Baada ya kuweka koma kwenye orodha ya kwanza ya Mawaziri, Rais Samia asema atatangaza orodha mpya karibuni

Ua nyani Mama,usitazame usoni, aheshimiwe anayejiheshimu tu, asiyejiheshimu tupa nje atakuharibia kazi.
 
Katiba mpya ingefanya haya yote
 
Hapa Majaliwa Majaliwa apishe wengine habari hio, atengeneze baraza lake aache kulalamika, akiacha kulalamika tutamsifia sana kwa maana hatuna chuki nae tunataka ajitambue ajue nini maana ya kuwa Rais, awe Mkomavu wa fikra na awe na maarifa na ufahamu wa mambo wa kutosha, asimamie makusanyo ya kodi awe makini kwenye matumizi, asiwe mwizi, awe na huruma kwa wananchi habari ya gharama za kuunganisha umeme? Samia apambane nchi hii Ikulu inaviatu vya jinsia ya Kiume hamna kisingizio
 
Mbona na yeye alishasema anautaka 2025.
Akishawatoa wenzake atajiuzuru ili naye akajitayarishe?
 
Wakuu heri ya mwaka mpya...

Kama tulivyo msikia Mama akisema kuwa hivi karibuni atafanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri
Je kwa mtazamo wako wakiutendaji kwa mawaziri hao
Je ni nani anafaa kubaki kwenye baraza ilo na ni nani anafaa kuondolewa kwenye baraza hilo

Aya twende kazi..
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Leo Jumanne Januari 04, 2022 ametoa tamko hilo thabiti la kuwa tayari ana listi yake mpya ya safu ya viongozi watarajiwa wanaoweza kufanya kazi naye bila kuwa na mambo ya vichwani mwao ya kugombea nafasi za uongozi.

Rais ametoa angalizo hilo wakati akipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Matumizi ya Fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.


Mh. Rais akasisitiza kuwa panga pangua hiyo inakuja baada ya kutambua viongozi wenzake baadhi yao wapo katika harakati kubwa kuwania uongozi na hivyo kukosa mwelekeo na utulivu wa kuchapa kazi ktk nafasi zao.

Hivyo Rais atachagua safu mpya ili wale wenye ndoto vya kuwania nafasi wawe nje wakajitayarishe vizuri na pia yeye Mh. Rais kuwa na safu mpya ya watu watakaokuwa wanachapa kazi za kutumikia wananchi kikamilifu bila mambo kibao ya kuwania uongozi.
Source : Global TV Online.
 
Samia mfia dini utaona atajaza waislam wenzake tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…