwamba hata ikatokea mka achana, kwenye mgao wa mali Akaunti yako hii isifamike na yeyote yule.

Maana siku zote watoto watakuwa upande wa Mama kumsapoti.

Mwanaume lazima uwe na fungu lako la kujisapoti mwenyewe wakati wowote ule wa dharura.
Sasa Mkuu kwenye Ule Mgawanyo wa Mali huwa wanangalia kile ulicho nacho Yani unamiliki Nini Sasa hapo utakuaje na account ya Siri Alfu isijulikane, hata kama Mke wako asipojua lakin Mahakama itajua tu mwishoe unakwapuliwa zote unabaki patupu.

Inshort haya Mambo yanahitaji Neema tu
 
Nashindwa sometimes kuelewa nini faida na umuhimu wa ndoa kama mambo yenyewe huwaga hivi.

Kuna mzee mmoja alikua jirani yangu, alikua mhandisi wa shirika moja kubwa hapa nchini

Mzee huyu kutoka kule migombani alioa mke wa migombani pia. Maisha yalikua mazuri wakati mzee bado anafanya kazi.

Alijenga nyumba mikoa mbalimbali na alijitahidi kuwasomesha watoto wake shule nzuri hizi za saint saint.

Watoto wake wote wana shughuli zao nzuri tu.

Baada ya kustaafu hapo ndo akaanza kuona rangi halisi ya mke wake. Kwanza alimtumia wakora wamfanye kitu mbaya ili mke arithi mali mapema bahati nzuri ndugu wa mume wakashtukia mapema mission ikabuma.

Tangu wakati huo mke akaanza kumtenga mume wake na kibaya zaidi hadi watoto wake aliowasomesha wakamtenga baba yao na kumsahau kabisa(sijui mama yao aliwaambia nini)

Dingi akaanza kunyimwa chakula, dingi akakimbiwa chumba na mke wake(alikua anatuambia vijana na kutuhasa juu ya makabila ya kuoa)

Baada ya muda mzee kaanza kurukwa na akili kwa maisha aliyokua anaishi.

Kwa sasa mzee karudi kwao lakini akili yake haiko sawa kaacha mali zote anaishi kijijini kwao. Watoto wake wamemtupa hawana time na baba yao

Je nini hasa wamama wanawaambia watoto wao kiasi cha watoto kuanza kumchukia baba yao na kumtenga ili hali aliwasomesha na kuwalea vizuri na juhudi zake waliziona.?

Hili ni janga kwenye familia nyingi baba akistaafu anaishi maisha magumu ya kunyanyasika juhudi zake zote alizofanya kujenga familia bora zinakua kazi bure anaishia kutengwa na kupata msongo wa mawazo na mwisho kufa.

KATAA NDOA NI UUAJI NA UTAPELI
Lengo lako lilikua kataa ndoa na si kingine... Acha kuzusha vitu vya uongo ili kuhalalisha huo ujinga wako
 
Aeleze vizuri PENSHENI KAPELEKA WAPI????
haiwezekani ustaafu tu kisha uanze kunyanyaswa haiwezekani!
Tunashuhudia mitaani wastaafu wakisha lamba mshiko tu wanahama nyumbani wanatafuta wananwake wa kula jasho la uzeeni .
WAKIISHIWA NDO HUKUMBUKA KAMA WANA MKE NA WATOTO NA WALIKUWA NA VIBANDA
 
Kuna mambo hayapo wazi kwenye hii story.
Ni lazima mzee kuna kitu alizingua,. Tuseme hajazingua kitu mtu una pesa na mali urukwe na akili kisa mke? Si umtimue watoto wake wamfate huko?

NIni hasa kinampa stress?

Hakuna mtoto ambae alikupenda tangu utoto wake aje kukubadilikia ukubwani bila sababu.

Kuna mambo ya ndani kabisa ambayo hayapo wazi hapa.
Shida inaanzia mtu akipata pesa familia inakua ni option kwake, zikiisha ndio anaikumbuka tena muda huo familia nayo inamfanya option....halafu walimwengu yanawatoka sasa kama hivi
 
Aeleze vizuri PENSHENI KAPELEKA WAPI????
haiwezekani ustaafu tu kisha uanze kunyanyaswa haiwezekani!
Tunashuhudia mitaani wastaafu wakisha lamba mshiko tu wanahama nyumbani wanatafuta wananwake wa kula jasho la uzeeni .
WAKIISHIWA NDO HUKUMBUKA KAMA WANA MKE NA WATOTO NA WALIKUWA NA VIBANDA
Thread ifungwe sasa turudi kwenye kimasihara 🤣🤣
 
Shida inaanzia mtu akipata pesa familia inakua ni option kwake, zikiisha ndio anaikumbuka tena muda huo familia nayo inamfanya option....halafu walimwengu yanawatoka sasa kama hivi
Na wanaona wakishatoa chakula na kusomesha watoto shule nzuri wamemaliza kila kitu. Ukute alikuwa hamtreat mke wake vzr anamchukulia poa. Kuna mambo yanajeruhi mioyo.

Waliosema fainali uzeeni hawakukosea.
 
Ukiona na kuamini mambo yanayozungumzwa Jf utaonekana tofauti sana mtaani na watu watakushangaa sana, sidhani kama utawahudumia wanao vyema kwa miaka na miaka halafu ukose hata mmoja tu wa kukushika mkono penye changamoto, labda unawazungumzia irresponsible fathers ambao hata humu tupo nao wengi,

Unakuta limtu limezaa zaa watoto huku na kule lakini halijui wanavaa nini, wanakula nini, wanachangamoto zipi,
Uzee ukishaliingia na limeishiwa nguvu linaanza kukumbuka kuwa mwaka fulani liliwahi nunua shati kwa mtoto eti hapo sasa ndo lilitoa huduma,

Ukiwekeza vyema kwa watoto wako Mungu ni mwaminifu hawezi kuacha jasho lako lipotee bure, hakuna mwanamke ukaishi nae vizuri akakugeuka, big no, acheni kupaka tope mama zetu kwa kisa kimoja cha mwanaume mpumbavu.

Mwisho kila mtu ajitafakari leo hii sa hii anaposoma hii comment, je anasimama kama baba kwa mtoto wake? Kama jibu ni hapana basi tegemea kuvuna ulichopanda.

Nawatetea wanawake, pamoja na mapungufu yao ila wanapitia changamoto nyingi sana.

Hapo mtaani kwenu kuna mamtu malevi,manyanyasaji ya wanawake tena mbele ya watoto.
Lingine pesa yake
 
All women are devils only your mother might be good to you, But she is still a devil to your father.

Mzee mmoja aliniambia kijana hata "Mama" awe mbaya na muovu kiasi gani na Baba awe mzuri kiasi gani, Siku zote watoto watakuwa upande wa Mama kumtetea maovu yake.

As a Man, lazima uwe na "back up plan" ya ku survive individually wakati wowote ule.
Hii Mimi nilikuwa tofauti
Ndio maana mzee wangu alinielewa
Mama akawa ananiona kama kijipu uchungu.
Ila wako very trick usipokuwa na misingi
Utamuacha mzee wako
 
wanawake ni sumu kubwa katika maisha ya mwanaume,wanawalisha sumu watoto ingali wadogo, mzee aliyumba sasa ivi ukiwa na mkwanja mrefu .una jenga nyumba za kupangisha kama 50 baada ya hapo unatafuta mwanamke mwenye akili wa kuzaa naye ila sio wa kuoa full stop .hizo nyumba 50 zitakusaidia mpaka unaenda chini ,kwa kuwa mawe yatakuwepo utakuwa unagonga videmu kama kawa .watoto utawapa haki zao kila kitu.kuoa ni ufara afu ni uoga wa maisha kwanini upate ukichaa wa kujitakia? kataa ndoa ila zalisha masingo maza wawe wengi ili tupate utelezi wa bure
Mawazo ya kijana masikini. Juzi tumemzika jamaa alikuwa na akili kama zako. Hakuwa na familia, alikufa n hkuna aliyejua hdi pale harufu ilipoanza kutoka ndani. Mazishi huwa saa 8 hadi 10 jioni kwa kawaida, ila jamaa amezikwa saa 5 kasoro. Bajeti ya msiba huwa kuanzia milioni 2 na kuendelea, ia jamaa bajeti ya msiba ilikuwa th 200,000 n watu waklewa. Amezikwa kama vile hkuwahi kuw na ndugu. Inasikitisha
 
Hii thread imenigusa sana. Kuna siku maza alinikalisha chini nakuanza kuniambia namna mshua alivyokua anazingua. Namna alivyokua mtu wa starehe sana kipindi cha ujana wake (hapo kabla sijazaliwa, maana nimezaliwa mdingi ameshavuka 40s huko).

Alifika mbali na kuniambia ninapopata chochote nisiwe namzingatia sana. Maana japokua baba ni mzee anaendekeza matumizi ya hovyo hasa kutuma tuma ela kwa ndugu zake.

Dah! Nilikaa chini nikaanza kufikiria. Yani nisimzingatie baba wakati alijinyima sana hata hakujenga nyumba nzuri kwa ajili ya kupambania elimu zetu watoto wake. Alipambana tukasoma shule nzuri na alikua mstari wa mbele kutukalipia pale tulipokua tunazingua kimasomo (mara nyingi kauli zake zilikua zinalenga tujipambanie tutoke kielimu ndio urithi pekee).

Mzee alijinyima sana hata hakua anapendeza na kuvaa nguo za fashion wakati ule anatusomesha. Nyakati za kulipa ada tulikua tunaona kabisa anavyochanganyikiwa kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa tunaenda shule. Na sasa umri umeenda sana, ameshastaafu, kutwa kulalamika maumivu ya kiuno, mgongo na macho kwa kazi ngumu alizokua anafanya wakati ule.

Eti ndio nimfungie vioo kisa mama kasema alikua anazingua ujanani! Hapana kwa kweli! Chochote nachokua nacho hua nahakikisha wananufaika wote bila kuwabagua. Hua najitahidi kua mfariji wa mzee wangu na anapokutwa na changamoto hua naitatua haraka sana.

Bado sijajua kwanini kina mama wengi wanakuaga wabinafsi sana na kupenda kuwalisha sumu watoto wawachukie baba zao. Inafikirisha sana.
 
Kuna Makabila Wana Laana ya Tamaa Inabidi Tuwahusie Watoto wa Watoto wetu wasijalibu Kuoa huko
 
Hawaambii chochote ni uchawi na ushetani tu wa baadhi ya wanawake, mtoto ambaye hajarogwa hawezi kumtenga baba yake.
 
Hii thread imenigusa sana. Kuna siku maza alinikalisha chini nakuanza kuniambia namna mshua alivyokua anazingua. Namna alivyokua mtu wa starehe sana kipindi cha ujana wake (hapo kabla sijazaliwa, maana nimezaliwa mdingi ameshavuka 40s huko).

Alifika mbali na kuniambia ninapopata chochote nisiwe namzingatia sana. Maana japokua baba ni mzee anaendekeza matumizi ya hovyo hasa kutuma tuma ela kwa ndugu zake.

Dah! Nilikaa chini nikaanza kufikiria. Yani nisimzingatie baba wakati alijinyima sana hata hakujenga nyumba nzuri kwa ajili ya kupambania elimu zetu watoto wake. Alipambana tukasoma shule nzuri na alikua mstari wa mbele kutukalipia pale tulipokua tunazingua kimasomo (mara nyingi kauli zake zilikua zinalenga tujipambanie tutoke kielimu ndio urithi pekee).

Mzee alijinyima sana hata hakua anapendeza na kuvaa nguo za fashion wakati ule anatusomesha. Nyakati za kulipa ada tulikua tunaona kabisa anavyochanganyikiwa kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa tunaenda shule. Na sasa umri umeenda sana, ameshastaafu, kutwa kulalamika maumivu ya kiuno, mgongo na macho kwa kazi ngumu alizokua anafanya wakati ule.

Eti ndio nimfungie vioo kisa mama kasema alikua anazingua ujanani! Hapana kwa kweli! Chochote nachokua nacho hua nahakikisha wananufaika wote bila kuwabagua. Hua najitahidi kua mfariji wa mzee wangu na anapokutwa na changamoto hua naitatua haraka sana.

Bado sijajua kwanini kina mama wengi wanakuaga wabinafsi sana na kupenda kuwalisha sumu watoto wawachukie baba zao. Inafikirisha sana.
Wapo Vijana Wachache Waliokuwa na Akili hizo
 
wanawake ni sumu kubwa katika maisha ya mwanaume,wanawalisha sumu watoto ingali wadogo, mzee aliyumba sasa ivi ukiwa na mkwanja mrefu .una jenga nyumba za kupangisha kama 50 baada ya hapo unatafuta mwanamke mwenye akili wa kuzaa naye ila sio wa kuoa full stop .hizo nyumba 50 zitakusaidia mpaka unaenda chini ,kwa kuwa mawe yatakuwepo utakuwa unagonga videmu kama kawa .watoto utawapa haki zao kila kitu.kuoa ni ufara afu ni uoga wa maisha kwanini upate ukichaa wa kujitakia? kataa ndoa ila zalisha masingo maza wawe wengi ili tupate utelezi wa bure
Bangi za wapi hizi? Wewe jamaa uko mzima kichwani? begi la pesa
 
Nyumba alimilikisha watoto ambao ndo hao wamemtelekeza kwa hiyo kwa sasa hana uwezo wa kufuatilia tena amekua na tatizo la ugonjwa wa akili na hili limetokea miezi michache baada ya kustaafu ndo mke nae akaanza hapo hapo ukatili dhidi ya mume wake kwa kushirikiana na hao watoto wake. Na pia mzee alikuwa na watoto wengi

Unaongelea mambo ya ndani usiyoyajua
Wanaume kuna umri mkiwa na nguvu huwa mna entertain michepuko na marafiki , mkishaishiwa nguvu mnajitilisha huruma kwa wake zenu.
Kanuni ni moja mwanamke anasamehe ila huwa hasahau kamwe.
 
Back
Top Bottom