Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Achana nao kiongozi, siku zote huwezi kuungwa mkono/kupendwa na kila mtu,,,


Usione la ajabu,ni ukamilifu wa ubinadamu, hivyo jikubali as long as ulieleza hisia zako juu ya suala hilo, uwepo wao pia sio wa kubezwa, walifanya uzi wako ufuatilie na wengi.

Wasamehe!!
Kweli mkuu sina kinyongo nao.
Kikubwa wajifunze
 
MWAMA.jpg


AUAE KWA UPANGA, ATAKUFA KWA UPANGA!

"Kila auae kwa upanga, naye ataangamia kwa upanga" (Mathayo 26:52)! Hayo ndiyo maneno ambayo Yesu alimwambia Mtume Petro usiku wa Alhamisi Kuu. Hiyo ni kanuni ya kiroho! Upanga katika Biblia ni ishara ya mamlaka. Mtu ye yote aliyekabidhiwa mamlaka hatakiwi kuitumia mamlaka yake vibaya kwa kutesa, kufedhehesha, kunyanyasa, kuharibu, kunyamazisha, kupora, na hata kuua wengine. Akifanya hivyo, na yeye atakuja kufanyiwa hivyo hivyo na mamlaka nyingine iwe ya kidunia au ya Mungu moja kwa moja! Ninawatakia tafakuri njema ya Ijumaa Kuu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Habari zilizo teka mitandao na nje ya mitandao ni taarifa ya vifurushi vilivyo badilishwa.
Hii ilinilazimu kuandaa uzi maalumu usemao Tanzania tupaze sauti kupinga mfumo wa vifurushi vipya
Kwa namna moja au nyingine nilionekana kama naropoka tu.
Lakini siku ya leo mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wameliona hilo na kuja na taarifa hizi👇
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.



Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.



“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.



Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.


Sauti yetu imesikika.

Hebu acheni Upuuzi wenu na kutaka kuwapa Sifa ( Kiki ) za Kipumbavu hawa TCRA wenu.

Hivi anayesikia Kilio anatakuwa azuie ( arekebishe ) Jambo kabla halijawa katika Utekelezaji wake au anaruhusu litokee kisha likishawaumiza wengi ndiyo anajifanya Kujitokeza Kukutetea?

Msidhani Watanzania ni Wapuuzi hivyo.
 
Hebu acheni Upuuzi wenu na kutaka kuwapa Sifa ( Kiki ) za Kipumbavu hawa TCRA wenu.

Hivi anayesikia Kilio anatakuwa azuie ( arekebishe ) Jambo kabla halijawa katika Utekelezaji wake au anaruhusu litokee kisha likishawaumiza wengi ndiyo anajifanya Kujitokeza Kukutetea?

Msidhani Watanzania ni Wapuuzi hivyo.
maendeleo hayana chama, polepole tutafika
 
Kwa hili kosa ilitakiwa Dr Faustine Ndugulile ajiuzulu mara moja kwa kudanganya umma ,alishupalia kwamba gharama zitashuka za data kutoka sijui Tsh 50 hadi 2 mpaka 9 Tsh ,cha ajabu gharama zime double , yaani 1000 napata MB 350??? 10000 GB 4 kutoka GB 12? TCRA inabidi wakusanye maoni upya maana tunarudi nyuma ,nchi nyingi gharama za internet zipo chini sana ila huku wanazidisha.

Na pia wasiangalie gaharama kubwa za data ,waangalie pia Mobile Money ,tozo za kutuma na kutoa pesa ni kubwa sana ,kila siku tunaona makampuni wanatoa records zao za faida kwa kuwakamua wananchi...imagine voda inaingiza mabilioni ya shillingi kwa mwezi kutoka kwenye Mpesa yaani wanatengeneza faida maradufu kwenye Mpesa,why TCRA wasi regulate faida kama EWURA wanavyoregulate price ya mafuta? How Mpesa waingize faidi ya zaidi ya bilioni 15 kwa mwezi? Huo si wizi? Kwanini gharama za kutuma na kutoa wasipunguze?
Usilogwe kuhamisha hela kutoka Bank kwenda mitandao ya simu and Vice versa. Ni balaa
 
Nilisema tupige kelele juu ya swala hili, wachache waliunga mkono na wengine kusema kasomi umechanganyikiwa.
Kidogo kidogo tutaelewana
 
Back
Top Bottom