Nimemuona kupitia TV (ITV) akiwa kwa Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje...tehtehtehtehWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imni Patterson ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.
Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.
Ubalozi wa Marekani wasisitiza maambukizi ya Corona jijini Dar yameshika kasi. Wadai Hospitali zimeelemewa! - JamiiForums
Ni maoni yako wewe
Mtu mwenyewe hajaangaika na mitanzania yeye ameamua kuwa alert watu wa nchi yake ambapo kimsingi ni jukumu lake la kwanza. Hapa serikali imefanya utopolo mtupu. Mimi namuunga mkono balozi maana kwa hilo tangazo lake na mimi naponea humo humo kwa kuendelea kuchukua tahadhari. Acha wanaoficha maradhi waendelee hivyo hivyo.
Mnaomba misaada ya kupambana na Corona huku mnasema mumeifuta! [emoji112][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]
hivi huyu king kinya anaishi Tz au Ughaibuni?[emoji16][emoji16][emoji16] View attachment 1460164
Mtazamo wako ni wa kiumaskini uliotopea!!! Somoni vijana muongeze ufahamu, elimu haina mwisho
Tunamghwaya kwa vipi...Mimi nimesomea International relations...ni miongoni mwa field zangu za kujidai...diplomacy...ndivyo ilivyo kote duniani..Tuna mgwaya
Sasa sijui wanaficha kitu ganiSisi tutaishia kutoa “masikitiko yetu” tu na ubalozi wataendelea kutoa travel advisory kwa raia wao ambazo kama Nchi hatuna mamlaka ya kuwazuia. Ukitaka kuepusha speculations, weka data hadharani
Kuandika makorokocho ni therapy nzuri...
Huyu Beberu anaenda kuhojiwa na Kabudi ana kwa ana alafu atashea taarifa ncini kwake kwa Mabeberu wakuuMabeberu this time wanahaha
Kataa misaada yao kwanza then ndio urudi kuongea hayo iran tuliona walikataa mpaka misaada ya corona.
Weusi wanaouawa na polisi sio raia wake?
Marekani gani inayojali raia wake?
Swali gumu hili usimuulize tena[emoji3]
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
Kama ubavu upo fungeni ubalozi wao. Hizi zingine ni mbwembwe tu na hazitobadili chochote.
Ndiyo maana mnapukutikaMababu waliishi vizuri hadi kutuzaa bila science.
Science gani ime work kwenye korona?
Muwekeni ndani huyo Kaimu Balozi au fungeni ubalozi wao kama jeuri ipo.
Kwa tafsiri ya matango poli ii amfurahishe mzee babaTuna Kabudi atatutafsiria
Hizo maiti zinazozikwa usiku hazina ndugu, majirani au rafiki? Au wewe una ndugu, jirani au rafiki aliyezikwa usiku. Subiri na wewe uzikwe usiku.Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
CIA waliosema rais wa korea kaskazini amekufa [emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app