Baada ya kuweka koma kwenye orodha ya kwanza ya Mawaziri, Rais Samia asema atatangaza orodha mpya karibuni

Baada ya kuweka koma kwenye orodha ya kwanza ya Mawaziri, Rais Samia asema atatangaza orodha mpya karibuni

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza hayo Ikulu Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19

Amesema "Nataka niwaambie nitatoa list mpya [ya mawaziri] karibuni. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi...nitakwenda nao. Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje."
 
Nchi yetu inahitaji service delivery sio mihemko hii ya kila wakati,my President please punguza cabinet yako to 15 minister's,hawa ni rahisi to manage them,sign them performance contract,ondoa RCs wote na bakisha wataalamu kuongoza idara chini ya RDD,hii itasaidia kupunguza matumizi ya serikali na kupeleka fedha nyingi za maendeleo hasa huku Lingusenguse ambako muda mrefu kumesahaulika kwa muda mrefu mno.
 
"Nataka niwaambie nitatoa list mpya [ya mawaziri] karibuni. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi...nitakwenda nao. Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje."- Rais Samia Suluhu
Ni hatua nzuri kwa sababu tutawajua wanaotaka kwenda 'kule' na tuwapime kama watafika ama la. Kikubwa wasiguswe mboni zao tu ! Ha ha ha haaaa!
 
Ninatabiri huyu kupewa wizara ile!
Lakini ni mchapa kazi!
EA9B6821-24E0-44F5-BAFD-8A9541C12281.jpeg
 
Rais kasema ana moyo wa Nyama sio glass.Inaonekana miongoni mwa waliopita kutoa salama wengine kawaona Kama wanafiki tu
 
Safi mama, tulikuwa tunalisubiri hili Kwa hamu, nchi hii ina watu wasiohitaji huruma, hawabebeki...Kama mbwai mbwai tu, watoe warudi kitaa waone Kama wataendelea kuota...huku huo usingizi tu hakuna.
 
Back
Top Bottom