Niulize, hivi ofisi ya msajili haina watu walioelimika wanaoweza kuandika summary
Pili, msajili ametokea wapi , mbona hatumsikia mtumishi wa umma wa TISS kuvaa nguo za CCM
Yule mwenyekiti wa uvccm aliyesema watu wauawe , Jaji Msajili hakuona hatari leo anaona hatari ya 'kufa na kupona'' . Huyu ni Jaji anayepaswa kujua tishio na msemo. Jaji !!
Tatu, msajili kaiubuki wapi wakati CCM wakiruhusiwa kufanya kampeni wenyewe.
Huyu msajili ni Jaji kitaaluma, na hapa kuna maswali mengi sana kuhusu yeye na sheria nchini zama hizi
Huyu ni jaji kumbukeni na ni yule yule aliyechagiza mgogoro wa CUF bila kujali sheria akiwa mtu wa sheria. Shame
Kitu kimoja wasichojua, kule Tanga kuna msemo usemao ''kuchamba kwingi kuondoka..''
Mambo kama haya yanaliweka Taifa katika uso wa dunia. Hadi sasa dunia inaianalia Tanzania kwa jicho la mashaka
Kuendelea kujipendekeza kwenu kunaiweka serikali katika wakati mgumu sana
Jaribu kufuta ACT Wazalendo kama vikwazo vya kimataifa havitaingia Tanzania.
Jaribuni mtaona matokeo yake ! Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kila nyendo it's a matter of time, sasa wapeni sababu.