Baada ya Mwandishi Manyerere Jacton kueleza kinachoendelea Ngorongoro, sasa ndio naiamini Serikali, Wanahama kwa Hiyari

Update

Kuona ni kuamini, mkisikia maendeleo ya kweli, sasa ndio haya!.
P
 
Tuwekee video na daily updates.
Mkuu Ralph Tyler , asante sana kwa ushauri huu, umetekelezwa nimeweka update. Wamefika salama Handeni.

Kuona ni kuamini, mkisikia maendeleo ya kweli, sasa ndio haya!.
P
 
Mkuu, Naskia ulipata degree baada ya miaka 10, embu fafanua kudogo ilikuwaje
Mkuu mbobezi11 , it's true tena to be precise ni after 15 years!. Elimu haina mwisho na haina muda. Wengine husoma kwa miaka 3, na sisi wengine ndio kama hivyo, miaka 15. NB. Naomba tujifunze kujadili hoja iliyopo mezani, kusoma kwangu na ku graduate after 15 years, have got nothing to do with hoja iliyopo mezani.
Karibu mitaa hii Hatimaye ndugu yetu Pascal Mayala amehitimu UDSM
P
 
Hako kamgogoro kanachochewa na inchi fulani. Unajua juhudi za rais kutafuta wawekezaji zinayakera baadhi ya mataifa jirani hapa East Africa.

Na hii ndo vita ya uchumi
Mkuu Morogoro kaskazini , ni kweli kabisa, hawa ni jirani zetu tunaogombania nao Utalii wa Kaskazini, Royo Tua imewatia wazimu!. Ila kitu cha ajabu kabisa, kuna baadhi ya wenzetu wanawasupport majirani hawa wasio tutakia mema!. Kiukweli hawa wenzetu wasiolitakia mema taifa letu, ni mamluki hawa.
P
 

Ngorongoro wanahama kwa hiyari, bila shinikizo lolote na bila ya vurugu zozote.
Kaka, naomba kuuliza, hivi kuna kuondoka kwa hiari bila ya kuwa na kishawishi au shinikizo lolote?

Haiingii akilini mwangu kuwa hawa wamasai waliamka tu na kudai kuhamishwa, tena kwa hiari!
Haiingii akilini kuwa hakuna shinikizo lolote.

Toka nimeanza kuzisikia hizi habari za Watanzania wenzangu, wana jamii wa Kimasai, sijawahi ona pale kulipotokea makubaliano(mkutano) wa Jamii hii kuomba Serikalini au popote pale kuwa wanataka kuhama kwenye ardhi ambayo wamekaa na kuishi kwa Karne...as a matter of fact, sijawahi kusikia Jamii yeyote Duniani inayoomba kuondoka katika maeneo yao(ancestoral) kwa madai yeyote iwe kwa janga, vita n.k kwa Hiari hata kukiwa na vishinikizo vya makali ya majanga kama hayo niliyoyataja ....I am ready to be corrected.

Naomba kuelimishwa.

Manyerere akiwa Ngorongoro, ameeleza jinsi anavyoshudia wakazi wa familia 20 za mwanzo, huko Ngorongoro zinavyohamishwa kutoka Ngorongoro na kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga.
Wabarikiwe na mwenyezi mungu awaonyeshe njia.
Wananchi hao pia wamehojiwa na kuuthibisha uhiari wao na kueleza mategemeo yao. Manyerere ataandamana nao hadi mwisho wa safari yao

Je safari hii alianza nao lini...kabla au baada ya taarifa za taharuki. Siwezi kataa kuwa "walihojiwa" ila tu....hayo ya kuelezea "Mategemeo" yao tungepata kufahamu, itakuwa vizuri...Wana mategemeo gani huko wanapoenda baada ya....?
Kunapotokea sintofahamu yoyote kati ya serikali na jamii, ni vema sana kutumia an independent media na Kuwatumia independent journalists wanaaminika zaidi na jamii kuliko maofisa wa serikali.
Naamini michango mikubwa ya Waandishi wa Habari popote pale, na hasa kama kwa mfano uliotumia, lakini hilo halisemi kuwa hana pande? Je alienda huko kuhakiki taarifa za vurugu pekee? Je kulikuwa na uvunjwaji wa sheria kwa pande zote?
Hivyo sasa nawaomba tuiaminie serikali yetu, wakazi wa Ngorongoro wanahama kwa hiyari hakuna kulazimishwa kokote wala shinikizo lolote.
Kwa hilo hapo juu, nitakataa kuamini kwa moyo wote(sijaridhika) kwa sababu tu bado kuna sintofahamu, binafsi naona hivyo.
Ahsante.
P....Nimekurupuka kwa hili na kuna uwezekano kuna maelezo zaidi huko juu.
...na bila kusahau Una haki zote za kuwa na mtazamo huo.
 
Maghu alikuwa ameishakufa,macho makavu kabisa serikali ikaendelea kutuambia JPM yupo ofcn anachapa kazi.
Samaki wamekufa mto mara,tukapewa ripoti na profesa wa majararani kuwa kinyesi Cha ngombe ndio chanzo Cha vifo vya samaki
 
Kwani hao wa ubeberuni ndiyo hawako biased? Angalia propaganda zao kwenye vyombo vya habari vya magharibi kuhusu vita vya Ukraine ndiyo utajua hao unaowasifia hawana lolote.
Hoja hapa ni Wamasai wa Loliondo. Tukiwatumia waandishi wa kujitegemea kutoka Nchi za dunia ya kwanza, walau tutaweza kupata unfiltered story kuliko hawa waandishi wenye kadi za ccm akina Pasco na wenzake
 
Huyo jamaa ana IDs zake tano zote zimepigwa ban ndiyo juzi akafungua hii mpya,kazi yake kubwa ni kutibua mijadala kwa kuhusisha watu au mada ambazo hazihusiana na mjadala uliopo mezani
 
Na jana waziri wa mambo ya ndani katoa maelekezo kwa askari wa uhamiaji kuto ruhusu watu kutoka inje ya inchi kuingia ingia hovyo ndani ya eneo hilo
 
Njaa zinawasumbua hao mamluki hakuna kingine. Hiyo ni move ya kisayansi yenye nia ya kuipaisha Tanzania.
 
Hoja hapa ni Wamasai wa Loliondo. Tukiwatumia waandishi wa kujitegemea kutoka Nchi za dunia ya kwanza, walau tutaweza kupata unfiltered story kuliko hawa waandishi wenye kadi za ccm akina Pasco na wenzake
Nadhani una tatizo la kuelewa. Ninachosema ni kwamba, hata hao waandishi kutoka nchi za ubeberuni pia wana bias zao, watakuandikia story kwa kuduata interests zao. Mfano ni jinsi wanavyoandika kuhusu vita ya Ukraine.
 
Wakenya wanatuma masai na migolole yao kuja kuharibu mbuga ili nyumbu wakienda Masai Mara wasirudi Tizii
 
Vile serikali huwa inajibu linapokuja suala la wamasai😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Huyo comred wako pia ni njaa tu
 
We jamaa una matatizo sana. Manyerere ni mwanaccm nani wa kumuaamini?
Mkuu Muuza Kangala , acha mambo ya kwenye kilabu cha kangala, kwani mtu ukiwa CCM ndio huaminiki?. Mimi mwenyewe sio tuu ni mwana CCM, bali pia ni kada mwaminifu wa chama cha Mapinduzi, CCM, na ni mtu wa kuaminika.
Kiukweli humu JF, sisi CCM, tunaonewa sana!. Niliwahi kuuliza Je, mtu kujiunga CCM ni ujinga? Je, wana CCM ni wajinga? Je, watanzania wanaoichagua CCM, kila uchao ni wajinga? Its not fair
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…