Ukiona na kuamini mambo yanayozungumzwa Jf utaonekana tofauti sana mtaani na watu watakushangaa sana, sidhani kama utawahudumia wanao vyema kwa miaka na miaka halafu ukose hata mmoja tu wa kukushika mkono penye changamoto, labda unawazungumzia irresponsible fathers ambao hata humu tupo nao wengi,
Unakuta limtu limezaa zaa watoto huku na kule lakini halijui wanavaa nini, wanakula nini, wanachangamoto zipi,
Uzee ukishaliingia na limeishiwa nguvu linaanza kukumbuka kuwa mwaka fulani liliwahi nunua shati kwa mtoto eti hapo sasa ndo lilitoa huduma,
Ukiwekeza vyema kwa watoto wako Mungu ni mwaminifu hawezi kuacha jasho lako lipotee bure, hakuna mwanamke ukaishi nae vizuri akakugeuka, big no, acheni kupaka tope mama zetu kwa kisa kimoja cha mwanaume mpumbavu.
Mwisho kila mtu ajitafakari leo hii sa hii anaposoma hii comment, je anasimama kama baba kwa mtoto wake? Kama jibu ni hapana basi tegemea kuvuna ulichopanda.
Nawatetea wanawake, pamoja na mapungufu yao ila wanapitia changamoto nyingi sana.
Hapo mtaani kwenu kuna mamtu malevi,manyanyasaji ya wanawake tena mbele ya watoto.
Lingine pesa yake