Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.

Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.

Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.

“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.

Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
 
Habari.

Habari ya muda huu inayosambaa kwa sasa ni serikali kusitisha bei mpya ya vifurushi vilivyotangazwa na mitandao husika mwanzo wa mwezi huu.

Na imani yatakuwa maamuzi bora na itakuwa habari njema kwa wananchi.

Nawasilisha Mzee Mkoloni

Cc: Kichwa Kichafu.
 
20210402212203.jpg
 
Samia safiiiiii...mama la mama safiiiii??

Nilijua tu, waziri wa teknolojia wa saivi ni wa hovyo kuwahi kutokea ...na sijui kwanini mama la mama amemuacha, ila nina imani na mama hii product ya kipuuzi ataitupilia mbali
 
Hahaha.. nimejaribu kila line niliyonayo kutafuta kifurushi chenye unafuu awapi!

Ule mkongo wa taifa unatusaidiaje sasa!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimeifufuaa ttcl nako nakuta kama wengine japo wanatamba kuwa wao wako kama mwanzo
 
Back
Top Bottom