Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe alitangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo

Mchakato wa Membe ulianza zaidi ya miezi minne iliyopita huku serikali ikifuatilia kwa karibu...
Mie naona nguvu ya Maalim kule Zanzibar ndio chanzo cha yote
 
Nimeisoma maelezo ya barua hii mpaka karibu kufikia mwisho, honestly sijaona sababu genuine zaidi tu ya vijisababu vya kuokoteza....

Mfano;

1. Kauli kama "uchaguzi wa mwaka huu 2020 utakuwa ni wa kufa na kupona" haiwezi kuwa na maana ile msajili anayoilazimisha iwe ndiyo maana. Hiyo ni tafsiri yake yeye ili ku - suit interest yake za kutaka kuhalalisha anachotaka kufanya huku ikiwa haina "locus stand" ya uhalali kisheri. Lakini mzungumzaji ndiye anajua alitumia katika muktadha gani.

Mfano, mimi nnaweza kusema hivi; ".....mwaka huu ni wa kufa na kupona ktk biashara zangu kuhakikisha zinatoa faida inayoeleweka...".

Msajili atueleze, je kwa mimi kutamka hivi inakuwa na maana ya kuhamasisha vurugu kwenye bashara za watu wengine??

2. Kauli ya maalimu Seif kuwataka wananchama wa ACT Wazalendo kwenda kulinda ofisi zao kwa nguvu zote bila kuchoka kwa kutumia silaha za jadi kama shoka, panga nk inawezaje kuwa ni kosa?

Kuna kosa gani mtu kulinda mali yake kwa kutumia silaha yoyote aliyonayo?

Kama msajili nyumbani kwake anajilinda kwa bunduki na bastola ni kwa sababu ana uwezo kununua na kumiliki silaha hizo.

Je, wasio na silaha hizo wajilinde kwa kutumia silaha gani eti? Ni kosa kisheria mtu kujilinda?

What's wrong with this msajili wa vyama vya siasa???

## Nimesoma ujinga huu mpaka nikachoka kabisa na kuona kumbe watu wanalazimisha fujo na vurugu ktk nchi hii bila sababu yoyote ya msingi.

Ni eti tu CCM na Magufuli wao wasipate ushindani ktk uchaguzi huu.

Hivi inawezekanaje mtu (Magufuli) ambaye kila siku na kila mahali anapata promotion ya SIFA na NYIMBO na hata kuitwa "YESU wa CCM" kumhusu yeye kwa "YANAYOITWA MAZURI ALIYOFANYA" awe anaogopa ushindani ktk uchaguzi wa wazi na huru wakati yapo mazuri yanayombeba..!!????

Hivi iweje mtu ambaye amefanya MAKUBWA na MAZURI ambayo dunia haijawahi kuyaona aogope ushindani toka kwa watu ambao hawajafanya lolote??

Ukiona hivi ndiyo mjue kuwa, yote yanayosemwa juu ya sifa na utukufu wa mtu huyu aitwaye Magufuli wa CCM ni upupu mtupu...

Na ndiyo mjue kuwa kumbe ni kweli kabisa CHEMA CHAJIUZA na KIBAYA (MAGUFULI na CCM) CHAJITEMBEZA KUCHA KUTWA ILI KIUZIKE...!!!
 
Ngoma ikivuma sana hutaka kupasuka. Kwa kuwa waliopewa mamlaka badala ya kutumia weledi wenye kuzingatia maadili na uadilifu ndani ya kazi zao, wanageuka kuwa nia mbovu. Imefika wakati ambapo mbeleko la chama dola linaanza kuchanika.

Zanzibar mwaka huu hakutakuwa na utulivu wowote ule endapo matokeo ya kura za wananchi yatakaposhindwa kuheshimiwa. Na sasa huku Bara napo wanaanza kutikisa kwa makusudi kibiriti. Jukumu la kuilinda amani ya nchi yetu si la wana CCM pekee yao, bali ni la wananchi wote.

Kamwe tusifananishe utulivu na amani. Utulivu ambao hutokana na hofu ya watu ktk kukabiliana na vyombo vya dola hata kama wanaonewa na haki zao kupuuzwa. Kwa kuwa hata wafungwa pale wanapokuwa korokoroni ndani ya kuta za magereza, nao pia huwa na utulivu kutokana na mazingira, bali hukosa kabisa amani mioyoni mwao.
 
Yaani bila aibu mtu mwenye dhamana kubwa anatoa sababu ambazo hata kwenye michezo ya watoto hazipo. Msajili anataka kukiadhibu chama kwa sababu viongozi walihamasisha wanachama kusimamia haki za chama chao? Chama kulinda mali (ofisi) zake ? Ndio maana siku zote naamini kwamba wanao ilinda amani ya nchi ni viongozi wa upinzani.
 
Akifutie kwa kosa gani hasa?
Duh, yaani huoni makosa kweli au kipofu wa akili! Huyu msajiri mbona anapodoapodoa Sana!? Hebu kifutilie mbali ili liwe fundisho kwa kanjanja wote na ukuwadi wao kwa mabeberu! Wengine tunayo nchi hii tu ya Tz! Hawa wenye urais wa DRC, Oman, na Canada wasituvuluge Bali tuwAvuluge wa
 
Niulize, hivi ofisi ya msajili haina watu walioelimika wanaoweza kuandika summary

Pili, msajili ametokea wapi , mbona hatumsikia mtumishi wa umma wa TISS kuvaa nguo za CCM

Yule mwenyekiti wa uvccm aliyesema watu wauawe , Jaji Msajili hakuona hatari leo anaona hatari ya 'kufa na kupona'' . Huyu ni Jaji anayepaswa kujua tishio na msemo. Jaji !!

Tatu, msajili kaiubuki wapi wakati CCM wakiruhusiwa kufanya kampeni wenyewe.

Huyu msajili ni Jaji kitaaluma, na hapa kuna maswali mengi sana kuhusu yeye na sheria nchini zama hizi
Huyu ni jaji kumbukeni na ni yule yule aliyechagiza mgogoro wa CUF bila kujali sheria akiwa mtu wa sheria. Shame

Kitu kimoja wasichojua, kule Tanga kuna msemo usemao ''kuchamba kwingi kuondoka..''
Mambo kama haya yanaliweka Taifa katika uso wa dunia. Hadi sasa dunia inaianalia Tanzania kwa jicho la mashaka
Kuendelea kujipendekeza kwenu kunaiweka serikali katika wakati mgumu sana

Jaribu kufuta ACT Wazalendo kama vikwazo vya kimataifa havitaingia Tanzania.
Jaribuni mtaona matokeo yake ! Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kila nyendo it's a matter of time, sasa wapeni sababu.
 
Kwanini iwe Sasa? Msajili acha kuegemea upande mmoja. Bora msajili angetoka asasi za kiraia
 
Back
Top Bottom